Mkurugenzi wa Green Acres Secondary School Aumbuka.

Mkurugenzi wa Green Acres Secondary School Aumbuka.

lile Sakata la Islamic Knowledge lilitukanisha sana Waislaam na Uislaam, leo kibao kimegeuka ! Allah'u Akbar !

attachment.php

attachment.php


attachment.php

attachment.php

attachment.php


 
Nimeangalia matokeo ya shule yake imejaza maziro nadhani alikuwa anatumia uongo kuchagua NECTA maana anajua kuwa biashara imeingia dosari. Hata hivyo, nashangaa vyombo vya habari vinawezaje kuchapa habari nzito namna hiyo bila kusikiliza upande wa pili wa shilingi.

Duuuh vyombo vingine vya habari ni janga la taifa
 
Bujugu nasikia ni diwani wa maccm hili tatizo angelipeleka lijadiliwe kwenye vikao vya chama.
 
Walizoea kuiba mitihani hao sasa imekula kwao.Wanaumbuka kila kona
 

Ya Islamic Knowledge yangekuja hivi hivi, ingekuwa poa ! .............maana mpaka ilipotumika nguvu ya ziada na mashinikizo (Bunge, Wawakilishi na maandamano) ndo ikafanyika review, na kuprove kulikuwa na makosa !
 
Tuwe wakweli kwa hilo la matokeo wala wasimtishe kwani hata mimi ofisini kwangu kuna vijana wanne wamekuja kuangalia matokeo na kukuta wamepewa points kwenye masomo ya Sayansi wakati hawakuyafanya. Hilo ni kweli wala si uongo.


Hapo vipi?? Vijana waliokuja kwako inaonekana hawajui namba zao walizofanyia mitihani kama alivyokuwa mkurugenzi wa Green Acres, Mr. Bujigo. Ona alivyoumbuka hapa
 
Ya Islamic Knowledge yangekuja hivi hivi, ingekuwa poa ! .............maana mpaka ilipotumika nguvu ya ziada na mashinikizo (Bunge, Wawakilishi na maandamano) ndo ikafanyika review, na kuprove kulikuwa na makosa !
Mkuu si kweli hata kidogo kwamba NECTA ilishughulikia suala la Islamic knowledge baada ya Bunge, wawakilishi na maandamano.

Kwanza ujue suala la Green Acres ni suala la shule moja na linalohusu wanafunzi wachache sana. Suala la Islamic Knowledge lilikuwa suala la nchi nzima, kwa wanafunzi wote waliofanya somo hilo, hivyo kutoa taarifa ndani ya siku moja inaeleweka.

Mkuu hatua zilichukuliwa mara baada ya NECTA kupata barua toka kwa Umoja wa Waalimu Wakuu wa Shule za Kiislam, na ndani ya siku mbili matokeo mapya yalitoka. Matokeo yalitangazwa tarehe 1/05/2012, NECTA ilipokea barua ya kuhusu tatizo hilo tarehe 28/05/2012, na tarehe 30/05/2012 marekebisho yakawa yamekamilika. Kikao cha Tarehe 31/05/2012 kikaidhinisha marekebisho hayo, na tarehe 1/06/2012, siku 4 tu baada ya kupokea malalamiko ya Walimu wa Shule zinazofanya somo la Islamic Knowledge, barua rasmi iliandikwa kwa shule zote zinazofanya Islamic Knowledge kuwajulisha, na matokeo yakawa yamerekebishwa rasmi mtandaoni.

Aidha Tarehe 7/06/2012, ikiwa ni siku 10 tu tangu NECTA ipokee barua ya malalamiko hayo, Waziri Kawambwa aliandika barua yake kwa umma.


Soma Tamko la Waziri Kawambwa.

