Mkurugenzi Mkuu TCRA Dkt. Jabiri Bakar asisitiza Postal code ni suluhisho la utoaji huduma kwa wananchi

PendoLyimo

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2014
Posts
969
Reaction score
1,055
"POSTAL CODE" NI SULUHISHO LA UTOAJI HUDUMA KWA WANANCHI

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imefanya semina kwa watoa huduma za Posta leo oktoba 7, Jijini Dodoma katika kuelekea maadhimisho ya siku ya Posta duniani. Akizungumza na Waandishi wa habari Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano amesema kuwa kazi kubwa ya Mamlaka ya Mawasiliano kusimamia watoa huduma za Mawasiliano ikiwemo Posta, utangazaji na mawasiliano ya simu

" Sisi kama TCRA jukumu letu kubwa kuhakikisha "Postal code" zinawekwa kwa kuzingatia taratibu za kimataifa ili hata mtoa huduma wa kimataifa asipate changamoto wakati wa kutoa huduma kwa Wananchi kwa kutumia mfumo wa "Postal Code" - Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Jabir Bakari

"Kukamilika kwa huduma ya "Postal code" itasaidia sana kutatua changamoto za upatikanaji wa huduma kwa wananchi katika kipindi hiki cha UVIKO 19 na wakati wa majanga mengine Mwananchi atapata huduma akiwa nyumbani kwake kwa kutumia mfumo wa kidijitali utakao saidiwa na mfumo wa Postal code - Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Jabir Bakari

Pia katika kuadhimisha siku ya Posta Duniani Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inawakumbusha watoa huduma wote kuzigatia taratibu na Kanuni zinazokubalika na Mamlaka katika kutoa huduma bora kwa wananchi

#SikuYaPostaDuniani

#UbunifuKwaPostaEndelevu
 
Posta inasaidia nini kwenye maisha ya watu, yaani mnaletewa vimiradi vya upigaji mnaacha kutumia akili zenu mnashadadiiiia posta yenyewe ishakufa duniani watu wako kidijitali zaidi, hapo hamna kitu hapo ni hewa tu.
 
Mkuu umesoma content au umeishia kwenye kichwa cha habari. Kiwango chako cha elimu ni kidogo sana!
 
Wewe mwenye elimu kubwa ndio unashadadia post codes kwenye nchi hii ambayo bado mnasomea nje chini ya miti? una matatizo makubwa sana ila hujijui tu, hatujielewi ndiomaana tuko hapa tunaenda tunarudi
 
Kwani zoezi la sensa SI litatoa hizi postal code au Mimi ndo sikumwelewa afisa aliyefanya majaribio kwenye makazi yangu
 
Sasa mtu anakwambia hii inaleta maendeleo, ujue aliyeturoga ameshakufa siku nyingi sana
... kuna kaukweli Mkuu! Miongoni mwa vitu muhimu ili kumletea mwananchi maendeleo ni kumtambua (ID); kujua yuko wapi (postal code); n.k. ili apatiwe huduma kwa urahisi. Ila kumbuka hakuna HAKI bila WAJIBU, zingatia sana hayo maneno mawili hususan WAJIBU (kulipa kodi, etc. etc. etc.).
 
Postal code ndio nini wakuu.
Assume X ameagiza kifurushi kutoka China anachotaka kusafirisha kwa postahadi Dar , na anwani ameandika P.O. Box 1578 Dar es salaam, labda na namba ya simu.

Kama ilivyo kwa X, Y nae ameagiza kutoka China lakini fomu ya anwani, amejaza Postal Code 14107, Dar es salaam.

Sasa, kwa uandishi wa aina hiyo, mzigo wa X utafikia Posta, na kama ni Posta Mpya, basi X itabidi akaufuate mzigo wake hapo Posta Mpya.

Kinyume chake, Y ameandika 14107, hapo inajulikana moja kwa moja kwamba 14 ni postal code ya Wilaya ya Kinondoni, na 107 ni postal code ya Makumbusho, na kwahiyo badala ya mzigo kuishia Posta Mpya, huu wa Y utafikishwa hadi Makumbusho, na anaweza kuletewa hadi mlangoni au ataufuata Posta Makumbusho!

