Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kama ulikuwa ujui akuna watu wanaopend lushwa kama wachinaHapo watakuwa wamenyimwa rushwa ndio maana wameyaona haya yote, na wachina hawawezi kutoa rushwa mara mbili.
2020 huyu jamaa akiendelea kuwa Rais nitawashangaa sana watanzania ikulu Hakuna Rais hapo kuna jitu la ajabu linaishi humoHili halina ubishi ni Ukweli mtupu.
Ndiyo faida ya kuingia mikataba kwa Siri.Jk alikubali
Salute Mkuu. Yaani masikini ni madkini tu hadi akilini. Makodi kibao wakati kwenye mtwa kuwekeza hujachangia hta sh Moja?? Tanzania ta makodi hii hatuwezi kufika popote. Wachina wamejifunza hawatarudi kuwekeza kitu chochote wanasubiri tuwape ikandarasi wa barabara tu wakisanye chao wasepe.Nchi ingefilisika kivipi ?
Wewe huoni kuwa hizo kodi na tozo ni nyingi sana?
Kwa mfanyabiashara yeyote duniani hawezi kuwekeza mtaji unaozidi Tril .10 halafu akubali makodi na matozo mengi yasiyozingatia ukubwa wa mtaji wake.
Ni sisi pekee waafrika tunaofanya biashara za wanasiasa na kisiasa bila kujali faida.
Tunatumia matrilion ya kodi kununua Ndege,korosho,stiglers, reli bila kujua faida inaanza kupatikana baada ya kurudisha mtaji wote.
Bila kuwa na uhakika wa kurudisha Mtaji kwa kipindi kifupi basi hiyo itakua sio Biashara ni huduma !
Hakuna mwekezaji anayewekeza mtaji wake kwa ajili ya kutoa huduma tu isiyo na faida kama Red Cross au World vision.
Mtu anakuja na mtaji wake halafu tunatumia siasa kuanza kumwita mwizi ,mnyonyaji ,beberu, shoga , mpigaji ,mkwepa kodi ,halafu tunataka kupata wawekezaji!!
Tutabaki na wawekezaji wa viwanda vya vifungashio,ndala ,yeboyebo , viti na meza za Plastiki na juiisi.
Kinachotuumiza waafrika ni kupinga unyonyaji kwa kutumia mifumo ya kodi ,sheria na mifumo ya utawala ya wakoloni tuliowafukuza.
Afrika baada ya Uhuru hawakuwahi kukaa na kujadili mifumo yao ya utawala ,siasa na uchumi.
Watawala wengi baada ya kile walicjokiita Uhuru Walifurahia kukalia viti vile vya watawala wa kikoloni na sheria zake zote na mabavu yake.
Tukaendeleza elimu yao kwa ajili ya kulinda maslahi ya watawala tu na wananchi wanabaki kama watumwa kwenye nchi zao kama ilivyokua mwanzo.
Wasomi wa Mwanzo walipaswa kufanya tafiti na kuja na mifumo ya kiafrika ya Ardhi ,uwekezaji na mifumo ya kuwawezesha wananchi wao maskini sana wawe na maisha bora sio kama ilivyo sasa serikali ndiyo inataka kuwa na mapesa ya kugawa barabarani wakati wananchi wengi hawana hata ardhi achilia mbali nyumba zaidi ya kupangishiwa vichaka.
Tukiwa na mifumo yetu wenyewe Kuna namna nyingi sana za kupata wawekezaji hata kwa kuwasamehe hizo kodi za moja kwa moja kutoka kwao.
Tunaweza kuwaambia wafungue Account zao zote kwenye Local Benki kwa ajili ya kupitisha malipo yao yote.
Tunaweza kuwaambia vifaa vyote vya ujenzi kama nondo,sementi, mawe ,kokoto , misumari, n.k wanunue hapa nchini kwenye viwanda vyetu.
Tunaweza kuwaambia mafuta ya Petrol na Diesel wanunue nchini ili tupate tozo zilizopo huko.
Tunaweza tukawaambie wakate bima kwenye miradi yao yote kwenye mashirika ya ndani huko tutapata kodi.
Tunaweza tukawaambia wanunue vyakula vya kitanzania.
Tunaweza tukawaambia kuwa ni lazima watumie umeme wetu na sio majenereta ili wanunue Luku na huko kodi inakatwa.
