alexander paulo
JF-Expert Member
- Dec 21, 2011
- 492
- 155
Jana wakati nafuatilia taarifa ya habari ITV saa mbili usiku niliona mgogoro ulipo katika kiwanja mojawapo kilichopo Yombo wilaya ya Temeke lakini wakati mwandishi wa habari anatafuta ukweli wa jambo hilo alipojaribu kumpigia simu Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke ajulikanaye kwa jina la Lusubilo Mwakabibi nataka ufafanuzi wa mgogoro huo kwa kuomba nafasi ya kuonana naye ofisi kwake aliishia kujibiwa kuwa huyo mwandishi hana hadhi ya kuonana naye! Swali ni je wenye hadhi ya kuonana na viongozi hawa ni waandishi wa namna gani?
MKURUGENZI WA MANISPAA YA TEMEKE AACHE KUTISHA NA KUFEDHEHESHA WAANDISHI WA HABARI!
Tarehe 2 Desemba 2020, ITV ilikuwa na taarifa kuhusu kero ya wananchi katika Manispaa ya Temeke. Mkurugenzi wa Manispaa ambaye ni Mteule wa Rais anapigiwa simu na mwandishi wa habari wa ITV kutaka ufafanuzi kuhusu jambo muhimu la kijamii lenye masilahi kwa taifa. Badala ya kujibu au kutoa ushirikiano kwa mwandishi wa habari, yeye anaamua kumfokea mwandishi wa habari kwa kumwambia kuwa, yeye (Mkurugenzi) siyo saizi yake (mwandishi wa Habari), hivyo aliyetakiwa kumpigia simu Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke ni Mkurugenzi [wa ITV?] na wala siyo mwandishi yule wa habari.
Vyombo vya Habari na Waandishi wa Habari katika nchi hii wasipozinduka watakuwa wanakaripiwa na kila Mtendaji wa Serikali. Uhuru wa Vyombo vya Habari katika nchi hii umewekwa mfukoni mwa Serikali na hili la Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke kumfokea mwandishi wa Habari wa ITV ni kielelezo kimojawapo!
Tunamuonya Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke, ndugu Lusubilo Mwakabibi, kuacha tabia ya kuwafokea, kuwadharau na kuwatisha waandishi wa habari. Anahitaji kuwa mnyenyekevu kwa kuwa anakalia ofisi ya umma inayoendeshwa kwa kodi za Watanzania! Kama tuliwahi kuwakemea na kuwaonya wengine, ni wajibu wetu kumkemea na kumuonya na yeye pia! Tunaomba rehema kwake ili atambue kuwa alilofanya halikuwa jema machoni pa Watanzania.
Tunaishauri Serikali isianze kumfuatilia Mwandishi wa ITV aliyeripoti tukio lile na wala ITV isifuatiliwe kwa kurusha hewani tukio lile. Badala yake Serikali ijikite katika kuwaonya na kuwaelekeza watendaji wake kujirekebisha. Tunamshauri pia Mwakabibi asianze kumfuatilia mwandishi, bali ikiwezekana amuombe msamaha mwandishi yule na ITV yenyewe kwa kumnyanyasa mwandishi wake!
Tunatimiza wajibu wetu wa kikuhani kwa Serikali na jamii kwa ujumla (Ezekieli 33:1-20)!
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula - Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki