Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) ana mtihani mkubwa sana akifanikisha hili anastahili tuzo

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) ana mtihani mkubwa sana akifanikisha hili anastahili tuzo

Japo anaelipa ni Mwananchi laiki iyo 18% ya VAT mfanyabiashara hataki kuiwasilisha TRA.
hataki kuiwasilisha vipi tena? TRA hawalazi damu wanatembea vyema na report
 
Nakuelewa vizuri lakini kumbuka bila nchi kukusanya kodi inayotoshereza haiwezi kwenda!
Hilo lipo wazi kabisa. Shida ni hiyo kodi inakusanywaje. Poor tax administration.
 
Shida huwa hatuna uhiali wa kulipa kodi
Si unakumbuka hata kipindi cha JK na Mkapa kodi ilikusanywa pia? Na ioiongezeka pakubwa katika vipindi vyao? Lakini biashara hazikufungwa.
 
Wengine wanachanganya kati ya kodi na madeni ya kodi ambayo ilishakuwa established awali.

Zile nyingi ilisemekana kuwa Tax arrears.

Zilipoisha ndipo ikabidi wajiongeze kwa hizo mbinu nyingine [emoji3][emoji3]
 
Upande mmoja anatakiwa atumie akili na hekima kukusanya kukusanya kodi kwa maelekezo ya Rais.

Upande wa pili ni lengo la trilioni 2 kwa mwezi kwa maelekezo ya Makamu wa Rais.

My take:
Siku zote mfanyabiashara lengo lake ni kutengeneza faida kubwa hapa naongelea "Big potatoes" au wafanyabiashara wakubwa ambao kila kitu wakichuma Tanzania wanapeleka kwenye account zao Canada/Ulaya.

Wafanyabiashara wa jamii ya Asia ni wajanja sana na wengi wao hawana uchungu na nchi yetu maana sio RAIA hawana hata kiwanja cha 20*20 hapa kwetu. Bado kuna makampuni makubwa yanayodai kila mwaka yanaingiza hasara ila hayafungi biashara au kuacha kuchimba madini.

Bado kuna ujanja wa kubadili majina ya kampuni baada ya grace period ya kodi kuisha. Wafanya biashara ni wajanja mno. Muhindi anaingiza mzigo kutoka China anausambaza kwenye store zaidi ya tano kisha dukani anaweka kamzigo kadogo ukienda kumkadiria kodi anajikuta analipa laki 1 kwa mwezi sawa na mtumishi kwenye salary ya laki 7.

Ukiweza kutimiza malengo haya yote mawili kwa ukamilifu, kwangu mimi wewe utakuwa mkurugenzi bora Tanzania.

"KAZI IENDELEE"
Swala la kubadili jina la kampuni ni ngumu kulizua hata wakati wa JPM hiyo njia iliendelea kutumika maana kisheria mfanyabiashara anakwambia amefirisika unamlazimishaje kwamba hajafirisika utampa mtaji ili asifunge Hilo jina la biashara......wakati wa JK alikusanga 900bil magufuli alitikia 1.3tril ambayo ikaanza kushuka baada ya miaka miwili kufikia 1.1 tril kwamaan mwaka wa kwanza na wapili alitumia nguvu na unganganyi...unagundua wakati wa JK na magu ni upishani wa hela ndogo tu...cha msingi mkurugenzi atengeneze mfumo waondoe ule mfumo kandamizi Kodi zitozwe kawaida bila kuonea na kwa haki watu watalipa tu Kama walivokuwa wanalipa kipindi cha JK na sasahivi itaongezeka Kama jk 2013 alikusanya 900bil means leo baada ya miaka sita wafanyabiashara na idadi ya watu imeongezeka watakusanya zaidi hata wasipofika kwa haraka kwene hio 2 tril
 
