BigWanyamela hawa mabosi wa Magu DC kama wanakubabaisha na pesa zako dawa ni kuwashtaki tu kwa mabosi wao TAMISEMI ilimradi una ushahidi.
Kumbe Diwani Mashaka alikula milioni 2 alizotoa Mhe. Stragomena Tax kwa ujenzi wa choo ambacho mpaka leo hakijaisha na limebaki pagale kama linavyoonekana pichani?
Hivi huyu mama wa watu anajisikiaje anapoona hali hiyo na Magu ni kwao?
BigWanyamela, shitaki hao watu TAMISEMI kwa Naibu Katibu Mkuu Msonde ambaye ni mchapakazi sana. Nakumbuka alipokuwa NECTA alileta mapinduzi mengi chanya kwenye taasisi hiyo ikazidi kuheshimika.
Namwona hata sasa kwenye vyombo vya habari anavyopambana na wabadhirifu wa mali ya umma na wazembe.
Nikiwa mdau na mkereketwa wa Elimu, namwomba Naibu Katibu Mkuu Msonde aimulike sana idara ya Elimu msingi Magu maana imeoza; siyo kwa sababu ya DEO Hapana; DEO anapambana sana, lakini kuna maofisa wala rushwa pale (tunamshukuru Nyagabona amehamishwa Magu kwenda Misungwi) Lakini Afisa Taaluma aliyepo hapo (JOHARI MWASHA) ni mnyanyasaji sana wa waalimu, anawadharau, anawabeza na kuwanyanyasa sana, kiasi kwamba Mwalimu akiwa na suala la kwenda ofisi ya Elimu wilayani hatamani kabisa kukutana na JOHARI MWASHA; maana ni mtihani. (Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI fuatilia suala hili Kwa waalimu wa Wilaya ya Magu utathibitisha maneno yangu)
Nina hakika kabisa JOHARI MWASHA anamkwaza sana Mkuu wake wa Idara, hata kama huyo binti hasemi; maana unapovuruga waalimu na kuwavunja moyo ambao ndio watenda kazi shambani unategemea mavuno gani? Mwisho wa siku lawama zote zinatupwa Kwa DEO Msingi, ambaye anajitahidi kuwa shock absorber kati ya waalimu na Johari; kwa nini iwe hivyo?
Kama ninyi TAMISEMI mnampenda sana JOHARI MWASHA, labda ana ma-godfather huko wizarani, basi mpeni u-DEO Wilaya nyingine aendelee kuwafurahisha ninyi, au mpeni u-DEO hapohapo Magu mmuhamishe Glory ambaye naamini anateseka sana hapo Magu sababu ya huyo maushungi!! Mkuu Msonde fuatilia hilo; naamini network yako iko super na wewe ni intelligent sana.