Mkurugenzi wa Chunya akataa maombi ya Diwani na Wananchi kuhusu kushusha bei ya kuhifadhi maiti

Mkurugenzi wa Chunya akataa maombi ya Diwani na Wananchi kuhusu kushusha bei ya kuhifadhi maiti

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya, Mkoa wa Mbeya, Tamimu Kambona amegoma kupunguza gharama za kuhifadhia maiti 'mochwari' katika Vituo vya Afya vilivyopo wilayani humo kutoka Sh. 40,000 kwa siku mpaka Sh 20,000, baada ya maombi kadha kutoka kwa Wananchi ambao wamekuwa wakidai kiwango hicho ni kikubwa kwao.

Kambona amesema itakuwa ngumu kupunguza kiasi hicho wanachopaswa kulipa cha shilingi elfu arobaini kutokana na gharama kubwa zinazotumika katika uendeshaji mochwari hizo.
Screenshot 2024-05-02 214352.png
Wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri, Diwani wa Kata ya Chokaa, Samweli Komba aliibua hoja ya chumba hicho cha kuhifadhia maiti kujengwa kwa nguvu za Wananchi ili waweze kuondokana na adha ya kusafirisha umbali mrefu miili ya wapenda wao, badala yake imekuwa mzigo kwao kwa kutozwa fedha kubwa ambayo baadhi ya Wananchi wamedai kushindwa kumudu gharama.
 
Back
Top Bottom