Mkurugenzi mkuu wa TRC, Masanja Kadogosa amegoma kuja JF atufafanulie uhalali wa makatazo wanayofanyiwa wasafiri wa SGR

Usipande na vyakula kwenye ndege au SGR wewe ni wa basi na malori na treni za kawaida huko ndio saizi yako achana na SGR sio hadhi yako
.huko kwingine waweza beba hadi kande kula njiani

Kaa mbali na SGR sio hadhi yako
Sgr Ni hadhi ya nani mkuu?
Taja sifa tafadhar
 
Kwahiyo mabasi yanachakazwa na watu kuingia na maji?😆😆
Usipodhibiti masuala kama hayo ndo unasababisha vyombo vya mradi kuchakaa mapema. Kuna mtu atabeba Pombe atalewa na kujitapikia na mambo mengine mengi.

Jifunzeni kuishi kistaarabu tu. Ule ni mradi wa hela nyingi na kielelezo hivyo lazima ulindwe na kutunzwa kwa gharama yeyote ile!
 
Hili ndo jibu kwamba ni miradi ya watu(vigogo) ndani Sgr sio kivingine.
 
Haki za Binadamu zinakiukwaje?

Kwani umelazimishwa kupanda ile treni? Si upande mabasi au panda lile ngalqngala linaloenda kigoma ufike Dodoma baada ya siku 1. Hujakatazwa
 
Hiyo ni Kodi Yako/yangu Kuna haki ya kuhoji. Pia huwezi pangia mtu asafiri na usafiri Gani sgr hii sio ya mtu binafisi ni ya watanzania wote lazima tuelekezwe ni vipi hairuhusiwi na kwanini.
Kuna usafiri lofa hatakiwi kupanda

Ndege maji na vyakula vimo ndani

Ndege na SGR ni ni Hotel pia huwezi ingia na maji yako na vyakula kwenye Hotel yeyote

SGR ni treni na Hotel vyote kwa pamoja sio kama mabasi yenu ya kwenda kigoma mwandiga au treni za kawaida
 
Haki za Binadamu zinakiukwaje?

Kwani umelazimishwa kupanda ile treni? Si upande mabasi au panda lile ngalqngala linaloenda kigoma ufike Dodoma baada ya siku 1. Hujakatazwa
Kukiuka haki siyo lazima ulazimishwe kupanda. Hata kulazimishwa kutoipanda bila sababu nako ni kukiuka haki.
 
Umechanganya kitu ambacho hatukiongelei hapa mkuu"POMBE"
Tunazungumzia maji ambayo Kila mtu hutumia sio mtoto Wala mzee ni binadamu wote.

Na kuingia na maji kwenye sgr sio ushamba Wala kutokuwa na ustaarabu kama Yana athali yoyote Ile basi haikuwa paswa hata kuuzwa mle.

Pombe hata kwenye basi sijawahi ona mtu kaingia na pombe ma ana inafahamika wazi kabisa si Kila mtu anakunywa pombe!

Pia kwenye tren sio shida kuwepo na behewa Moja ama mawili yenye bar sema hii inatumia muda mfupi kufika hivyo sidhani kama unaweza enjoy.

Sioni sababu kuu ya kuzuia kuingia na maji Ile ni miradi ya watu tu
 
Angalia nauli tu kulinganisha na treni ya kawaida
SGR ni ya high class na middle class sio ya malofa wabeba maji na kande za kula njiani
Nauli ya ndege ya kutoka mwanza to Dar (Go& Return )ya sgr ipi kubwa labda?

Kwa sababu unajibu tu Ili kujifurahisha Wacha Nami nikuulze tu Ili nijifurahishe.

Kwahiyo na wahaya wanazuiliwa kuipanda? Maana Wana maji Automatic 😂😂
 
Kingine mtu asiye na kitambulisho haluhusiwi kupata tiketi
 
Angalia nauli tu kulinganisha na treni ya kawaida
SGR ni ya high class na middle class sio ya malofa wabeba maji na kande za kula njiani
Ushamba na ulimbukeni, hiyo sgr yenye viti vigumu 2×3 kama daladala huku mkitazamana kama chai maharage na nauli sh.13,000/= wewe unaiita high class! Ni ushamba na ulimbukeni.
 
Ushamba na ulimbukeni, hiyo sgr yenye viti vigumu 2×3 kama daladala huku mkitazamana kama chai maharage wewe unaiita high class! Ni ushamba na ulimbukeni.
Kumbe ni chai maharage tena? Tanzania tuna laana kubwa sana na ccm na mwenge wao ndio laana yenyewe!
 
Ungejua hayo mabehewa ni mitumba usingesema hivyo, viti havina mikanda ya usalama na sehemu ya kuegemea kichwa vitambaa havipo pia viti havina tofauti na vya kwenye mabasi yaani 3×2 huku sehemu ya mabegi iko wazi tofauti na mabasi ambayo mabegi yanafunikwa.
 
nadhan wanakataza kwa ajili ya usafi na hulka yetu watazania tukiachiwa itakua vurugu.tuitunze reli jamen.ya. sasa hiv kwend dodom.wala.huwaz chap tu
 
Usafir we treni umekua usafiri kama usafri wa tren wakutoka ghangzhou mpja shanghai
 
nadhan wanakataza kwa ajili ya usafi na hulka yetu watazania tukiachiwa itakua vurugu.tuitunze reli jamen.ya. sasa hiv kwend dodom.wala.huwaz chap tu
Kwahiyo maji na mfuko wa kubebea nguo utachafua treni!
 

Dalili za ubabaishaji. Madudu yamejaa, hawajibiki, hovyo hovyo tu
 
Kukataa kwake kunaonesha hatuthamini abiria tusio na majina zaidi ya kupokea nauli zetu pendwa, TRC ndio wenye majibu nao hawako tayari kukutana nasi, yote ni kheri.
Sina hakika kama umepanda hii treni!!! Naunga Mkono makatazo. Kwa sababu ukiruhusu hayo mambo unayosema gharama za kukarabati zitaongezeka na hii italazimisha nauli ya treni kupanda.

Binafsi siungi mkono kupanda kwa gharama za treni kisa tu kuruhusu vitu ambayo vinavumilika kutiingia navyo ndani ya treni!
 
Chupa ya maji itaharibu treni! Treni haitengenezwi kwa unga wa ngano kuwa maji yakimwagika yatalainisha mabehewa.
 
Sio kweli, pale TRC wana utaratibu mzuri kabisa kuhusu silaha. Ukifika utaikabidhi pale kwa ofisi ya Polisi unaandikisha ukifika unakokwenda unakabidhiwa silaha yako labda kama unazungumzia kuingia nayo ndani ya treni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…