Pre GE2025 Mkurugenzi wa Jiji Dar asema Jiji halitawavumilia wakandarasi wanaochelewesha miradi, Ufungaji wa kamera za CCTV katika Soko la Kariakoo kuanza

Pre GE2025 Mkurugenzi wa Jiji Dar asema Jiji halitawavumilia wakandarasi wanaochelewesha miradi, Ufungaji wa kamera za CCTV katika Soko la Kariakoo kuanza

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

upupu255

Senior Member
Joined
Sep 4, 2024
Posts
119
Reaction score
144
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Elihuruma Mabelya, amesisitiza kuwa jiji hilo halitawavumilia wakandarasi wanaochelewesha miradi.

Tamko hilo amelitoa katika Viwanja vya Karimjee kwenye hafla ya utiaji saini wa miradi mitano muhimu inayolenga kuboresha huduma za jamii na usalama Wananchi ambapo amesema wanataka kuona utekelezaji unafanyika kwa kasi na viwango vya juu ili wananchi wapate huduma bora.

Amesema utiaji saini wa Ufungaji wa kamera za CCTV katika Soko la Kariakoo ni hatua muhimu kwenye kuimarisha usalama wa wafanyabiashara na wateja, ikizingatiwa kuwa soko hilo ni kitovu cha biashara jijini humo.

Hata hivyo Mabelya amesema haflya ya makabidhiano ya maroli ya uzoaji taka yanalenga kuboresha usafi wa jiji na kupunguza changamoto za taka mitaani.

 
Back
Top Bottom