So, kwa lugha nyepesi, Postal Code inatumika for package delivery to the nearest possible area. Hizi Postal Codes zimefikishwa hadi vijijini, kwahiyo kama mtu uliandika postal code ya Nanjilinji, kifurushi/barua haitaishia mjini bali itapelekwa hadi Nanjilini.

Hata wewe unaweza kufunga mzigo wako kutoka Dar hadi Njombe vijijini huko, na unaandika Postal Code ya huko vijijini! So, mzigo ukifikia Njombe Mjini, Postal ya Njombe utaisafirisha hadi kijiji husika (as of now, codes zetu zinaishia kwenye ngazi ya kata)
 
Kama DHL au EMS wanakueleza uende ukapokee mizigo yako au barua ofisini mwao wakati umeweka namba ya simu au unakuta kikaratasi katika sanduku la posta, hiyo postcode itafanikiwa? Tatizo ni uwajibikaji wa watu wetu
 
Mkuu Chige ,kongole kwa ufafanuzi rahisi lakini unaoeleweka vyema.
Kuna watu Mungu amewapa vipawa kama wewe na hiki cha kufafanua mambo kwa lugha rahisi na inayoeleweka vyema, vitumieni vipawa vyenu ili Mungu atukuzwe kupitia kwenu.
Ubarikiwe sana mkuu.
 
Watanzania wanaongoza kwa USAFI wa fikra nikipata Urais nitahakikisha WATANZANIA WOTE hasa WAANDISHI WA HABARI, WATU WA USTAWI WA JAMII wanazimiliki lengo muwe na story zinazofanana NJE ya nchi na Ndani ya NCHI – BORA hazifanani kabisa zina maana kwenye SEKTA YA UJENZI

Serikali haijafikiria kuwafirisi maana siyo kuwaza barabara, hospitali, flyover!?

andika kwa kiswahili labda nitakuelewa.
 
Mkuu Chige ,kongole kwa ufafanuzi rahisi lakini unaoeleweka vyema.
Kuna watu Mungu amewapa vipawa kama wewe na hiki cha kufafanua mambo kwa lugha rahisi na inayoeleweka vyema, vitumieni vipawa vyenu ili Mungu atukuzwe kupitia kwenu.
Ubarikiwe sana mkuu.
Much respect Mkuu Residentura...
 
Kama DHL au EMS wanakueleza uende ukapokee mizigo yako au barua ofisini mwao wakati umeweka namba ya simu au unakuta kikaratasi katika sanduku la posta, hiyo postcode itafanikiwa? Tatizo ni uwajibikaji wa watu wetu
Tatizo la uwajibikaji wa taasisi moja haifanyi taasisi nyingine iache kuwajibika kwa upande wake.

Suala la DHL na hao wengine kushindwa kuwajibika haiwezi kuwa sababu ya kuwafanya TCRA nao wasiwajinike kwa upande wao kwa kutoa postal codes, na elimu ya namna gani postal codes zinaweza kutumika ili kurahisisha package delivery.

Na pia ukumbuke kwamba, changamoto kubwa kwa Bongo ni physical addresses, na ndo maana zoezi la postal codes linaenda sambasamba na ku-name mitaa kule ambako inawezekana kufanya hivyo!! Lakini kwa upande mwingine, je unayo DHL Account inayotaja physical address ya unapoishi au kufanyia kazi?

That's one but two, umeshasema mzigo umefikia DHL na umeandika number ya simu... je, namba ya simu inatambulisha physical address?! Kama haioneshi, unatarajia nini zaidi ya kupigiwa simu kwamba ufuate kifurushi ofisini!!

On top of that, baada ya kupigiwa simu kwamba ufuate ofisini, na unapoishi au ofisini kwako kuna physical address, unashindwa nini kuwaambia wakuletee mzigo wako ofisini au nyumbani kwako?!

Kushindwa kuwajibika kwao kusikufanye wewe kama wewe uache ku-demand haki yako!! Ikiwa siku hizi unanunua bidhaa Instagram na mtu ukamwambia akuletee mzigo hadi mlangoni, na akafanya hivyo, kwanini usiwaambie DHL hivyo hivyo ikiwa service uliyolipia ni home/office deliverly?
 
Back
Top Bottom