BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Agizo hilo limetolewa kupitia Muongozo wa Mashitaka Namba 1 wa mwaka 2022 ambao pia unaagiza upelelezi wa mashitaka kukamilika ndani ya siku 90 na zikizidi iwe kwa kibali maalumu cha DPP.
Aidha muongozo huo umeongeza kifungu cha 131A kinachoweka ulazima wa kukamilisha upelelezi kabla ya kufungua mashtaka isipokuwa kwa makosa makubwa kama Unyang'anyi wa Kutumia Silaha, Usafirishaji Haramu wa Binadamu na Dawa za Kulevya, Umiliki wa Nyara za Serikali na Makosa ya Mahakama Kuu.
Pia, DPP ameagiza watuhumiwa kupewa dhamana wakati upelelezi ukiendelea ili kuhakikisha mahabusu hazina msongamano wa watuhumiwa ikiwa ni pamoja na kufanya ukaguzi kwenye mahabusu za polisi kila wiki.
KUHUSU UKOMO WA MUDA WA UPELELEZI
Mwongozo wa Mkurugenzi wa Mashitaka Namba 1 wa mwaka 2022 unawaagiza Wakuu wa Mashitaka na Vyombo vya Uchunguzi kukamilisha Upelelezi wa Makosa ya Jinai ndani ya siku 90 na endapo zitazidi, DPP atoe kibali maalumu cha ongezeko hilo
Mwongozo huu kupitia Sheria Namba 1 pia unaweka masharti ya Ufunguaji wa Mashitaka kwenye Mahakama za Wilaya na Hakimu Mkazi kupitia kifungu cha 131A ikiwemo kuangalia ukubwa wa shitaka au kosa la mtuhumiwa ili kulinda Haki zake Kisheria.
====
DPP: Upelelezi ukamilike siku 90
By James Magai & Peter Elias
Muktasari:
Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP), Sylvester Mwakitalu ametangaza ukomo wa siku 90 kukamilisha upelelezi wa makosa ya jinai huku akibainisha kuwa yale makubwa mashtaka yake yanaweza kufunguliwa mahakamani hata kabla ya kukamilisha upelelezi.
Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP), Sylvester Mwakitalu ametangaza ukomo wa siku 90 kukamilisha upelelezi wa makosa ya jinai huku akibainisha kuwa yale makubwa mashtaka yake yanaweza kufunguliwa mahakamani hata kabla ya kukamilisha upelelezi.
DPP Mwakitalu ameyasema hayo kwenye mwongozo wa Mkurugenzi wa Mashtaka Namba 1 wa mwaka 2022, unaohusu ukamilishaji wa upelelezi na ufunguaji wa mashauri ya jinai mahakamani.
Mwongozo huo wa Septemba 3 ulioanza kutumika Oktoba mosi, ameuelekeza kwa wakuu wa mashtaka wa mikoa, wilaya, waendesha mashtaka viongozi na kwa wakuu wa vyombo vya uchunguzi nchini.
Katika mwongozo huo, DPP amesisitiza uzingatiaji wa marekebisho ya Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Jinai Sura ya 20 iliyofanyiwa marekebisho kupitia Sheria ya Mabadiliko ya Sheria namba 1 ya mwaka 2022 kwa kuongeza kifungu cha 131A kinachoweka masharti ya ufunguaji wa mashtaka mahakamani katika mahakama za hakimu mkazi na mahakama za wilaya.
Masharti hayo ya lazima ni upelelezi kukamilika kwanza kabla ya mashtaka kufunguliwa mahakamani kwa makosa yote isipokuwa makubwa ambayo mashtaka yake yanaweza kufunguliwa hata kabla upelelezi haujakamilika ni ya unyang’anyi wa kutumia silaha, usafirishaji haramu wa binadamu na dawa za kulevya, umiliki wa nyara za Serikali na makosa mengine yanayosikilizwa Mahakama Kuu.
Marebisho hayo yamesisitiza kama upelelezi haujakamilika mtuhumiwa anatakiwa kupewa dhamana. Katika mwongozo huo DPP amewaelekeza wakuu wa mashtaka na vyombo vyote vya uchunguzi vinavyohusika kufungua mashtaka wahakikishe wanazingatia kifungu cha 131A cha Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Jinai.
