Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums, Maxence Melo anashikiliwa na Polisi, anyimwa dhamana

salama salmini lakini yupo lupango....hivi lupango ni salama au unamaanisha nn
 
Watumiaji wa mtandao wa JamiiForums wako huru kuweka mijadala, kuanzisha mijadala, kuchangia chochote pasipo kuvunja sheria za nchi au kuhatarisha usalama wa taifa.

Hiyo Sentensi nimelipenda. Mahakama ndiyo ipewe Nafasi katika kuamua maana ndiyo walinzi wa mambo ya Sheria kupitia Katiba na Sheria zenyewe.
 
Mungu akulinde Max. Naamini kwa leo utapata dhamana na maisha lazima ya endelea. Hata Martin Luther King toka wakati huo aliamini pamoja na ukandamizaji na utumwa wa enzi zile USA bado ndoto ya ilikuwa iko siku Black atakuwa President of USA.
 
duuuh hii nchi hii kweli nilishasema tunaelekea kubaya mno
 
THE GUARDIAN
"THE founder and managing director of popular social online platform JamiiForums, Maxence Melo, was yesterday arrested by the police in Dar es Salaam for allegedly refusing to divulge user data to the authorities".

JamiiForum is an internet forum where anybody can contribute his/her thoughts, the problem with this country is that we are living in 21st century but we still think as though we are practising Azimio la Arusha.

I believe there is another forum in Africa which I can describe it as a global one in terms peoples' contributions, you can read what they are talking about Muhammad Buhari.

Search
 
Wakuu moderators tunaomba mfungue uzi wa kutupa updates za mahakamani leo
 
jamani niliimisi sana Jf,imenisaidia vitu vingi sanaaaa ambavyo nlikua busy navyo hadi nikapotea humu jukwaani.
habari hii imenishitua sanaaaa........
ni mwendo wa kuzidisha maombi tu,haya yote yatakwisha.....
Hizi dhana za maombi Tanzania huwa sinanifurahisha sometimes. Naona Mungu tunamtwisha hata mambo yasiyomuhusu. Tumepewa uhuru wa kutawala na kujitawala tangu uumbaji, let fight for our right tuache kumchosha Mungu
 
Mpaka hapo alipofikia Max ni shujaa, angekua mwingine Jf ingepoteza dira siku nyingi. Natumai Sheria itachukua mkondo wake haki itapatikana. Dua zetu kwako Max.
 
Ndugu wanajamvi;

Naandika haya nikiwa nina maswali tata kadha wa kadha kichwani mwangu lakini majibu yake naona hakuna wa kunipa kwa sasa!

Suala la Ben sanane kupotea katika mazingira ya kutatanisha siyo jambo nzuri kwa afya ya siasa zetu ilo tulijue wote siyo upinzani siyo chama tawala. Ni vizuri kuhoji amepoteaje kuliko kuchukulia uepesi kama wengine ninavowaona humu ndani au kushangilia moyoni.

Ni lazima tujue wote kuwa Ben sanane ni mtu na ana haki zake kama mimi kama wewe hivyo basi tuachilie mbali harakati zake za kisiasa labda alikuwa anakosoa upande fulani ni haki yake kikatiba kama mimi kama wewe tunavoona makosa ya mbowe na kukosoa ! Hii ndio aina ya siasa ambayo tumelelewa na tumekulia.

Ukweli utuweke huru kuliko chuki kutamalaki kwenye mambo yenye maslahi ya taifa, ni vyema vyombo vinavohusika vifanye uchunguzi wa haraka na umakini utawale ili kuuondoa minong'onong'o na taharuki katika jamii yetu.

Mimi ni miongoni mwa wale wanaoamini kuwa waziri wa mambo ya ndani juzi alilitoea majibu mepesi kwenye maswali magumu na ata yeye akiitafakari nahisi atajua hilo ni mda huu wa kujisahisha na kuja na majibu yanayoridhisha kuuhusu ile miili saba iliyozikwa kinyemela! Nashukuru angalau PM ameagiza uchunguzi lakini katika hili angeongezea neno huru iwe "IWE UCHUNGUZI HURU" ili kuondoa taharuki hii kwa wananchi .

DUKUDUKU LANGU KWA CHADEMA KUHUSU BEN SANANE:

Naomba Ukweli utuweke huru kabsaa! Ben kathibitika amepotea ndani za siku ishirini tena kwa kutooenaka mtandaoni maswali ya kujiuliza ni mengi hapa na mengine yawezekana tusipate majibu yake lakini turudi kwenye hoja ya msingi!

Chama kikubwa kama chadema inakuja kutoa tamko juu ya hili jambo baada ya wadau wa kawaida tyuu kuhoji na kupaza sauti zao usiku na mchana nahisi ata kikatiba ya chama kila mtu ni sawa bila kujali ushawishi au cheo chake. Je angepotea Tundu Lisu ata kwa wiki mmoja chama kisingetoa tamko? tukumbuke Ben saanane naye ni kada kindakindaki wa chadema ni Afisa kwenye ngazi ya uongozi ndani ya chama.

Ni maoni yangu kuwa Freeman Mbowe kama Mwenyekiti wa taifa na anayejipambanua kuwa ni mzalendo na mpigania haki za watanzania alivyosikia hii habari ya ben sanane kupotea angesitisha ziara yake kwa heshima yake ndani ya chama na ndani ya nchi kuja kufuatilia na kuongoza uchunguzi kuhusu hili jambo na ata zile maiti waliozikwa kimyakimya.

Hapa ndipo tukubali, tukatae siasa zetu bado zipo nyuma sanaa hii issue ingetokea ata kwa majirani wetu kenya ingekuwa hot kwelikweli lakini mkuu wa upinzani yeye yupo ulaya hana mda na haya mambo kwangu mimi napatwa na ukakasi mkubwa! Wewe ndiye mpambaji mkuu halafu upo nyuma kabsaa la jambo gumu kama hili sisi wapambanaji wa kawaida tukuchukuliaje?

Katibu mkuu Dk. Mashinji anaongea kwenye gazeti la mtanzania halafu la kwake limeishia kiivo! Ni watanzania wangapi wana acces kusoma gazeti la mtanzani? Haya ndiyo majibu mepesi kwenye mambo magumu kama haya! Hapa ndipo tukubali tukatae DK. Slaa bado ataonekana kuwa mpambanaji bora kwenye vita katika mda wote.

Ni wale wanaoamini Ben yupo hai ata kama yupo mikononi mwa majasusi au la ni vyema apatikane akiwa hai kwa haraka hili mambo kadha wa kadha yaendeleee katika nchi yetu, Na siamini katika nchi yetu tumeshafika kwenye siasa za kutekana mimi naamini nchi yetu bado ni huru na wananchi wanatakiwa kuwa huru.

KUHUSU CEO WA JAMIIFORUMS, MAX:

Kama kichwa changu cha habari tuache na kuweka itikadi zetu vya vyama pembeni tuweke maslahi ya taifa kwanza kwenye hili jambo!

Ila swali kwenu je Jamii forum ikizimwa nani atafaidika???? ndipo tuanze hapo kutafakari kwa kina kuliko kubishana na ukweli!

Ni wako kijana mtiifu, Mwanaharakati na mzalendo wa kweli katika taifa hili.
Mungu ibariki Tanzania.
 
Huku zanzibar kuna mazombi zaid ya miaka 20 hajakamatwa hata mmoja. Tanganyika inahitajika uhuru mpya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…