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI

TAMKO LA SERIKALI KUHUSU MALALAMIKO DHIDI YA MATOKEO YA SOMO LA ISLAMIC KNOWLEDGE KATIKA
MTIHANI WA
KIDATO CHA SITA 2012


1.0 UTANGULIZI

Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha sita 2012 yaliyotangazwa rasmi tarehe 01/05/2012. Tarehe 28/5/2012 Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ilipokea barua kutoka Baraza la Wakuu wa Shule za Kiislamu yenye Kumb. Na. BSK/W/012/01 ya tarehe 22/5/2012 iliyoeleza kutoridhika na ufaulu wa watahiniwa waliofanya somo la Islamic Knowledge kwa kuwa waliona matokeo yaliyotangazwa hayakuwa na uhalisia wa uwezo wa wanafunzi. Kutokana na barua hiyo, Serikali ilifanya uchunguzi kwa kuangalia mambo yafuatayo:

. Kulinganisha alama za watahiniwa zilizojazwa katika vituo vya usahihishaji mitihani na zile zilizohifadhiwa katika Kompyuta, yaani database ya Baraza la Mitihani ili kubaini kama kuna tofauti yoyote; na

. Kulinganisha alama za somo la Islamic Knowledge zilizochakatwa na Mfumo wa Kompyuta na sampuli ya alama zilizokokotolewa kwa kutumia kikokotozi (calculator).


2.0 MATOKEO YA UCHUNGUZI
. Baada ya kupitia hatua za uhakiki kuhusu usahihishaji na utoaji wa matokeo, ilibainika kuwa alama za mwisho katika somo la Islamic Knowledge zilizokokotolewa na Mfumo wa Kompyuta ZILITOFAUTIANA na alama zilizopatikana kwa kutumia kikokotozi. Uchunguzi zaidi uliofanyika kwa lengo la kubaini chanzo cha tatizo katika uchakataji wa matokeo hayo kwenye Mfumo wa Kompyuta ulionesha kuwa uchakataji uliotumika awali kutoa matokeo ya mwaka 2012 ulitumia jumla ya "Paper" tatu kama ilivyokuwa mwaka 2011.

. Kutokana na mabadiliko ya Fomati ya Mtihani wa somo la Islamic Knowledge yaliyoanza kutumika rasmi katika Mtihani wa Kidato cha Sita 2012, mtihani huo kwa sasa una "paper" mbili na siyo "paper" tatu. Hivyo, tofauti ya alama iliyobainika imetokana na Mfumo wa Kompyuta kuendelea kutumia "paper" tatu katika kupata wastani wa alama za mwisho badala ya kutumia "paper" mbili.


3.0 HATUA ZILIZOCHUKULIWA NA SERIKALI
. Baada ya kugundua dosari hiyo kwa somo la Islamic Knowledge, uhakiki ulifanyika kwa masomo yao yote ya Mtihani wa Kidato cha Sita 2012 yaliyokuwa na "paper" zaidi ya moja ili kujiridhisha endapo uzito sahihi ulitumika katika kupata wastani wa alama za watahiniwa. Matokeo ya uhakiki huo yalionesha kuwa alama sanifu zilizokokotolewa na mfumo wa kompyuta ni sawa na alama zilizokokotolewa na Kikokotozi. Hivyo hakuna dosari yoyote iliyobainika katika masomo mengine.

. Matokeo ya somo la Islamic Knowledge yaliyotangazwa awali yamerekebishwa kwa kutumia Paper mbili kama inavyotakiwa ili kuendana na mabadiliko ya Fomati ya somo hilo. Marekebisho hayo yaliridhiwa na Baraza la Mitihani katika Kikao chake Maalum kilichofanyika tarehe 31/05/2012.

Aidha, Kikao kati ya wajumbe wa Baraza la Mitihani na wawakilishi wa Baraza la Wakuu wa Shule za Kiislamu kilifanyika tarehe 31/05/2012 ambapo walielezwa kuwa Wakuu wote wa Shule wenye watahiniwa waliofanya somo la Islamic Knowledge wataandikiwa barua rasmi kufahamishwa kuhusu marekebisho yaliyofanyika na barua hizo ziliandikwa tarehe 01/06/2012. Pia walifahamishwa kuwa matokeo yao yote ya masomo mengine hayana dosari yoyote na yanabaki kama yalivyotangazwa na Baraza la Mitihani la Tanzania. Matokeo hayo yamewekwa kwenye tovuti ya Baraza la Mitihani na pia yatatangazwa kwenye magazeti.

. Pamoja na marekebisho hayo, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi itaunda Kamati ya wataalamu kuiwezesha serikali kujiridhisha zaidi na hatua zilizochukuliwa na Baraza la Mitihani ili kuepuka dosari ya aina hiyo isijitokeza tena kwa siku zijazo.

. Viongozi wa Baraza la Wakuu wa Shule za Kiislamu waliridhika na hatua zilizochukuliwa na Wizara na wameandika barua ya kuishukuru Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kuhusu namna walivyoshughulikia malalamiko yao.


