Mkurugenzi na Afisa Elimu Sekondari Halmashauri ya wilaya Uyui-Tabora, Makinikeni hii sio sawa

Mkurugenzi na Afisa Elimu Sekondari Halmashauri ya wilaya Uyui-Tabora, Makinikeni hii sio sawa

NAMBA MOJA AJAYE NCHINI

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2019
Posts
9,863
Reaction score
20,806
Idara ya utumishi na Tsc

Kuna watumishi mliwahamisha vituo vya kazi tangu mwezi July mwaka jana Hadi leo hamjawalipa stahiki zao za uhamisho na BADO wapo vituo mama wakisubiri fedha zao Hadi leo na hawafanyi kazi KWA takribani mwaka mzima.

Watumishi hao wanalipwa mishahara bila kufanya kazi KWA mwaka mzima wakisubiri fedha zao za uhamisho Hadi leo!

Hivi mnafikiri hayo malipo hewa sio hasara KWA serikali na wananchi kuhujumiwa kodi zao!!?au mnatumia nini kufikiri hilo!?

Hamuoni huo ni ubadhirifu na matumizi mabaya ya fedha za serikali!!?
Amueni Moja Kati ya haya;

1.Kusitisha uhamisho na kuwapa barua waendelee kufanya kazi katika vituo mama kama hamna fedha za kuwalipa!!?

Au

2. Walipeni fedha zao mapema Ili waende kulitumikia TAIFA lao kwenye vituo vyao vipya vya kazi!

Mamlaka ya Tsc Uyui mnalijua Hilo!!?Mbona mmekaa kimya kwa mwaka mzima!!?

Nimepewa ujumbe nimeufikisha fanyieni kazi kabla mamlaka ya utumishi kitaifa haijawachukulia hatua za kinidhamu!
 
Kuhamishana kijinga jinga hivi kunaleta udwanzi Sana...unapewa barua halafu kumbe hawana pesa ,,,siku dawa ndio hiyo kukomaa mpk watoe cash...lasivyo mtuache tujenge Taifa nyie lipaneni posho huko tu.


Tusisumbuane kabisa.
 
Hapo ni kulpa fedha wakafanye kazi vituo vipya.

Ukiwaandikia barua ya kufanyia kazi kituo mama maana yake ni uhamisho mwingine.

Kumbuka walisharipoti kituo kipya na wanasubiri mwajiri awalipe sitahiki zao.

Kisheria hawana kosa. Waendelee kula bata batani
 
Back
Top Bottom