Hujui ulisemalo, ksbb hufanyi biashara. Kwa sisi tuliopo kwenye hiyo sekta kipindi hiki imepitia kigumu sana. Elewa T.R.A hakuishia kwa wa Asia tu. Biashara za wazawa wengi tena wadogo zimefungwa. Ona kariakoo ilivyo sasa na miaka 10 nyuma. Hivi sasa unapata chumba cha biashara maeneo tu mazuri bila kutumia dalalali. Unajua maana yake?. Vyumba vingi viko tupu pale,watu wamefunga biashara. Wapo waliofirisiwa. Ndio unayataka hayo?.
Kibaya zaidi ile kariakoo ilitakiwa iwe kitivo cha biashara kwa nchi za DRC,Rwanda,Burundi,Malawi,Zambia,Mozambique. Lakini kinachofanyika sasa?. Nchi zote hizo wanafuata bidhaa zao Kampala Uganda,nchi ambayo haina bandari.
Unajua tatizo liko wapi hapo?. Bidhaa nzuri kariakoo hamna,eidha watu waliokuwa wanafuata hiyo bidhaa wamefunga biashara au wamefirisiwa. Pili bidhaa za kariakoo wenye bandari ni ghari kuliko Kampala wenye bidhaa zinazopitia bandarini kwetu.
Siku hizi ni kawaida kwa kariakoo kukosa baadhi ya bidhaa kabisa,tofauti kabisa na kipindi cha nyuma.
Walikuwa wanaingia kwenye account za watu. Hata kama una biashara yako umeamua kuhifadhi pesa bank labda kwa kidogo kidogo mpaka kufikia milioni 20,siku wakikuibukia unajua nini walikuwa wanafanya? Mosi ilikuwa lazima uingie kwenye makubariano nao,ukijifanya unajua taratibu ndio hapo unafunguliwa kesi za uhujumu uchumi. Na account inafungiwa kwanza.
Nenda pale tunduma mpaka wa Zambia na Tz. Wafanyabiashara wamehamia upande wa zambia. Unajua ipoje? Mamlaka za Zambia baada ya kunusa wafanyabiashara kunyanyasika na mamlaka za mapato Tz wakawakaribisha kufanyia biashara upande wa Zambia. Tumekimbiza wengi pale,tumekosa mapato mengi sana.
Mwisho ujue wapo walipata strock ksbb ya hawa jamaa,wapo walio maisha kabisa. Ndio unayataka hayo?
Mkuu upo vizuri na wewe hakika ni mfanyabiashara mtu ambae si mfanyabiashara haya yote hawez yajua
 
Shida nyie wafanya biashara mna ujanja mwingi sana,huwa hampendi kulipa kodi,mnapenda mpate faida tu,ndo maana hata zile mashine za EFD zilipokuja mlilalamika sana kwa kisingizio eti zinauzwa bei ya juu,bado hamkuweza kutoa list ya EFD zaid ya kutuandikia kwenye makaratasi, asilimia kubwa ya wafanya biashara wa Tanzania janja janja ni nyingi mno na ujuaji ni mwingi mno,mnapenda mpate faida tu pasipo kutoa kodi,mkibanwa kidogo tu kelele kibao,acheni ujanja lipeni kodi,mbona sisi wafanyakazi serikalini tunalipa kodi kubwa tu tena zaid ya mfanya biashara mkubwa!
Wafanyabiashara si kana kwamba hawapendi kulipa Kodi ila mfumo wa tra kuchukua Kodi kubwa kuliko uhalisia ndio sasababu inazalisha ukwepaji Kama huo....mbona miaka ya nyuma tulipa Kodi vizur tu kwasabab wakati ule mtu upikuwa unalipa Kodi halali na unaridhika awamu ya tano ikabadilisha upepo mtu unakamuliwa mpaka mtaji,kunyang'anya hela za watu kwene akaunti kisa tu wapate hela za SGR kiuhalisia magufuli kauwa private sector na angeendelea miaka kumi hali ingekuwa mbali Sana
 
Kuna siku nilikuwa kwa muhindi mmoja k/koo. Dukani pale nilinunua feni, pasi ya umeme na vitu vingine vichache jumla ilikuwa kama laki 2.2
Baada ya kuniwekea kwenye mfuko naona muhindi anajizungusha tu, Mimi nimetulia namuangalia mwisho wake, naona akashtuka akanipa risiti ya EFD yenye thamani ya elfu 20 na tarehe ya nyuma. Nikamwambia hii sio yangu naomba risiti yangu. Akaanza Boss hivi vitu tumekupunguzia bei sana blah blah kibao ila nikakomaa nae
Sijaelewa hoja yako!!kwani hakuna sehemu mimi nimesema kuwa wahindi hawakwepi kodi, na hilo hata aje nani hawezi kusema kuwa ataweza kulimaliza.
 
Kulipa Kodi ni lazima sio ombi..!
Tukianza kuchukulia kama kulipa kodi sio lazima tutayumba kama Taifa.

