Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums, Maxence Melo anashikiliwa na Polisi, anyimwa dhamana

Najua hata apple walikataa na serikali ya marekan ikaamua kutumia wadukuzi wake kifunga simu hapa kwetu tunamshauli maxence melo kutotoa taarifa yoyote hadi kesi yao ya kikatiba iliyo funguliwa isikilizwe na iishe
 
hivi huwa mnasoma heading na kucoment bila kusoma content au!!? mmeambiwa sababu ni kuwanyima polisi taarifa za memba wa jf pindi zinapotakiwa
wewe mwanzoni hii taarifa haikutaja sababu ya kukamatwa kwake
 

Pole sana Bw. Maxence Melo.

Najua huna hatia, najua hujatenda uhalifu kustahili dhalili unazopitia wala huna nia yoyote mbaya dhidi ya Mtu au Nchi yako zaidi ya kuipenda nchi yako na taaluma yako kwa vitendo. Max umekuwa jasiri na kusimamia sheria, taratibu na haki za binadamu kwa wananchi wa Taifa lako, usivunjike moyo wala kukata tamaa.

Melo unaweza kubambikwa mashtaka ya ajabu tena mazito na hivyo kuteseka na hata kudhurika. Usiogope. Jipe moyo mkuu, usiogope. Nyakati kama hizi lazima zipite kabla ya kufikia nchi ya ahadi ambayo ni ndoto na maombi yako, yangu na ya kila mwenye nia njema na Taifa letu.

"Haki huinua Taifa bali dhambi ni aibu ya watu wowote"
 
Umekazania uchochezi tu, unaweza kutueleza hizo taarifa unazozitaja zilichochea nini na wapi?
Kuna uzi humu ulisema wazi na ushahidi kuwa Makamu wa rais amejiuzulu.

Kuna uzi humu ulipost barua ya ikulu ikionyesha nembo ya ikulu na sahihi ya msemaji wa ikulu ikielezea kutenguliwa kwa mrisho gambo. Huo sio uchochezi ? Au uchochezi kwako ni mpaka watu washike bunduki
 
hivi huwa mnasoma heading na kucoment bila kusoma content au!!? mmeambiwa sababu ni kuwanyima polisi taarifa za memba wa jf pindi zinapotakiwa
Hii habari ilietwa mara ya kwanza ikiwa haina maelezo ya kutosha ila baade ndio ikaletwa taarifa hii mpya unayoiona sasa hivi hapo juu.
 

Mkuu KAULI ya kusema "fanya yako na familia yako naomba uifute" ni Kauli ya kishenzi na ninaomba ipuuzwe

fikiri tena leo hii wazee walioipigania TANGANYIKA na sasa tanzania enzi ya ukoloni wangetumia Kauli yako ungekua wapi au sote tungekua wapi
 
Teh teh teh..... Eti Magu hahusiki!! Umesahau alisema anatamani Malaika (mashetani kwa mujibu wangu mimi kwakua Malaika hawafanyikazi za kijinga) washuke waje wazime hii mitandao ya kijamii!? Mbona na wewe unaanza kuleta Taarifa za kizushi na kijinga humu.
 
POLE SANA ADMIN WETU MAXENCE MELO. KUWA NA SUBIRA; BAHARI HAIKOSI MAWIMBI NA DHORUBA BAADAE HUTULIA.
 
Tumesoma Terms & Conditions za JF? Privacy Policy je? Kama Polisi walifuata taratibu kwa kupata kibali cha mahakama kuomba taarifa binafsi kutoka kwa mmiliki wa JF, basi alitakiwa atoe, otherwise ni ubabe wa polisi na mmiliki wa JF yuko sahihi kukataa kutoa taarifa hizo
 
muwe mnaandika mambo ya maana. msidhani kuficha ID zenu ndo ujanja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…