Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke aache kutisha na kufedhehesha Waandishi wa Habari

alexander paulo

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2011
Posts
492
Reaction score
155
Jana wakati nafuatilia taarifa ya habari ITV saa mbili usiku niliona mgogoro ulipo katika kiwanja mojawapo kilichopo Yombo wilaya ya Temeke lakini wakati mwandishi wa habari anatafuta ukweli wa jambo hilo alipojaribu kumpigia simu Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke ajulikanaye kwa jina la Lusubilo Mwakabibi nataka ufafanuzi wa mgogoro huo kwa kuomba nafasi ya kuonana naye ofisi kwake aliishia kujibiwa kuwa huyo mwandishi hana hadhi ya kuonana naye! Swali ni je wenye hadhi ya kuonana na viongozi hawa ni waandishi wa namna gani?

 
Malaika
 
Nadhani ni kulewa tu kamshahara na tuposho ambatwo wamepata hapo juzijuzi
 
Mwaka 2015 aligombea ubunge Rungwe akashindwa kura za maoni.

Akateuliwa kuwa mkurugenzi wilaya fulani huko Kigoma.

Baada ya uchaguzi mdogo huko ambao ulotokana na kifo cha Kasuku Bilago wa CHADEMA, na CHADEMA kupoteza Jimbo wakiwa na Eliya Michael wao, ambaye kwa sasa nasikia ni kada kindakindaki na mtendaji kata, Mwaka alihamishiwa TMK
 
Kada kindakindaki wa chama gani
 
Nadhani ni kulewa tu kamshahara na tuposho ambatwo wamepata hapo juzijuzi
Sio kweli huyo jamaa pesa anayokitambo tu na sio mtu wa njaa sema Ni amezaliwa hivyo Ni mtu mpenda sifa na utani wa hapa na pale .

Namjua kwa kias chake coz tunatoka sehem moja huko Budokelo -Mbeya .

Kwanza jamaa wanadai Ni kitengo.

Pia huyu jamaa kudhihirisha kuwa hana njaa huko kijijin kwao amejenga bonge moja la bangaloo Ni hatar na nusu .

So elewa jamaa hana njaa kabisa wala hawez kulewa kamshahara ka Uded so uelewe jamaa ndivyo alivyo zaliwa ,utani mwingi ,vituko vya hapa na pale ,sifa za hapa na pale ,pia Ni mtu wa watu sana hana shida.
 
Mitano tena, hii ndiyo CCM halisi
 
Reactions: PNC
Hasafishiki hata kwa jiki acha kumpaisha huyo mlevi ma madaraka. Eti huna hadhi ya kuonana na mimi. Yeye kama nani? Wameondoka waliokuwa na mamlaka kina mkapa na wakawekwa uwanjani siku karibia tatu akina mahiga waliokuwa na heshima zao lakini uliona msiba wake ulivyokuwa

Aache dharau.
 
Nadhani ni kulewa tu kamshahara na tuposho ambatwo wamepata hapo juzijuzi

Kama ni kweli basi huyu Lusubilo Mwakabibi atakua amepoteza hadhi ya kuwa mkurugenzi sasa
Halafu kitu cha kawaida sana alichoulizwa kwanini amepanick kama mwizi?

Maendeleo hayana vyama
 
Naomba unielewe Ndugu sipo hapa kumsafisha huyo jamaa .ila nimekwambia ndivyo alivyo hayupogo sirias sana Ni mropokaj sana .

Sasa nimsafishe kwa kipi ,nimeongea ivo coz namjua kwa kiasi maana natoka nae sehem moja japo vijiji tofaut huko Busokelo-Mbeya .

Hata huko home Ni maaluf sana sabab ya vituko vyake vya hapa na pale ,lakin tukirud kwenye ukwel jamaa hana shida kabisa na Ni mtu wa watu sana
 
Huyu Mkurugenzi ni kiongozi wa hovyo kuwahi kutokea. Nilisikia mbwembwe zake. Hana sifa ya kuwa kiongozi bali jambazi. Nafikiri ana backup nzuri ya kufanikisha yakiyofanikishwa hivyo ndiyo maana alipayuka hovyo. Kiongozi hana maadili. Very poor communication skills.
 
Hii ndio shida ya viongozi wa kuteuliwa, halafu kateua viongozi s/mtaa, kijiji, madiwani, wabunge nchi mzima [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…