Naomba kukuomba uweke mapungufu waliyonayo Wafanyabiashara kwenye kulipa kodi.
Hakuna mfanyabiashara anaekataa kulipa kodi. Na kodi ya Tz inalipwa mara nyingi. Mfano mzigo unapoingia toka ulikotengenezwa labda dubai au china,unapoingia tu Tz pale bandarini unalipiwa kodi kubwa tu. Unapotoka dukani la jumla labda kariakoo unalipiwa kodi. Aliejumua nae hapo huko mkoani nako utalipiwa kodi unapotoka. Mwisho wa siku hiyo bidhaa itakuwa na gharama kubwa. Na ndicho kinachopelekea,nilichoeleza pale mwanzo unakuta,bidhaa hiyo hiyo ukienda Kampala uganda (ambao hawana bandari mizigo yao wanapotishia kwenye bandari yetu)unanunua bei ndogo kuliko dar,wenye bandari. Ndio hapo niliposema mfumo haujawekwe sawa.
Mfano mwingine mdogo ni wewe una rafikiako Mmalawi,mmeagiza magari mawili aina ya corola toleo aina moja,yote mawili yataingilia bandari ya dar ksbb Malawi hawana bandari. Kule mmeagiza mfano kwa milioni 3,3 @ . Hilo la kwako kodi utalipia hapa mfano milioni 6 Tsh. Yule mwenzio wa malawi ataenda kulipia kule isiyozidi milioni 3,wakati wewe una bandari yako mwenyewe. Hapo namaanisha kodi yetu ni kubwa.
Mapungufu ya wafanyabiashara zaidi ni elimu tu jinsi ya ukokotoaji wa ulipaji kodi. Hii elimu hata hawa wengi tu maafisa wa kukusanya kodi hawana hiyo elimu,yeye ameambiwa akusanye tu kodi,hajui akusanye ipi,na ndio maana wanakusanya hata kwenye mtaji.
Hiyo elimu sio ya kukusanya tu wafanyabiashara na kuwaambia lipeni kodi kwa maendeleo ya Taifa. No. Hii elimu nadhani ianzie shule ya msingi kumjengea uwezo hata yule ataekaefungua biashara huko kijijini akimaliza darasa la saba,awe anaweza na anajua namna gani alipe kodi
 
Shida nyie wafanya biashara mna ujanja mwingi sana,huwa hampendi kulipa kodi,mnapenda mpate faida tu,ndo maana hata zile mashine za EFD zilipokuja mlilalamika sana kwa kisingizio eti zinauzwa bei ya juu,bado hamkuweza kutoa list ya EFD zaid ya kutuandikia kwenye makaratasi, asilimia kubwa ya wafanya biashara wa Tanzania janja janja ni nyingi mno na ujuaji ni mwingi mno,mnapenda mpate faida tu pasipo kutoa kodi,mkibanwa kidogo tu kelele kibao,acheni ujanja lipeni kodi,mbona sisi wafanyakazi serikalini tunalipa kodi kubwa tu tena zaid ya mfanya biashara mkubwa!

Pumbavu kweli we, mimi sasa naacha kufanya biashara natafuta kazi nyingine ambayo sitauona mlango wa TRA kulipa kodi. Kulipa kodi ni ujinga tu, kila kitu unachonunua unalipa kodi, bado unachonunua ukienda kuuza ulipe tena kodi, huu ni uzwazwa, lipeni ninyi wafanyakazi
 
Swala la kubadili jina la kampuni ni ngumu kulizua hata wakati wa JPM hiyo njia iliendelea kutumika maana kisheria mfanyabiashara anakwambia amefirisika unamlazimishaje kwamba hajafirisika utampa mtaji ili asifunge Hilo jina la biashara......wakati wa JK alikusanga 900bil magufuli alitikia 1.3tril ambayo ikaanza kushuka baada ya miaka miwili kufikia 1.1 tril kwamaan mwaka wa kwanza na wapili alitumia nguvu na unganganyi...unagundua wakati wa JK na magu ni upishani wa hela ndogo tu...cha msingi mkurugenzi atengeneze mfumo waondoe ule mfumo kandamizi Kodi zitozwe kawaida bila kuonea na kwa haki watu watalipa tu Kama walivokuwa wanalipa kipindi cha JK na sasahivi itaongezeka Kama jk 2013 alikusanya 900bil means leo baada ya miaka sita wafanyabiashara na idadi ya watu imeongezeka watakusanya zaidi hata wasipofika kwa haraka kwene hio 2 tril
Hiyo trilioni 2 ilishafikiwa na TRA kipindi hiki cha JPM
 
We unataka watu wapokonywe hela kwenye akaunt zao...
 
Back
Top Bottom