Mkurugenzi TANESCO apewe Tuzo, umeme Unapungua haujawahi katika! CHAWA ni kielelezo cha vijana walio tayari kufanya lolote kwa Dhumuni!

Mkurugenzi TANESCO apewe Tuzo, umeme Unapungua haujawahi katika! CHAWA ni kielelezo cha vijana walio tayari kufanya lolote kwa Dhumuni!

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2016
Posts
15,835
Reaction score
23,776
Umeingia ofisini saa 2 asubuhi, ukakuta hakuna umeme umekaa siku nzima ukisuniri umeme.

Unaamua kuondoka saa 11 jioni, ukijifariji kwamba utaukuta umeme nyumbani angalau ufanye kazi za wateja wako.

Unafika nyumbani saa 1 kasoro unakuta hakuna umeme wanakuambia wamekata saa 12 jioni. Unajaribu kuusubiri umeme Hadi saa 6 usiku, hakuna umeme.

Unaamua kwenda kulala, kitandani una mtoto wa miezi 10 unakuta anahangaika joto usiku mzima analia. Unashindwa hata kulala. Huku ukiwa na stress za kazi za watu.

Mwisho wa siku muendelee kusema Vijana wa Tanzania ni wavivu, hawajitumi, uzembe mwingi. Asubuhi nitaamka, unakuta sms za TRA wanakusubiri Kodi zao za ajabu za kubambikiwa, Jiji na leseni zao wanaakusubiri tozo nyingi nyingi... Daaahhh!

Anyway mnaopush agenda[CHAWA], na hashtags ni MAJASIRI sana, Mungu awasaidie kuona MAISHA HALISI kuliko kuona Pesa. Sijui mnaishije wenzetu, sijui mko Tanzania ya wapi wenzetu Tunajitekenya wenyewe tunacheka wenyewe.

Tujifunze kupendana Kwanza na tujifunze kujaliana. Pia tujifunze kuambizana ukweli. UBINAFSI unarudisha Maendeleo. Na ubinafsi wa watu kadhaa umekwamisha Taifa kufika kwenye malengo.

SIASA TOO MUCH IS HURTFUL AND HURTFUL

crdt : Lusaj0
 
Mkiambiwa jitokezeni Barabarani hamtoki sasa mmebakia kupost mipsho humu, sikiliza hakuna sehemu yoyote malalamilo yalileta mageuzi.Sasa endeleeni na Post za kulalamika ila mkiambiwa tokeni Barabarani hamtaki mnataka Mbowe atoke na Familia yake awatetee
 
Hayo ndio matunda ya ccm, kuwa mpole tu mkuu maadam umechagua mwenyewe kuwa mnyonge.
 
Vijana wanalipwa Tsh. 20,000 ku push hashtag za kishenzi twitter, huwa najiuliza kama mtu analipwa Tsh. 20,000 kuficha ukweli wa jambo ambalo hata yeye na ukoo wake linamuathiri je akipewa Tsh. 10 milion si anaweza kuuza utu wake kwa kukubali kuliwa kiboga??!!.
 
Mkuu heshima kwako

Umeiweka vizuri sana

Ingawa title yako ilinishtua
 
Aiseeee umeongea Kwa uchungu mkubwa Sana.
Nchi hiii kama tunaishi jehanamu Fulani hivii
 
Mjinga mwingine ni Joti

Screenshot_20240125-210712_X.jpg
 
Dada nimekukubali chawa hapaswi kusogelea mlango wa kanisa au msikiti ni hela dhuruma kama wakabaji wengine akina lucas mwasa-mbwa..
 
Tunataka umeme na sio POROJO..chukueni hatua za muda mfupi wakati tukisubiri hicho kinu hiyo March..TWAFAAA!
 
Mkiambiwa jitokezeni Barabarani hamtoki sasa mmebakia kupost mipsho humu, sikiliza hakuna sehemu yoyote malalamilo yalileta mageuzi.Sasa endeleeni na Post za kulalamika ila mkiambiwa tokeni Barabarani hamtaki mnataka Mbowe atoke na Familia yake awatetee
Kwa hiyo,barabarani ndo shida zinaishia! Kazi kweli kweli
 
Hii nchi kufanya kazi inayohitaji umeme ni kama vile Laana!! mi tenesco walinitoa barabarani kipindi natotoresha vifaranga!! ila Kwasasa niliamua kuanziasha kampuni ya uvuvi Sina shida na umeme wa mchongo.
Jiulize sasa wangapi wametolew kwenye reli.
 
Tunataka umeme na sio POROJO..chukueni hatua za muda mfupi wakati tukisubiri hicho kinu hiyo March..TWAFAAA!
Mvua za mafuriko nchi nzima toka december,2023 lakini bado visingiio, sasa kama Mungu wa Israel asingeleta mvua sijui ingekuwaje?
 
Back
Top Bottom