Mkurugenzi wa Halmashauri Songea: Watu 5,720 wamenufaika na TASAF - Songea kati yao waliohitimu ni 1,450

 Mkurugenzi wa Halmashauri Songea: Watu 5,720 wamenufaika na TASAF - Songea kati yao waliohitimu ni 1,450

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Awali, Mdau wa JamiiForums.com alilalamikia utendaji kazi wa TASAF Wilaya ya Songea. Alidai Moja ya changamoto ambayo imekuwa ikitokea ni baadhi ya wahusika kuondoa wanufaika kwenye mfumo kwa vigezo kwamba anajimudu kiuchumi, jambo ambalo halina ukweli.

Mdau aliongeza kwamba, Kuna watu ambao ikifika muda wao wa kwenda kuchukua fedha za TASAF hawazipati na ukifika muda wa wao kwenda kuhoji pia hawapewi majibu ya kueleweka.

Akijibu hoja hiyo ya Mdau, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea, Elizabeth Mathias Gumbo amesema Halmashauri kwa kushirikiana na TASAF wameweka utaratibu mahususi wakupokea na kushughulikia malalamiko kuhusu mpango. Malalamiko hayo hupokelewa kwa njia mbalimbali ikiwemo Simu, Mikutano ya moja kwa moja na wananchi na kujaza kupitia Daftari la malalamiko ambalo lipo katika kila kijiji.

Hapa chini ni Majibu yaliyotolewa na Mkurugenzi...
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea, Elizabeth Mathias Gumbo anapenda kutoa ufafanuzi kwa Mdau wa Jamii forums aliyetoa shutuma kwa kitengo cha TASAF Halmashauri ya Wilaya ya Songea.

Kwanza napenda kuchukua nafasi hii kumshukuru Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwaangalia wananchi wa hali ya chini na kuweka kitengo mahususi chenye lengo la kuziwezesha kaya zenye kipato cha chini, kuongeza kipato, fulsa na uwezo wa kugharamia mahitaji muhimu.

Sisi kama halmashauri tumekuwa tukitekeleza hili kwa kiwango cha juu, kwa kuamini kwamba lengo la Mhe. Raisi ni jema kwa wananchi wake.

Utekelezaji wa mpango wa kunusuru kaya za walengwa kwenye halmashauri ya Wilaya ya Songea ulianza mwaka 2014, ambapo jumla ya vijiji 32 vilihusika kwenye utekelezaji huo, Mpaka mwaka 2021 mpango huu uliweza kufikia vijiji vyote 56.

Jumla ya walengwa walionufaika na Mpango huo mpaka sasa 2024 ni Walengwa 5,720. Walengwa wanaoendelea ni 4,054, walengwa waliohitimu kwa sababu mbalimbali ni 1,450, wengine 216 wapo waolifariki na kuhama Halmashauri.

Walengwa 1450 waliohitimu kwa sababu zifuatazo:-
1. Walengwa 1139 waliopokea Ruzuku ya Uzalishaji kwa lengo la kuanzisha miradi ya kuongeza kipato endelevu katika kaya husika. Miradi hiyo ni pamoja na Ufugaji, Biashara ndogo ndogo na Kilimo

2. Walengwa 311, wamehitimu kutoka kwenye mpango baada ya kufanyiwa uhakiki na Tathmini kisha kujiridhisha hali zao zimeimalika kiuchumi

Halmashauri kwa kushirikiana na TASAF wameweka utaratibu mahususi wakupokea na kushughulikia malalamiko kuhusu mpango. Malalamiko hayo hupokelewa kwa njia mbali mbali ikiwemo Simu, Mikutano ya moja kwa moja na wananchi na kujaza kupitia Daftari la malalamiko ambalo lipo katika kila kijiji. Namna nyingine ni kama ifuatavyo

1. Viongozi ngazi ya kijiji wanawajibu wa kupokea malalamiko ngaji ya kijiji yanayohusu utelezaji wa mpango

2. Malalamiko yakishindikana kupata ufumbuzi ngazi ya kijiji, yanaletwa kwenye Ofisi ya Mkurugenzi.

3. Malalamiko yanayoshindikana kupata ufumbuzi kwenye ngazi ya Halmashauri yaneæenda moja kwa moja TASAF Makao Makuu

Aidha katika kuimarisha usimamizi na uafatiliaji wa shughuli za mpango uongozi wa TASAF Makao Makuu wana utaratibu wa kutembelea Halmashauri kwa lengo la kujionea utekelezaji wa mpango unavyoendele ambapo wamekuwa wakifanya hivyo mara kwa mara.

Hata hivyo kwa mara ya mwisho Octoba 2024, Mkurugenzi wa Fedha pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF walifika Halmashauri ya Wilaya ya Songea kwa lengo la Kujionea utekelezaji wa Miradi ya Miundombinu ya Stendi inayoendelea katika kijiji cha Parangu na Lundusi, Kisha Kijiji cha Mdunduwalo kutembelea mradi wa ujenzi wa Nyumba mbili za watumishi wa Afyana uchimbaji wa kisima kirefu cha maji na vyoo matundu sita. Hata hivyo walipata fursa ya kuongea na baadhi ya Wananchi.

Mwisho napendanda kuushukuru Uongozi wa TASAF kwa ushirikiano wanaotupa kwenye utekelezaji wa mpango ikiwemo miradi mbalimbali ya ndani ya Halmshauri, nawashukuru Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea kwa ushiriki wao kwenye utekelezaji wa mpango na miradi mbalimbali inayotekelezwa kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Songea.

Natoa wito kwa wananchi wote wenye malalamiko, watumie njia jatwa hapo juu ili kupata ufumbuzi wa malalamiko yao."

Imetolewa na
Augustine S. Nongwe
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini (W) Songea 11/12/2024



songea_dctz_0c56cbaadd6941f9aa05b006f3f694c3.jpg
songea_dctz_d2fe0845b09745a095cbffda6b975665.jpg
 
Hata hawa wenzenu taasisi ya umma waliandika uongo! Winchi ni mbovu kwa zaidi ya miaka 2 lakini wakaandika miezi mwili,
Taasisi za umma jitafakarini kwa kuwa waongo!
1731343220099.jpg
 
Wanapiga Mpunga Tu, TASAF Ni Jipu Lililokaa Tumboni
 
Mwenye Number Ya DED Aiweke Hapa Tumtumie Link Ya Huu Uzi
Aone Mwenyewe Wana Ruvuma Wanapotoa Ushahidi
 
Kwanini kiongozi wa ngazi ya huu anapokuja mfano Shadrack Mziray hasikutane Na wananchi ? Anaishia ofisini kwenu Na kuondoka?
 
Jambo jingine Kama mnufaika kaondolewa kwanini asiambiwe kuwa umeondolewa mnampaje majibu aende manispaa, Na mnamuondoaje bila kumpa taarifa rasmi anaendelea Kwenda kituo cha kupokelea Pesa kila mwezi Kama sio kumchosha ili aghairi Pesa ipigwe?
 
Back
Top Bottom