Mkurugenzi wa baraza la manispaa mjini Bi Hasna Attai Massoud Leo mapema amefanya ziara ya kushtukiza ya ukaguzi wa vituo vya dala dala visivyo rasmi ambavyo vilivyo pigwa maraufuku ndani ya manispaa ya mjini pamoja na uwekaji mbaya wa magari.
Katika ziara hiyo Bi Hasna amesema kuwa hali inarizisha ingawa kuna changamoto ndogondogo ambazo zinakutokana na ujenzi wa bara bara unao endelea ambapo ameahidi kukaa pamoja na maafisa wa mamlaka ya mawasiliano pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama kuona wanafanya nini kuepuka changamoto hiyo wakati wa Mchana na jioni.