Mkurugenzi wa Green Acres Secondary School Aumbuka.

Mwanaukweli

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2007
Posts
4,786
Reaction score
1,715
Mkurugenzi wa Green Acres Bw. Bujugo ameumbuka baada ya kutoa habari zisizo za kweli juu ya matokeo ya shule yake, akishutumu NECTA kwa kile alichokiita uzembe mkubwa.

Baadhi ya tuhuma za Bw. Julian Bujugo zilinukuliwa gazeti la Tanzania Daima
Alitaja mfano wa mwanafunzi, Humphrey Sanga, mwenye namba 01197/148, ambaye hakufanya mitihani hiyo lakini matokeo yanaonesha amefaulu kwa kupata alama nzuri.

"Huyu mwanafunzi tulimsimamisha na hakufanya mitihani, lakini matokeo yake yanaonekana amepata hivi; Civics D, Historia D, Jiografia C, Kiswahili D, English C, Physics D, Chemistry C, Biology C, Basic Mathematics D, ambapo amepata daraja la tatu pointi 24," alisema Bujugo.

Alimtaja mwanafunzi mwingine, Martin Rushaigwa, namba 01197/0173, ambaye alifanya masomo ya ‘Arts'.
Alisema matokeo ya mwanafunzi huyo yanaonesha kuwa ameongezewa alama za masomo ya biashara ya Bookeeping na Commerce, ambayo hakuyafanya kabisa.

Alimtaja mwanafunzi mwingine aliyefanya mtihani huo lakini matokeo yake yanaonesha amewekewa ‘absent' na mwanafunzi mwingine, Mbazi Volta, hakufanya mitihani lakini amepewa alama za ufaulu.

Hata hivyo, habari zilizopatikana leo hii zinaeleza kuwa uongozi wa shule hiyo uliitwa Baraza la Mitihani ili kuthibitisha madai hayo na ukashindwa kuzithibitisha.

Wanasheria wa Baraza la Mitihani wako mbioni kumchukulia hatua Bw. Julian Bujugo kwa upotoshaji huo.

Attachments

  • Baraza.PNG
    29.6 KB · Views: 150
  • Necta.PNG
    121.6 KB · Views: 149
  • baraz.PNG
    49.4 KB · Views: 148
  • Baraza.PNG
    33.6 KB · Views: 3,225
  • Baraza1.PNG
    32.8 KB · Views: 3,205
  • Necta.PNG
    74.1 KB · Views: 3,212
  • Necta1.PNG
    60.4 KB · Views: 3,228
  • necta2.PNG
    11 KB · Views: 3,097
Uongo wa kwanza huu hapa:

"Alimtaja mwanafunzi mwingine, Martin Rushaigwa, namba 01197/0173, ambaye alifanya masomo ya ‘Arts'.

Alisema matokeo ya mwanafunzi huyo yanaonesha kuwa ameongezewa alama za masomo ya biashara ya Bookeeping na Commerce, ambayo hakuyafanya kabisa".

Matokeo yanayoonekana mtandaoni ni:
[TABLE="class: cms_table, width: 617"]
[TR]
[TD]S1197/0173[/TD]
[TD="width: 4%"]M[/TD]
[TD="width: 6%"]34[/TD]
[TD="width: 4%"]FLD[/TD]
[TD="width: 58%"]CIV-F HIST-F GEO-F KISW-D ENGL-F LIT ENG-F BIO-F B/MATH-F

[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Hata wewe unaweza kuthibitisha kwa kuangalia
https://www.jamiiforums.com/matokeo2012/data/s1197.htm Namba 0173.
 
kazoea huyo shule yake inahistoria ya kuiba mitihani sana

Alizoea kuiba mitihani sasa keshadhibitiwa na NECTA, hivyo anaonesha bifu lake. Ukiangalia data za matokeo utabaini kuwa madai yake yote ni feki, kapotosha umma ni vema watu kama hawa wakachukuliwa hatua.
 
huwez jua labda waliyabadilisha baada ya shutuma. Kama waliyaprint/save ya kwanza itawasaidia lakini kama hakuna changes ni waongo. Du mi nilijua ni ya kishua sana kumbe nao kuna walio-differentiate a constant wa kutosha
 
Copies zilizochapishwa zipo.
 
huwez jua labda waliyabadilisha baada ya shutuma. Kama waliyaprint/save ya kwanza itawasaidia lakini kama hakuna changes ni waongo. Du mi nilijua ni ya kishua sana kumbe nao kuna walio-differentiate a constant wa kutosha
Mzee unatoshia watu,si unajua hesabu janga la taifa hiyo ku differentiate const utafanya watu wa google
 
Hivi st mary, happy skilful na st mathew matokeo yake yakoje ? Kwani hawa ni mabingwa wa madesa !
 
Tuwe wakweli kwa hilo la matokeo wala wasimtishe kwani hata mimi ofisini kwangu kuna vijana wanne wamekuja kuangalia matokeo na kukuta wamepewa points kwenye masomo ya Sayansi wakati hawakuyafanya. Hilo ni kweli wala si uongo.
 
Hapo ndio utawajua watanzania. Kwani hayo matokeo ni siri, watu wengi wanayo wanaweza thibitisha kama ni kweli. Huyo jamaa lazima apewe adabu.

Unadhani ni rahisi kuthibitisha, wakati matokeo yametoka kwa namba? Ni rahisi kuzibadili namba ndgu!
 
Tuwe wakweli kwa hilo la matokeo wala wasimtishe kwani hata mimi ofisini kwangu kuna vijana wanne wamekuja kuangalia matokeo na kukuta wamepewa points kwenye masomo ya Sayansi wakati hawakuyafanya. Hilo ni kweli wala si uongo.

Hao watoto majina yao ni kina nani? Namba zao za mtihanni ngapi? na wamesoma shule gani?
Tuna matatizo mengi sana kiasi kwamba haiingii akilini kwanini mtu abuni tatizo la uongo. Mbona matatizo ya ukweli yapo, kwanini tusiongelee hayo???
 
HAJAUMBUKA. Tumeumbuka tuliolipa ada 4 years halafu vijana wetu wanachanganyiwa matokeo. maana yake ni kwamba elimu yooooooooooooote ya Olevel imo ndani ya namba ya mtihani tu. no need to go to school.
 
Mkuu muongo kavurunda anatapatapa,wamebadilisha wataweza kubadili wakati matokeo watu tumeprint,kweli bongo siasa imekua kila kitu siasa
 
Mbona hakuna hayo masomo aliyoongezewa ya Bookeeping wala commerce?
Bujugo 2liosoma pale miaka hyo 2namjua vizur kwa kununua mitihan
 
huwez jua labda waliyabadilisha baada ya shutuma. Kama waliyaprint/save ya kwanza itawasaidia lakini kama hakuna changes ni waongo. Du mi nilijua ni ya kishua sana kumbe nao kuna walio-differentiate a constant wa kutosha
Nimelipenda hilo neno la kudiferentiate a constant..
 
Nimesikia tetesi kutoka Facebook kuwa katika matokeo ya kidato cha IV ya mwaka 2012, mwanafunzi Marehemu Alex katika Shule ya Sekondari Lubala iliyopo wilayani Rungwe, Mkoa wa Mbeya apata DIV 4, wakati alifariki Aprili, 2012!! Tanzania ni zaidi ya uijuavyo!!!
 
mama mdogo 1012?????
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…