Mkurugenzi TPA: Mkataba wa Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo ungeifilisi Tanzania

Mkurugenzi TPA: Mkataba wa Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo ungeifilisi Tanzania

Wawakilishi wepi hao mkuu? Hawa akina Lusinde ,Lusinde,Mlinga na mapoyoyo mengine ambayo yakishalishwa sumu kwenye vikao vyao vya ndani wakija bungeni utadhani si wa TZ? Rejea ishu ya ESCROW ndo utajua CCM ni nani. Jiulize Ngugai ana maslahi gani kufikia hatua ya kupinga waziwazi kama si 10%?
Tunaishi ktk Dunia ya Ubepari, kumbuka Ubepari ni Unyama hakuna utu kabisa
Katika hali ya kawaida kibiashara hatupaswi kususa. Tulipaswa na sisi tuseme lipi tunalitaka kwenye huo Mkataba na lipi hatulitaki katika Mkataba huo
Ndio maana hili suala la Mikataba lilishaongelewa miaka nenda miaka rudi hii mikataba iwe wazi ijadiliwe Bungeni ili wawakilishi wetu watusaidie kudadavua kipi chenga, kipi Mchele
 
Siamaini kama haya yalikuwa kweli ni masharti ya huu mkataba. Yanaonekana kama vile mtu anajisemea tu ....... Anyway, na yale Masharti aliyotuletea Msiba last week, mbona yako tofauti na haya ya wiki hii ..............!!?

Ni kama vile kwa sasa kila mtu anakuja na yake ya kutunga ilikuwaridhisha Wananchi. Kama haya ni kweli au yale ya Msiba last week kwa nini Waziri asingyasema Bungeni kama alivyoombwa na Spika!!
 
Usiniwekee maneno yako mdomoni mwangu.Eti namkubali huyo fisadi kwa shingo upande? 😳😳😳Vipi wewe!? Usilazimishe kisichokuwepo wala ambacho hakitakuja kutokea eti mimi nimkubali huyo nduli wa Ikulu.
Utabaki kulalamika na muda utakuaibisha DOGO
 
bahati mbaya sana serikali yetu hii kesho utasikia,mtu katumwa china na Oman kwenda kuzungumza nao ni suala la Muda tu.Foreign Direct investment haiwezi filisi nchi labda mniambie grace period imekuwa ndefeu mno
 
Huu mkataba kweli kama tunavyoambiwa na kila mtu ni mbaya sana, hivi hakuna namna ya huu mkataba mbaya kuwekwa wazi hata kama ni sehemu chache tu, ili wote tujiridhishe kuwa ni mbaya. Isije kuwa ni wimbo tu tunakaririshwa, kwanini huu mkataba mbovu usiwekwe wazi? Tuwanyamazishe hawa wapiga kelele?
 
Are you one of them Zwazwas? Just asking
It is just a relative term. It depends on one who terms the other. But nowadays one is clever because he/she can behave uncouthly in public. Logic has failed in Tz. Good luck.
 
It is just a relative term. I depends on one who terms the other. But nowadays one is clever because he/she can behave uncouthly in public. Logic has failed in Tz. Good luck.
Duh. You left me empty. Never understood a word from this Idiom you have just written
 
Bandari ya Bagamoyo ingefilisi, kuuza nchi
Sunday May 19 2019
pic+kokoko.jpg

Kwa ufupi
Pamoja na kusamehewa kodi na ushuru mbalimbali kama zile za lazima kisheria, kulipwa fidia ya hasara ya kibiashara watakayopata kwa mujibu wa mahesabu yao, mwekezaji pia aliweka sharti la kuachiwa ajipangie bei ya kuwatoza watakaosafirisha mizigo kupitia bandari hiyo,.

By Peter Saramba na Jonathan Mussa, Mwananchi mwananchipapers@mwananchi.co.tz

Mwanza. Wakati Watanzania wa kawaida, wabunge na Spika Job Ndugai wakiendelea kujiuliza kwanini Serikali imesitisha majadiliano kuhusu uwekezaji kwenye mradi wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo, imebainika kuwa Serikali ingefilisika iwapo ingekubali masharti ya mwekezaji.

Pamoja na kusamehewa kodi na ushuru mbalimbali kama zile za lazima kisheria, kulipwa fidia ya hasara ya kibiashara watakayopata kwa mujibu wa mahesabu yao, mwekezaji pia aliweka sharti la kuachiwa ajipangie bei ya kuwatoza watakaosafirisha mizigo kupitia bandari hiyo.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Deusdedith Kakoko akizungumza leo Jumapili Mei 19,2019 na Mwananchi katika mahojiano maalumu Jijini Mwanza, amesema licha ya Serikali kukubali kusamehe ushuru wa stempu, ukaguzi wa forodha (customs inspection) ile ya ukaguzi wa meli ambayo ni tozo ya Kimataifa na kufungua kituo (one stop center) cha kuhudumia biashara katika bandari ya Bagamoyo, mwekezaji aliibua masharti mengine mapya 14 yasiyotekelezeka.

Kakoko ametaja masharti mapya yaliyoibuliwa na mwekezaji kuwa ni ya kusamehemewa kodi ya mapato, kodi ya taasisi, kodi ya ongezeko la thamani ya mali, kodi ya mapato kwa watu binafsi, ushuru wa Seriali za mitaa na kodi ya majengo.

“Mwekezaji pia alitoa mashari ya kusamehewa tozo ya ardhi, kodi ya fidia kwa wafanyakazi, kodi ya uendelezaji wa ujuzi, kodi ya forodha na kodi ya ongezeko la thamani, VAT.
“Walitaka wasamehewe kodi, ushuru na tozo zote za vibali vya kuishi na kufanya kazi nchini; hii ingesababisha wageni, hata wasiohitajika wala kuwa na kazi ya kufanya kujazana nchini,” amesema Kakoko.

Amesema mwekezaji aliweka masharti hayo kwa kisingizio kwamba hakuna shehena ya kutosha na kuhoji inakuwaje mwenye fedha awekeze kwenye biashara isiyolipa.

“Hakuna shehena ya kutosha wakati wewe (mwekezaji) unataka kuwekeza kwenye reli na bandari. (Ni lazima) Unakuja kwa sababu biashara ipo” amesema Kakoko
Amesema masharti hayo yangekubaliwa, ni dhahiri Taifa lingeambulia sifuri huku mwekezaji akichukua asilimia 100 ya kila kinachopatikana licha ya ukweli kwamba pande zote zimewekeza.

Mkurugenzi Mkuu huyo ametaja ardhi, rasilimali watu na nguvu kazi pamoja na mazingira bora ya uwekezaji uliopi nchini kuwa ni sehemu ya uwekezaji wa Serikali huku mwekezaji akitakiwa kuleta mtaji.

“Wakilegeza masharti na kukubali tugawane sawa sawa hakuna tatizo; waje na fedha zao. Lakini wahakikishe nasi tunapata. Haiwezekani sisi tupate sifuri lakini wao wapate asilimia 100,” amesema
Wachina ni noma lazima watuingize chaka tutajuta tu tatzo wtz huwa tunajifanya wajanja kumbe mamburura hahaaaaaaaaai inauma saaana
 
Back
Top Bottom