Mdomowabata
Member
- Sep 6, 2020
- 19
- 47
Mheshimiwa Rais sisi wakazi wa Nzuguni A tunakuomba uingilie kati zoezi hili lisiloisha kwa wenye makazi na viwanja katika eneo la Nzuguni A.
Zoezi hili linakaribia mwaka wa tatu lakini imekuwa linaenda kwa kusuasua sana urasimu umekuwa ni mwingi l, ubabaishaji na Rushwa imekithiri kupelekea watu kupoteza haki zao na kupelekea malalamiko mengi yasiyoisha kupelekea kukwamisha ukamilikaji wa mradi huo.
Binafsi ni mmiliki wa ardhi katika eneo hilo pindi nilipotaka kuanza ujenzi baada ya kukopa katika vikoba kulitolewa katazo la kutoendeleza chochote kwa miezi sita mpaka zoezi litakapokamilika basi nilivulia kwa kipindi hicho na sasa ni mwaka wa 3 hakuna kinachoeleweka kwa asilimia kubwa ya milimiki tuliozuiwa kuendelea kwa ujenzi, kwani maeneo mengi ya viwanja walivyopima wameweka maingiliano yaliyosababisha watu kushikiana mapanga,wengine viwanja kumegwa kutokana na miundombinu bila kuainisha utafidiwa vipi, asilimia kuwa tulionunua ardhi huku ni masikini basi imekuwa ni uonevu kupata haki na wale wanaojiweza wamejenga kwa kutumia nguvu zao.
Baada ya malalamiko mengi tuliadiwa kufanyiwa marekebisho kwa wale walikuwa na matatizo katika maeneo yao tokea mwaka Jana mwezi wa kumi lakini mpaka leo ni hadithi na mwenye pesa ndie atakamilishiwa haki ya kupata ardhi yake na sie masikini hatujui hatma yetu tunakuomba mama yetu uingilie kati mradi huu uweze kuisha ili tuendelee na shughuli nyingine za maendeleo ikiwepo ujenzi maana kodi zinatushinda watoto wanakuwa kwenye nyumba za kupanga zilizo finyu kwa kipato chetu.
Kuna wengine walichoka na zoezi hili lisiloisha wameendelea kujenga kukiuka maelekezo ya jiji ya kusimamisha ujenzi wakijiandaa kwa vita yoyote Sie wanyonge tunakuomba uingilie kati mama yetu kutuletea mkurugenzi mwingine huenda akawa na dawa kututatulia changamoto hiyo,asante.