4.0 HATMA YA WANAFUNZI WALIOREKEBISHIWA MATOKEO KATIKA MAOMBI YA KUJIUNGA NA VYUO VIKUU

Wizara inapenda kuwahakikishia watahiniwa waliorekebishiwa matokeo yao kwamba, kwa kuwa zoezi la usajili bado linaendelea hadi tarehe 30/06/2012, waliorekebishiwa matokeo yao watapata fursa ya kuwasilisha maombi ya kujiunga na vyuo vikuu endapo wana sifa stahiki. Aidha, kwa upande wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, maombi ya mikopo hufanyiwa kazi rasmi baada ya Tume ya Vyuo Vikuu kukamilisha mchakato wa udahili wa wanafunzi wa elimu ya juu. Hivyo, hapatakuwa na athari yoyote kwa watahiniwa husika kupata mikopo endapo watakidhi vigezo vinavyotakiwa.

5.0 HITIMISHO
. Napenda kuhitimisha kwa kuwasihi wazazi, walezi, wanafunzi na jamii kwa ujumla kuwa na imani na Baraza la Mitihani la Tanzania kama chombo chetu chenye dhamana kisheria ya kuendesha mitihani nchini.
Hapakuwa na hujuma yoyote iliyofanyika kwa watahiniwa ambao matokeo yao yamerekebishwa. Kosa lililojitokeza ni la kibinadamu, halikufanywa kwa makusudi wala kwa lengo lolote la kuhujumu kundi fulani la watahiniwa. Marekebisho yameshafanyika na matokeo stahiki yameshatolewa. Aidha, uhakiki uliofanyika kwa masomo yao mengine unaonesha kuwa hakuna dosari yoyote iliyobainika katika masomo yote.
. Kutokana na dhana ya baadhi ya watu kuwa kunakuwa na upendeleo kwa baadhi ya watahiniwa wa makundi fulani katika usahihishaji napenda kuwakumbusha kuwa wakati wa mitihani, watahiniwa huandika namba zao za mitihani na siyo majina. Katika taratibu za usajili wa Baraza la Mitihani hakuna kipengele chochote kinachomtaka mtahiniwa kuonesha kabila yake, dini au itikadi ya kisiasa. Vilevile, utaratibu unaotumika kuwapata wasahihishaji huzingatia uwezo wao kitaaluma na uzoefu kazini.

Aidha, katika fomu ya mapendekezo ya uteuzi wa wasahihishaji hakuna mahali popote ambapo Mkuu wa Shule hutakiwa kuonesha kabila yake, dini au itikadi ya kisiasa ya mwalimu anayependekezwa kusahihisha mitihani.


. Utaratibu unaotumika kusahihisha mitihani hautoi mwanya wa upendeleo. Katika kudhibiti uwezekano wa kupendelea mtu yeyote kila msahihishaji husahihisha swali moja tu na kisha humpatia msahihishaji mwingine asahihishe swali linalofuata. Aidha, kila msahihishaji hutakiwa kuweka vifupisho vya majina yake (initials) ili ufuatiliaji uweze kufanyika kadri itakavyohitajika. Pia uhakiki wa usahihishaji hufanyika kwa lengo la kujiridhisha na usahihi wa kazi na kuhakikisha kuwa kila mtahiniwa amepata alama anazostahili. Dosari zinazobainika zimekuwa zikirekebishwa katika mchakato wa usahihishaji na wasahihishaji wanaobainika kuhusika na dosari hizo wamekuwa wakichukuliwa hatua stahiki mara zinapobainika.

. Pamoja na hayo niliyoyaeleza nina taarifa kuwa yanapangwa maandamano ambayo yanalenga suala hili hili la kutoridhika na matokeo ya awali ya somo la Islamic knowledge. Kwa kuwa suala hili limeshapatiwa ufumbuzi, nawasihi wananchi wajiepushe kushiriki maandamano hayo kwa sababu suala la msingi lililo wafanya watake kuandamana limeshatolewa maelezo. Hivyo, maandamano hayo hayatakuwa na tija.


