Mkurugenzi NHC: Uamuzi wa Serikali kuhamia Dodoma umesababisha hasara kwa Shirika la Nyumba

Mkurugenzi NHC: Uamuzi wa Serikali kuhamia Dodoma umesababisha hasara kwa Shirika la Nyumba

Hii nchi ni ya ajabu sana, shirika ni la serikali na linategea kufanya biashara na serikali,
ndiyo mana hata mabenki mengi yana mashart ya ajabu ajabu kwenye mikopo!!
kuna uhitaji mwingi sana wa makazi ila kwa kuwa mmeona wanaopaswa kulengwa ni wafanyakazi wa serkali tu!

Alafu hao mnaoimba nyimbo wakajiajiri hata hiyo mitaji hamjui wanaitoa wapi!
 
Hoja yake ni kwamba miradi iliyokuwa inaendelea ilisimama,kusimama kwa miradi hiyo kulisababisha hasara kwa shirika.Kuamia kwa serikali Dodoma kulifanya mipango ielekezwe Dodoma.
NHC ni shirika la kitaifa sio la Dar es salaam tu, linatakiwa lipange mipango ya kupeleka uwekezaji nchi nzima na sio kurundika Dar tu hivyo ni hoja dhaifu.

Miradi ya NHC sio sawa na mradi wa kuuza nyanya, ni miradi na uwekezaji wa Muda mrefu alichotakiwa kufanya ni kuiendeleza pale ilipoishia na sio kuja la lawama.
 
Mpango wa kuhamia Dodoma ulikuwepo toka enzi ya Nyerere miaka ya Mwanzo ya 70.
Inakuwaje pamekucha ndio mtu anavuta shuka.Kwani hili hawakulijua cha kufanya piga chini badilisha kiongozi angetakiwa wakati anaingia awe analijua hilo.Ni sawa na kujenga tank kubwa la maji likiwa halina matoleo ya maji sasa baadae yale maji iamuliwe kuhamishwa pengine kwa vijibomba vingine katika mipango ya serikali.
Unatakiwa wewe uliyekabidhiwa kuangalia hilo tank usilalamike maji yanaisha buni mbinu za kuweka vibomba vingine vya kujazia maji yanayoondoka.
Wapo watu wanatafuta sehemu za kuishi hasa raia wa kigeni hawezi ishi uswahilini kwa usalama wao.Yako mashirika ya kimataifa ya nje wote hawawezi kaa oysterbay au Mikocheni wapangisheni kwa dola hizo nyumba.
Sio lazima tupange sisi watanzania hizo nyumba.
Simple mathematics
 
Hoja yake ni kwamba miradi iliyokuwa inaendelea ilisimama,kusimama kwa miradi hiyo kulisababisha hasara kwa shirika.Kuamia kwa serikali Dodoma kulifanya mipango ielekezwe Dodoma.
Aanzie alipopakuta. Serikali ilipoamua kuhamia dodoma ilijua hayo. So ye aanzie alipopakuta, hayo mambo ya hasara zilizopita aiachie serikali.

Kuhusu nyumba kupata wapangaji watuwekee bei rafiki. Nyumba za watu binafsi zina bei chee kuliko hizo za NHC. Eti vyumba viwili na sebule 500K. Kisha unasema huna wapangaji. Mbona zile za upanga za 150K zimejaa hadi huwezi pata nafasi.
 
Back
Top Bottom