Mkurugenzi Mkuu VETA: Hata wenye PhD wanakaribishwa VETA

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Anthony Kasore amesema kuwa sio tu wenye Shahada ya Awali, hata wenye elimu za juu zaidi kama vile Shahada ya Uzamivu (PhD) wanaweza kujiunga VETA, na wamewahi kuwa na mwanafunzi mwenye PhD ambaye amesomea masuala ya uchomeleaji.

Soma: Waziri Mkuu Majaliwa: Wenye degree kasomeni ufundi VETA mjiajiri

Akizungunza kwenye Kipindi cha Jambo Tanzania cha TBC1 leo Machi 17, 2025, Kasore amesema Serikali imeendelea kuboresha huduma za elimu ya ufundi hasa miundombinu na kuwahimiza watu wote wanaohitaji kupata ujuzi wajiunge na vyuo vya VETA vinavyopatikana katika maeneo mbalimbali nchini.

Reducing this important debate to meme. What a missed opportunity?!

1. Is it not a time for DIT, Moshi tech and the likes get back to their original course? Is it not a critical moment of maintaining pyramid education system that creates fewer administrators like we used before?
2. How do we mobilize and direct our university colleges towards this new direction?
2. How do we link the compulsory JKT training effectively from this or next year towards this new direction?
3. ⁠How do we assist graduates who wish to pursue VET training in response to the PM’s suggestion/advice?

These could be issues to discuss and reposition our young population to new realities in a well thought manner
 
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Anthony Kasore amesema kuwa sio tu wenye Shahada ya Awali, hata wenye elimu za juu zaidi kama vile Shahada ya Uzamivu (PhD) wanaweza kujiunga VETA, na wamewahi kuwa na mwanafunzi mwenye PhD ambaye amesomea masuala ya uchomeleaji.

Soma: Waziri Mkuu Majaliwa: Wenye degree kasomeni ufundi VETA mjiajiri

Akizungunza kwenye Kipindi cha Jambo Tanzania cha TBC1 leo Machi 17, 2025, Kasore amesema Serikali imeendelea kuboresha huduma za elimu ya ufundi hasa miundombinu na kuwahimiza watu wote wanaohitaji kupata ujuzi wajiunge na vyuo vya VETA vinavyopatikana katika maeneo mbalimbali nchini.

Yaani hata huyu, nae anaenda kichawa chawa kama, kasuku, kama msomi, ilibidi afafanue wahitimu wa vyuo vikuu waende veta kusoma nini?
Je kijana aliyehitimu degree ya statistics, anaenda veta kupata uzoefu wa takwimu, au aende akajifunze kutengeneza keki na batiki! Ajiajiri,aajiliwe, wakati anasubili kazi, ya degree aliyosomea? Au, Dokta kasoma miaka 6,anakuja veta kupata internship ya u dokta, au, anakuja kujifunza udereva, kutengeneza tiles, kupaka rangi,harafu aingie kitaa apige kazi na asahau kabisa Mambo ya u dokta?
 
Eti akabadili fani kwa mwamvuli wa kuongezea ufundi e.g. awe ni dokta anayepika keki au kuwaremba maharusi n.k. au
 
Ujinga wa veta eti lazima uvae uniform, hawana evining program. Mtimish ningumu kusoma kozi za veta hasa za serikali.
 
Aibu naiona mimi Tanzania, kutoka zama za Specialization mpaka zama za ujima wa Jack of all traders. Yaani mtu usome mpaka PHD alafu uende Veta ? Kwann asingemaliza la nne akaenda Veta ?

Dunia ya sasa inalazimisha uwe na Taaluma angalau 2 au hata zaidi,- ukimudu.

Iwapo hilo hulijui na unalishangaa, shukuru Mungu sasa unafunguliwa macho tena bila malipo.
Na ukweli ni kuwa umechelewa.

Bahati mbaya tumekaririshwa na kuaminishwa kuwa Taaluma moja hasa ikiwa ni hizo za juu kama uliyoitaja ndio baaasi, mbaya sana hii.

Huko kunakoitwa Dunia ya kwanza,
Watu kuwa na Taaluma 3 sikuhizi ni kitu cha Kawaida, tena sana.
Na kama ni 'Certifications' zinakuwepo na wanaweza kuzifanyia Kazi kutegemeana na ratiba zao
(sio ujanjaujanja)

Kuweka mjadala juu ya iwapo ni sahihi ama lah kuhusu hoja hii,
Inatutofautisha wenye mawazo ya kisasa dhidi ya wanaofikiri kwa mrengo wa Karne ya 18.

Nawasilisha.
 
Tustick na Tanzania ambayo tumekosa ma specialist wa vitu vingi kiasi kwamba hata consultancy kubwa zinafanywa na makampuni ya nje...baadala ya kufight kuwa na specialist wengi tunaforce kuwa na wana Veta wengi
 
Joanah mahi twende VETA tukajifunze mapishi, si unajua mimi na wewe kupika hatujui 😹😹😹
 
Back
Top Bottom