IMETOLEWA NA DKT SHUKURU JUMANNE KAWAMBWA


WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI


TAREHE 07/06/2012
 
Mkurugenzi wa Green Acres Bw. Bujugo ameumbuka baada ya kutoa habari zisizo za kweli juu ya matokeo ya shule yake, akishutumu NECTA kwa kile alichokiita uzembe mkubwa.Baadhi ya tuhuma za Bw. Julian Bujugo zilinukuliwa gazeti la Tanzania Daima
Alitaja mfano wa mwanafunzi, Humphrey Sanga, mwenye namba 01197/148, ambaye hakufanya mitihani hiyo lakini matokeo yanaonesha amefaulu kwa kupata alama nzuri.¡°Huyu mwanafunzi tulimsimamisha na hakufanya mitihani, lakini matokeo yake yanaonekana amepata hivi; Civics D, Historia D, Jiografia C, Kiswahili D, English C, Physics D, Chemistry C, Biology C, Basic Mathematics D, ambapo amepata daraja la tatu pointi 24,¡± alisema Bujugo.
Alimtaja mwanafunzi mwingine, Martin Rushaigwa, namba 01197/0173, ambaye alifanya masomo ya ¡®Arts¡¯.Alisema matokeo ya mwanafunzi huyo yanaonesha kuwa ameongezewa alama za masomo ya biashara ya Bookeeping na Commerce, ambayo hakuyafanya kabisa.Alimtaja mwanafunzi mwingine aliyefanya mtihani huo lakini matokeo yake yanaonesha amewekewa ¡®absent¡¯ na mwanafunzi mwingine, Mbazi Volta, hakufanya mitihani lakini amepewa alama za ufaulu.
Hata hivyo, habari zilizopatikana leo hii zinaeleza kuwa uongozi wa shule hiyo uliitwa Baraza la Mitihani ili kuthibitisha madai hayo na ukashindwa kuzithibitisha.Wanasheria wa Baraza la Mitihani wako mbioni kumchukulia hatua Bw. Julian Bujugo kwa upotoshaji huo.
attachment.php
attachment.php
attachment.php
attachment.php
attachment.php
i understand watu wanachukulia past ya green acres kua kisingizio eti wanafunzi lazima kila mwaka wafeli..but msipende kujudge watu kwa past ya shule. Nenda administration ukaulizie matokeo ya mwaka mzima wa green acres form four kabla ya necta. There was no div0 labda itoke moja. I zilikua kibao... The best students now wametoka na 0..something that is impossible.... They will gladly appeal because the results are not true. And if necta has wrongly marked thier exams kisa ya maneno mabovu yanayosambazwa kuhusu iyo shule, they will turn someone in.
 
i understand watu wanachukulia past ya green acres kua kisingizio eti wanafunzi lazima kila mwaka wafeli..but msipende kujudge watu kwa past ya shule. Nenda administration ukaulizie matokeo ya mwaka mzima wa green acres form four kabla ya necta. There was no div0 labda itoke moja. I zilikua kibao... The best students now wametoka na 0..something that is impossible.... They will gladly appeal because the results are not true. And if necta has wrongly marked thier exams kisa ya maneno mabovu yanayosambazwa kuhusu iyo shule, they will turn someone in.
Sasa hayo ni mengine.

tuhuma zote alizotoa dhidi ya Necta na majina yote aliyotaja kama kielelezo cha makosa ya NECTA yamethibitisha kuwa maneno ya Bujugo ni uongo.

Hayo ya best students kupata 0 ni vizuri akafuatilia, lakini kwa sasa tumemjua kuwa ni muongo.

Ajipange upya.
 
Haya ndio madhara ya kutoa number tu bila majina. Hii yote imetokana na matokeo ya Mwanaasha mwaka jana. Wekeni majina na number tuache huu ujinga wa kubadilisha taratibu
 
kaumkuka kweli kweli , lakini suala la kawambwa kujiuzulu lipo pale pale, naona jana alikuwa anajifariji kwa kujichekesha alipokuwa na JK
 
mh jamani, nina mpwa wangu nae kamaliza Lubala sec, anasema ni kweli Alex alifariki mda tu hivyo hukufanya mtihani, sa sijui majibu yametoka wapi, ila yawezekana wanauza hizo namba na majina ya marehem kwa watu wengine


Nani hawajui hii ni vita
dhidi ya Dr Ndalichako ang'oke baraza baada ya kuwadhibiti wezi wote wa
mitihani hapo baraza.
 
Back
Top Bottom