“Kesi zote ambazo zimeelekezwa kufunguliwa upelelezi wake ukiwa umekamilika mhakikishe hoja za awali ziandaliwe na kusomwa mahakamani wakati kesi inapofunguliwa. Kwa kesi zilizoruhusiwa kufunguliwa upelelezi ukiwa haujakamilika, mhakikishe upelelezi wake unakamilika ndani ya kipindi kisichozidi siku tisini (90) bila kuathiri maelekezo ya Mkurugenzi wa Mashtaka katika Mwongozo wa ufunguaji wa Mashtaka na ukamilishaji wa Upelelezi wa kesi za Jinai wa tarehe 24 Machi 2022,” amesema DPP Mwakitalu.
Mkurugenzi huyo amesisitiza kesi yoyote ambayo ina sababu ya msingi upelelezi wake kuchukua zaidi ya siku 90, mkuu wa mashtaka wa mkoa anatakiwa kuomba kwa maandishi kwa DPP kibali cha kuongezewa muda wa kuukamilisha.
Ameelekeza kuwa kibali hicho kitaombwa kabla ya siku 90 kukamilika bila kuathiri utaratibu na sheria zinazosimamia ukomo wa upelelezi.
Pia, ameelekeza watuhumiwa ambao sheria inataka wafikishwe mahakamani baada ya upelelezi wa tuhuma zao kukamilika wapewe dhamana wakati wakisubiri kukamilika kwa upelelezi huo.
Kuhakikisha hakuna msongamano wa mahabsu kwenye vituo vya polisi, ameelekeza ukaguzi wa mahabusu za polisi ufanyike kila wiki kna watuhumiwa wasishikiliwe muda mrefu wakisubiri kupelekwa mahakamani.
“Wakuu wa mashtaka wa mkoa, wilaya, waendesha mashtaka viongozi na wakuu wote wa vyombo vya uchunguzi wanapaswa kutekeleza na kusimamia maelekezo ya mwongozo huu,” amesisitiza Mwakitalu.
Akizungumza na Mwananchi kuhusu mwongozo huo, Mwakitalu alisema unasisitiza utekelezaji wa matakwa ya sheria ambayo hayakuweka utaratibu kwa makosa makubwa kufunguliwa hata kabla ya upelelezi kukamilika.
“Sasa mwongozo umeweka utaratibu wa siku 90 kukamilisha upelelezi na kama kuna sababu za msingi za kutokamilika ndani ya muda huo basi wakuu wa mashtaka na wakuu wa vyombo vya uchunguzi wanapaswa kuomba kibali kwa maandishi. Wanapoomba inatusaidia kujua changamoto ni nini na namna ya kushughulika nayo,” alisema.
Maoni ya wadau
Baadhi ya wanasheria waliozungumzia mwongozo huo wamesema hiyo ni hatua nzuri katika mfumo wa haki jinai nchini.
Wakili Fulgence Massawe alisema “hilo ni jambo jema na DPP ameonyesha nia njema kwa kuweka ukomo wa upelelezi lakini jambo hilo liwekwe kwenye sheria.”
Wakili kiongozi wa kampuni ya Haki Kwanza, Alloyce Komba alisema watuhumiwa kufikishwa mahakamani wakati upelelezi haujakamilika lilikuwa jambo la kushangaza katika haki jinai.
Utaratibu huo alisema ulisababisha magereza kujaa mahabusu ambao upelelezi wa kesi zao ulikuwa haujakamilika na akampongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwa kiongozi wa kwanza kuhoji kuhusu jambo hilo baada ya kuapishwa.
“Itasaidia kuondoa uvunjaji wa haki za binadamu ambao kwa sehemu kubwa ulitokana na kutokuwa na mwenendo sahihi kwa mujibu wa sheria,” alisema Komba.
Wakili wa Kujitegemea, Hekima Mwasipu alisema sheria mama inaeleza uhujumu uchumi, dawa za kulevya, ujambazi kwa kutumia silaha na kumiliki nyara za Serikali mtu anaweza kufikishwa mahakamani hata kama upelelezi haujakamilika lakini haijatoa ukomo wa muda wa upelelezi kama ulivyowekwa na DPP.
“Dhamira ni nzuri kwa sababu mahabusu walikuwa wanajaa magerezani,” alisema.
===
Soma Tanzania na uvunjaji wa haki za binadamu uliokithiri: Kwanini umweke mtuhumiwa rumande na hata kumnyima dhamana wakati upelelezi haujakamilika?