Tunaweza kuwaambia watumie simu za mitandao yetu ya ndani ili wanunue Vocha n.k.
Tunaweza kuwaambia walipie bima za ndani kuagiza Bidhaa toka nje.
Wakiingiza magari bila ushuru bado wanatakiwa wayakatie bima na wawekezaji mafuta na walipie Usajili ambavyo vyote vinaingiza mapato.
Tunaweza kuwaambia watumie Wahitimu wa vyuo vyetu kwenye Mafunzo kwa vitendo.
Tunaweza kuwapa masharti ya kujenga Bandari tu na maeneo mangine yawe ni fursa za watanzania wenyewe.
Vitu kama mahoteli ,nyumba za kupanga wafanyakazi, maduka, n.k.
Tunaweza kupata mapato Makubwa kwa wateja watakaokuja kutoka nchi nyingine kuja kutoka mizigo yao kupitia Vipimo kwenye mizani Tanroad, mafuta wanayoweka wanalipia Area,eura,Tarura, Vat ,motor vehicle n.k.
Nchi inafilisika kwa miradi inayofanywa na serikali bila utafiti kama wanavyokopa kule Zambia Kisiasa ili wawadanganye wananchi kuwa kuna maendeleo kwa kuonyesha miradi mikubwa isiyo na faida. Lakini kama mwekezaji amekuja na mtaji wake na hana madai kwetu zaidi ya mkataba ambao akivuruga tunaweza kumshitaki na kutulipa sioni kwa nini tunawadanganya watanzania kuwa nchi itafilisika wakati hakuna pesa ya kodi yetu itakayotumika zaidi ya sisi kunufaika na kupanda kwa mzunguko wa pesa kama tutawaruhusu wawekezaji waje na miraji yao na wasiungane na wanasiasa.
Kuna nchi nyingine sijajua kwetu wawekezaji walikua wanagoma kutokana na kupewa masharti marefu na tozo nyingi wakati huo huo wanaombwa 10% na wanapewa masharti ya kuajiri wanafamilia wa mawaziri husika na kusomesha watoto wao nje ya nchi ili wapewe fursa za kuwekeza.
Hali hiyo ilikua inasababisha wawekezaji wanakua wakwepa kodi ili kufidia masharti wanayopewa.
Sijajua kwetu Tanzania hali ikoje lakini zipo nchi za magaharibi kwa Afrika ni tatizo sana.
Wanasiasa sio wakuaminiwa sana mana mambo mengi wanayafanya kwa kuweka maslahi yao mbele na kupoteza fursa zenye Tija kwa Wananchi wengi.
Siamini kuwa watu wa Ukanda huo wa Pwani ambao ndio wenye ardhi hiyo iliyoporwa na wakolini na kupewa Malkia na baadae kupewa watawala wa kiafrika kwa sheria ya mkoloni na kuwaacha maskini wangeulizwa kuwa kuna fursa ya kupata mwekezaji wa Bandari kubwa Barani Afrika ,wangeona kuwa mwekezaji anakuja kuwaibia badala ya kuwapa fursa kubwa sana ya kuinua maisha ya watu wa mikoa ya Tanga ,Pwani na hata DSM ,morogoro n.k.
Pia tukumbuke Fursa ya wetu kupata ajira na kujiajiri itakua kubwa sana.
Vijana wakipata ajira wanatumia fedha kuendesha maisha yao.
Wakinunua mahitaji yao wanakatwa kodi.
Kupanga ni kuchagua lakini
Kuna wakati Kuchagua pia kunakua ni kupanga.
Yaani hii comment unasifia sifia kama lishoga!!!!BAK usiwe mnafiki still Rais Magufuli is the best for this country. Nani angeweza kukataa huo mktaba mbovu kama sio Rais Magufuli.
Au sometimes una smoke ile sigara kubwa
Tatizo wewe na lumumba hamnaga akiliMagu amezuia mkataba wa hovyo, BAK kaleta mada inayoelezea kitu kizuri kilichofanywa na awamu hii sasa huoni kuwa anakubali (japo kwa shingo upande) mazuri anayoyafanya Magu?
Cheki ulivyo choko hata kuandika ******** imekushinda kwa mahaba ya kichoko na kusifia ulokua nayo!!!!Pole. Maguliiii utabaki kuwa juuu. Utabaki kuwa juu mawinguni
Hukulelewa katika malezi bora ndio maana unatoa maoni hovyo hovyoYaani hii comment unasifia sifia kama lishoga!!!!
