Titho Dyakiye Philemon
Member
- Nov 15, 2019
- 49
- 128
Ndugu zangu wana JF, ukizaliwa wilayani Ngara, Mkoani Kagera ni rahisi sana kutegua kitendawili cha Kwanini Nguruwe hauzwi kwenye minada ya mifugo licha ya kuwa ni mnyama anayefugwa na mwenye jina rasmi kwenye kundi la wanyama.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara (DED) kwa sasa Ndugu Solomon O. Kimilike amegeuka kuwa Msalaba Mzito kwa mfumo mzima wa utawala katika halmashauri ya Ngara na hivyo kuwafanya wana Ngara kuendelea;-
1. Kuwa na uchumi usio na Mshikamano,
2. amewapoka madiwani nguvu ya uwakilishi madhubuti kupitia kwa mwenyekiti wa Halmashauri,
3. amejigeuza kuwa chuo cha kukasmisha ukuu wa idara kwa watumishi walioko chini yake ambao wanapohamishwa hushushwa vyeo na kuendelea kuifanya Halmashauri ya Wilaya ya Ngara na Waheshimiwa Madiwani kuonekana wenye fikra ndogo kwa vile wanabariki ukuu kwa watu wasio na sifa kwenye wilaya nyingine. Hii inaitia aibu Halmashauri yetu na Ngara kwa ujumla
4. ametengeneza hofu kwa watumishi katika idara zote zilizoko chini yake, na hivyo kuifanya Halmashauri isitawalike na iendelee kuonekana kama himaya yake.
Serikali yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni sikivu mno, lakini ninaamini ikija wilaya Ngara itagundua ni namna gani Mkurugenzi huyu alivyojifanya Papa kitendo kinachowafanya baadhi ya Watumishi wa Halmashauri ya Ngara kumuogopa kwa kuwa amekuwa akiwafukuzisha kazi watumishi wengi sana kwa nyakati tofauti tofauti kwa figisu na pengine bila kufuata taratibu stahiki za kisheria. Serikali ikiandaa kikosi kazi maalumu ikazama Ngara kwa ueledi wake kiutendaji ninaamini itabaini mengi sana.
Hivi sasa Mkurugenzi huyu yupo katika kesi nzito dhidi ya Katibu wa Afya wilayani humu ambaye amempelekea taarifa kuhusu mhudumu mmoja wa zahanati anayepokea Mshahara Mkubwa isivyo kawaida ikilinganishwa na Ngazi ya huduma aliyopo, elimu aliyonayo, na vigezo vingine kama vilivyowekwa wazi kwa ajira na mishahara ya kada husika. Badala ya Mkurugenzi huyo kuungana na mtoa taarifa ili kuweza kubaini tatizo na hatimaye kulidhibiti kwa maslahi ya umma yeye ameamua kumgeukia na kuanza kumlaumu hali ambayo inatia mashaka na kutuuacha kwenye sintofahamu. Hadi sasa binafsi nimejipa muda kuendelea kufuatilia mwisho wa hili na ueledi watakaoutumia waheshimiwa madiwani katika Baraza lao kuweza kuling'amua hili.
Mkurugenzi huyu Ndugu Solomon O. Kimilike akishirikiana na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Ngara Mheshimiwa Wilbard Bambala walifanikisha Mpango wa kumsimika (kumbariki) Bi. Sabra Mwankenda mtumishi wa Halmashauri ya Ngara na kuwa Afisa Utumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara, alipohamishwa Ngara Afisa huyo alivumiliwa cheo hicho na huko aliko ni mtumishi wa kawaida. Nadhani jamii na serikali inaweza ikaona ni namna gani Ndugu Kimilike (DED) anavyo tubebesha msalaba wananchi wa Ngara na kufanya tudharaulike kiutendaji.
Serikali inapaswa kutambua kuwa siyo kila mtumishi anaweza akapata ujasiri wa kupaza sauti dhidi ya Mkuu wake lakini baadhi ya wananchi na wazalendo tunapogundua kuwa kuna shida ndiyo maana tunaamua kuweka wazi kero ili serikali yenye mkono mrefu ichukue hatua stahiki na kwa wakati.
Ni aibu sana kwa watumishi kuona Mkurugenzi anasafiri halafu wakaanza kushangilia kutokuwepo kwake kazini yeye kama Mkuu wao.
Niombe serikali yetu sikivu, pamoja na wadau wote wa maendeleo hapa nchini, mpatapo ujumbe huu mjue wazi kuwa;-
1. Halmashauri ya Ngara inayumba kiutawala
2. Halmashauri ya Ngara inatakiwa kufanyiwa Ukaguzi maalumu (Special Audit) kuthibiti upotevu wa fedha za wananchi unaoonekana kupitia miradi viporo huku mitaani
3. Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya linalomaliza muda wake sasa limeshindwa kuiongoza Halmashauri na Badala yake Halmashauri kupitia kwa Mkurugenzi wake Ndugu Solomon O. Kimilike ndiyo inayoliongoza Baraza la Madiwani
4. Serikali inapaswa kuingia Ngara mapema sana na hatimaye iweze kubaini Mnyororo wa baadhi ya Madiwani wa Halmashauri unaoshirikiana na Mkurugenzi huyu kuihujumu Halmashauri na Hatimaye kupitia vikao vya uteuzi ndani ya vyama vya siasa serikali iweze kuangalia fikra mpya ambazo haziwezi kufungamana na uovu kutokana na upembuzi yaknifu utakaokuwa umefanywa na serikali pamoja na vyama vya siasa.
Mwisho: YAPO MAMBO MENGI SANA YA KUONGEA, ila ninaiomba sana serikali yetu sikivu ya Tanzania iweze kuingia au kutuma kikosi maalumu Ngara kuweza kufuatilia na kudhibiti muenendo wa Mkurugenzi huyu na Hatimaye Ngara yetu ibaki katika mikono salama. Ninaamini serikali ikiamua kuwa serious kwa Ngara, itajua mambo mengi sana.
Mungu ibariki Ngara!
Mungu ibariki Tanzania!