Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums, Maxence Melo anashikiliwa na Polisi, anyimwa dhamana

Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums, Maxence Melo anashikiliwa na Polisi, anyimwa dhamana

View attachment 445705
Mkurugenzi mtendaji wa Jamii Media, Maxence Melo, ameitwa na baadaye kuwekwa ndani, Central Police.

Polisi wanaeleza muda huu kwamba leo atalala ndani hadi kesho atakapofikishwa mahakamani.

Kosa ni kuwanyima Polisi taarifa binafsi za wateja wa mtandao wa JamiiForums zilipohitajika. Maxence ameendelea kushikilia msimamo kuwa ni uvunjwaji wa sheria na haki za wananchi kufanya hivyo.

Maxence Melo anakamatwa huku kukiwa na Kesi ya Kikatiba dhidi ya taarifa ambazo Jeshi la Polisi wanazitaka, kesi namba 9 ya mwaka 2016 dhidi ya Jamii Media dhidi ya polisi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kesi ambayo mahakama kuu itatolea hukumu, tarehe 20 Februari.
hivi hawa poliCCM ni lini wataacha kukandamiza haki za raia? Kesi hii ikipata wakili mzuri kama Tundu Lissu ataimaliza ndani ya dakika 10 tu.
 
Kwani umeambiwa wanatafuta wanachama wa vyama?
Inaelekea ni ruhusa kutukana upande wa pili-waite wapumbavu, malofa etc utakuwa safe lakini maneno hayo hayo elekeza upande ule......ni mil7 au huenda ikawa kifungo.
 
IMG-20161213-WA0006.jpg
 
Hayo yakwako
Mada hapa ni Sheria ya mitandao ilipitishwa kabla ya Magufuli kuwa Rais

Kosa lake ni lipi?

Kwani mkuu kwenye sheria ya mtandao Kuna kifungu kinasema kinaomba malaika washuke wafunge mitandao ya kijamii?
 
Kama ni hivyo

Basi akibananishwa tu ujue tumeumia humu

Wengine tutawaokotea mabwepande au tindikali zinawahusu
 
Hivi atakubali kweli tumbadilishe mwingine baada ya miaka yake mitano? Naona kama sasa amezidi, hataki kukosolewa, kusemwa vibaya, mbona katika jamii zetu sijawahi kuona mtu anasemwa kwa mazuri tu, hata ufanye mazuri mwingine anaweza kuona ni mabaya kwa mtazamo wake, yani leo wote tuwe na mtazamo sawa inawezekana kweli? Mbona mke kila mtu anachagua anayempenda iweje kwa kiongozi kulazimishana kumpenda wote?!!!! anyway duniani kuna kuzaliwa na kufa, yote ni maisha, hakuna atakayeishi milele, Hitler alikua mbabe kweli lakini mwisho wa siku alikufa.
Umeongea point. Kuna watu wana hoja kibao SA za kumkataa Mandela, ukiwaskiliza utachoka.
 
Hivi mkuu hataki kabisa kukosolewa?hivi hakumbuki hata Mao wa China kafa na alikuwa km Mungu mtu?
 
Hilo ni chaguo lake kama anataka kugeuka Mwanamapinduzi kwa ajili ya watu ambao wanasema watakuwa naye kiroho ni yeye tu ndo anapaswa kuamua, lkn maisha yamenifundisha mengi khs binadamu kwamba mwisho wa siku hakuna anayejali na utakuwa mwenyewe, lema ni mfano mzuri ukiondoa familia yake hakuna anayekosa usingizi kwa ajili yake hata Mbowe au Lowasa hawajakanyaga Arusha hata Tundu lisu ambaye ni Mwanasheria hajakanyaga Arusha kwa ajili ya Lema!
We kwa mawazo yako unafikiri lowassa, Mbowe, Sumaye hawajui kinachoendelea wa, kkwa taarifa yako hata Lema mwenyewe anajua jinsi hao jamaa kwa nje wanavyofight kwa ajili yake. Hayuko peke yake kama unavyodhani shida yako unataka kuwa kama Tomaso aliyetetaka uthibitisho kwa kuona alama za misumali kwa macho yake.
Kinachoendelea ni kikubwa kuliko unavyofikiri
 
Kama kuna kesi ya msingi na haijatolwa maamuzi basi hapo kesho Max ataachiwa tuu..mpaka kesi iliyopo ifanyiwe kazi wala hakuna la maana hapo.
 
Hapo penye nyekundu. Yaani serikali kweli ndiyo yenye nchi na sisi niwapangaji? Nafikiri hapa wigo umepanuliwa kupita kiasi. Nilifikiri watanzania ndiyo wenye nchi na serikali imepewa ridhaa ya kuwaongoza tu. Sitasema mengi kwani walengwa hapa ni sisi ........... Pole ndugu MM-ukifuata ushauri huu basi JF itakuwa Serikali Forum na kuelekea kuzimu.


Hiyo ni kinadharia kwamba ninyi ndio wenye nchi lkn kiuhalisia hakuna kitu kama hicho Dunia hii!
 
Mimi nipo Mikindani
Mahakamani sita hudhulia kabisa
Ni nani aliyekuomba kuhudhuria mahakamani? Mnafki mkubwa wewe.

Mods tafadhali pitieni uzi huu kwa makini mtawatambuwa maadui wa JF ni bora muwadelete permanent wao na IP zao.

By the way Max hii si mara ya kwanza kuwekwa ndani kwa sababu ya JF labda wageni hapa JF ndio hawajui na msidhani Max hajui risk anazobeba kuendesha mtandao huu, hivyo nawasihi msifadhaike.

Kuna wanaume wamejiapiza kabisa humu kwamba Polisi na jela ni kwa ajili ya watu fulani tu lakini niwaonya ole wao hata Zombe alikuwa Polisi mkubwa lakini amemalizia utumishi wake kama mjelajela.

Only fear for death.
 
Atumie ubabe wake kufungia vyombo vyote vya mawasiliano abakize magazeti ya ccm,tbc na star tv tujue moja.
 
Kuna uzi humu ulisema wazi na ushahidi kuwa Makamu wa rais amejiuzulu.

Kuna uzi humu ulipost barua ya ikulu ikionyesha nembo ya ikulu na sahihi ya msemaji wa ikulu ikielezea kutenguliwa kwa mrisho gambo. Huo sio uchochezi ? Au uchochezi kwako ni mpaka watu washike bunduki


Mkuu kwenye kampeni maghufuli alisema hakuna mwanafunzi aliye na sifa atakosa mkopo na hilo alilitamka dodoma, lakini mbona kafanya kinyume? Je huoni kwa hata yeye Mwenyewe anakichanganya?
 
Back
Top Bottom