Akili kwako ni kubandika mada ishirini kwa siku kuhusu Iran?Tatizo wewe na lumumba hamnaga akili
Bandari ya Bagamoyo ingefilisi, kuuza nchi
Sunday May 19 2019
![]()
Kwa ufupi
Pamoja na kusamehewa kodi na ushuru mbalimbali kama zile za lazima kisheria, kulipwa fidia ya hasara ya kibiashara watakayopata kwa mujibu wa mahesabu yao, mwekezaji pia aliweka sharti la kuachiwa ajipangie bei ya kuwatoza watakaosafirisha mizigo kupitia bandari hiyo,.
By Peter Saramba na Jonathan Mussa, Mwananchi mwananchipapers@mwananchi.co.tz
Mwanza. Wakati Watanzania wa kawaida, wabunge na Spika Job Ndugai wakiendelea kujiuliza kwanini Serikali imesitisha majadiliano kuhusu uwekezaji kwenye mradi wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo, imebainika kuwa Serikali ingefilisika iwapo ingekubali masharti ya mwekezaji.
Pamoja na kusamehewa kodi na ushuru mbalimbali kama zile za lazima kisheria, kulipwa fidia ya hasara ya kibiashara watakayopata kwa mujibu wa mahesabu yao, mwekezaji pia aliweka sharti la kuachiwa ajipangie bei ya kuwatoza watakaosafirisha mizigo kupitia bandari hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Deusdedith Kakoko akizungumza leo Jumapili Mei 19,2019 na Mwananchi katika mahojiano maalumu Jijini Mwanza, amesema licha ya Serikali kukubali kusamehe ushuru wa stempu, ukaguzi wa forodha (customs inspection) ile ya ukaguzi wa meli ambayo ni tozo ya Kimataifa na kufungua kituo (one stop center) cha kuhudumia biashara katika bandari ya Bagamoyo, mwekezaji aliibua masharti mengine mapya 14 yasiyotekelezeka.
Kakoko ametaja masharti mapya yaliyoibuliwa na mwekezaji kuwa ni ya kusamehemewa kodi ya mapato, kodi ya taasisi, kodi ya ongezeko la thamani ya mali, kodi ya mapato kwa watu binafsi, ushuru wa Seriali za mitaa na kodi ya majengo.
“Mwekezaji pia alitoa mashari ya kusamehewa tozo ya ardhi, kodi ya fidia kwa wafanyakazi, kodi ya uendelezaji wa ujuzi, kodi ya forodha na kodi ya ongezeko la thamani, VAT.
“Walitaka wasamehewe kodi, ushuru na tozo zote za vibali vya kuishi na kufanya kazi nchini; hii ingesababisha wageni, hata wasiohitajika wala kuwa na kazi ya kufanya kujazana nchini,” amesema Kakoko.
Amesema mwekezaji aliweka masharti hayo kwa kisingizio kwamba hakuna shehena ya kutosha na kuhoji inakuwaje mwenye fedha awekeze kwenye biashara isiyolipa.
“Hakuna shehena ya kutosha wakati wewe (mwekezaji) unataka kuwekeza kwenye reli na bandari. (Ni lazima) Unakuja kwa sababu biashara ipo” amesema Kakoko
Amesema masharti hayo yangekubaliwa, ni dhahiri Taifa lingeambulia sifuri huku mwekezaji akichukua asilimia 100 ya kila kinachopatikana licha ya ukweli kwamba pande zote zimewekeza.
Mkurugenzi Mkuu huyo ametaja ardhi, rasilimali watu na nguvu kazi pamoja na mazingira bora ya uwekezaji uliopi nchini kuwa ni sehemu ya uwekezaji wa Serikali huku mwekezaji akitakiwa kuleta mtaji.
“Wakilegeza masharti na kukubali tugawane sawa sawa hakuna tatizo; waje na fedha zao. Lakini wahakikishe nasi tunapata. Haiwezekani sisi tupate sifuri lakini wao wapate asilimia 100,” amesema
Kweli kamanda! Wale wasio wa hovyo wangepiga dili hapo.kama ni hivyo bas ni afadhari walivyopiga chini huo mradi, ILA UKWELI UTABAKI PALEPALE KUA MAGUFULI NI RAIS WA HOVYO KUWAHI KUTOKEA KTK HISTORIA YA NCHI HII, ova.