Mkurugenzi TPA: Bunge lina haki kuukubali au kuukataa mkataba wa DP World

Mkurugenzi TPA: Bunge lina haki kuukubali au kuukataa mkataba wa DP World

Mbona kama kuna ujumbe anajaribu kuutoa?,anachomanisha ni kwamba Bunge lisiridhie huo ujinga.
 
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Plasduce Mbossa amesema Bunge la Tanzania lina haki ya kuridhia au kutoridhia mkataba wa ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kwa ajili ya uendelezaji na uboreshaji wa utendaji kazi wa bandari(IGA).

Mkataba huo ulisainiwa Oktoba 25, mwaka jana kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai ili kuendeleza na kuboresha uendeshaji wa miundombinu ya kimkakati ya bandari za bahari na maziwa makuu, maeneo maalumu ya kiuchumi, maegesho ya utunzaji mizigo na maeneo ya kanda za kibiashara.

Hata hivyo hofu imeibuka kuhusu masilahi ya Taifa kwenye mkataba huo ambapo wanasiasa, wanaharakati na wasomi wanahoji vifungu 31 vya mkataba huo pamoja na nafasi ya Bunge katika kufikia uamuzi wa mwisho.

Kwa mujibu wa Ibara ya 63 (3) (e) ya Katiba ya 1977 kama ilivyorekebishwa, Bunge limepewa mamlaka ya kujadili na kuridhia mikataba yote inayohusu Jamhuri ya Muungano na ambayo kwa masharti yake inahitaji kuridhiwa.

“Kushauri ni moja kati ya kazi za Bunge na zipo nyingine nyingi kwa mujibu wa Katiba, katika hili hapa (mkataba wa IGA) Katiba inasema Bunge ndilo linaridhia kwa hiyo Bunge linaangalia ambacho Serikali imesaini na upande mwingine, basi linaridhia au haliridhii,” amesema Mbossa.

Mbossa ametoa kauli hiyo leo Juni 8, 2023 wakati wa mahojiano yaliyofanyika katika Kituo cha televisheni cha Clouds 360, asubuhi ikiwa ni mwendelezo wa kutoa ufafanuzi wa hoja na elimu kuhusu makubaliano ya mkataba huo kwa Taifa.

“Kama Bunge halitaridhia mkataba huu hautakuwepo kwa sababu una sharti lazima uridhiwe. Bila kuridhia utatekeleza kwa nguvu ipi?”amehoji Mbossa na kufafanua kuwa maelekezo yoyote ya kurekebisha vifungu vya mkataba huo kutoka bungeni, yatatafsiriwa ni kutoridhiwa kwa mkataba huo.

Chanzo: Clouds 360, Mwananchi
Yaani hata kama wali sign kwa kutambua kuwa kutakuwa na process ya kibunge, ndiyo wa sign ule upupu?
 
Daah huyo Boss wa TPA nae hajasoma huo mkataba au alilazimishwa kusaini tuu..
 
Sasa kama Bunge halitoridhia yeye kama DG atakuwa na kazi gani tena ya kuendelea na nafasu yake hiyo? Kwa maana yeye ni mmoja wapo wa timu ambayo itakuwa imeshiriki ktk mchakato mzima wote na mpaka unapelekwa bungeni watakuwa wameshajiridhisha kwa kila kitu.

Anyways, ktk hili mimi naona Mh. Rais Mama yetu amethubutu kwa kutaka kuwaleta serious investors hawa wenye cv kubwa za kazi hii ya bandari duniani baada ya sisi wenyewe kuilalamikia bandari yetu kwa miaka mingi kwamba imekuwa haina tija wala ufanisi mzuri na hakuna super profit yotote tunayopata kutokana na bandari yetu kana Taifa.

So Mama she is calculated risk hasibezwe bali apongezwe na wengi kabla yake walitamani kufanya hivi wakashindwa yeye amethubutu.Tuache tuone matokeo yake na halkika tusikosoe kwa hoja za uongo na upotoshaji kwa maslai yetu binafsi ya udini,ukanda,uchama n.k zisizokuwa na utafiti.

Mama kwangu ni shujaa ktk kuifungua nchi kwa kukaribisha hizi Multinational Organization's ambapo kwa uchumi wa sasa haiepukiki kama nchi haina uwezo wa kuendesha yenyewe au usimamizi ni mbovu imefeli na unawatajirisha wachache na kujilimbikizia mali kwa ufisadi pale bandarini ni bora tuwape wawekezaji serious.Asante na nipo tayari kwa kusahihishwa na kuelimishwa ktk hili.
 
Back
Top Bottom