Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) afanya ziara Visiwa vya Comoro

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) afanya ziara Visiwa vya Comoro

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,278
Reaction score
797
MKURUGENZI MKUU ZBC ZIARANI COMORO

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Zanzibar, Ramadhani Bukini yuko nchini Comoro ambapo amekutana na Mkurugenzi Mkuu mwenzake wa Shirika la Utangazaji Comoro ORTC na kutoa mhadhara wa “Maboresho Yanayofanyika ZBC” uliokuwa kivutio kikubwa.

Bwana Bukini aliwaeleza kuwa maboresho hapo tangu yameanza kumekuwa na ufanisi mkubwa ikiwemo kuongeza matumizi ya teknolojia na mitandao ya kijamii na mafunzo kwa watumishi.

Aidha, aliwaeleza pia maboresho hayo yamesaidia kuongeza mapato ya makampuni ya biashara na kuaminiwa na taasisi za ndani na nje ya Tanzania.

Ziara hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa Mkataba wa Ushirikiano baina ya ORTC na ZBC na imeratibiwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Comoro.

Bwana Bukini anatarajiwa kuonana na Waziri wa Habari na Wadau wengine katika ziara hiyo.
IMG-20241112-WA0025.jpg
IMG-20241112-WA0027.jpg

IMG-20241112-WA0024.jpg
IMG-20241112-WA0026.jpg

IMG-20241112-WA0024.jpg

IMG-20241112-WA0023.jpg

IMG-20241112-WA0022.jpg

IMG-20241112-WA0020.jpg

IMG-20241112-WA0018.jpg
 
Back
Top Bottom