Mkurugenzi TANESCO apewe Tuzo, umeme Unapungua haujawahi katika! CHAWA ni kielelezo cha vijana walio tayari kufanya lolote kwa Dhumuni!

Mkurugenzi TANESCO apewe Tuzo, umeme Unapungua haujawahi katika! CHAWA ni kielelezo cha vijana walio tayari kufanya lolote kwa Dhumuni!

Anyway mnaopush agenda[CHAWA], na hashtags ni MAJASIRI sana, Mungu awasaidie kuona MAISHA HALISI kuliko kuona Pesa. Sijui mnaishije wenzetu, sijui mko Tanzania ya wapi wenzetu Tunajitekenya wenyewe tunacheka wenyewe.
Hawa Watu ni Wapumbavu kuliko upumbavu wenyewe aiseeee
 
Umeingia ofisini saa 2 asubuhi, ukakuta hakuna umeme umekaa siku nzima ukisuniri umeme.
Unaamua kuondoka saa 11 jioni, ukijifariji kwamba utaukuta umeme nyumbani angalau ufanye kazi za wateja wako.

Unafika nyumbani saa 1 kasoro unakuta hakuna umeme wanakuambia wamekata saa 12 jioni. Unajaribu kuusubiri umeme Hadi saa 6 usiku, hakuna umeme.

Unaamua kwenda kulala, kitandani una mtoto wa miezi 10 unakuta anahangaika joto usiku mzima analia. Unashindwa hata kulala. Huku ukiwa na stress za kazi za watu.

Mwisho wa siku muendelee kusema Vijana wa Tanzania ni wavivu, hawajitumi, uzembe mwingi... Asubuhi nitaamka, unakuta sms za TRA wanakusubiri Kodi zao za ajabu za kubambikiwa, Jiji na leseni zao wanaakusubiri tozo nyingi nyingi... Daaahhh!!

Anyway mnaopush agenda[CHAWA], na hashtags ni MAJASIRI sana, Mungu awasaidie kuona MAISHA HALISI kuliko kuona Pesa. Sijui mnaishije wenzetu, sijui mko Tanzania ya wapi wenzetu Tunajitekenya wenyewe tunacheka wenyewe.

Tujifunze kupendana Kwanza na tujifunze kujaliana. Pia tujifunze kuambizana ukweli. UBINAFSI unarudisha Maendeleo. Na ubinafsi wa watu kadhaa umekwamisha Taifa kufika kwenye malengo.

SIASA TOO MUCH IS HURTFUL AND HURTFUL

crdt : Lusaj0
Kwenu TANESCO
Hujasema vile vinyama na vikuku kuharibika..
Hujawaongelea wenye stationery wanavyolala njaa..
Hujaongelea watengeneza keki, ashkirimu na barafu wanavyonyanyasika..
Hujaongelea wale wa dry cleaning...
Bado hujawasemea wa printing nk
Ni shidaaaa nyie waheshimiwa TANESCO
Kama mkikata umeme kateni mpaka ikulu, Kwa mama Samia na viongozi wake wote wakuu ili waelewe hii aidha, huu uchungu, huu umaskini mnaotubambika utaisha lini?!
 
Back
Top Bottom