Mkurugenzi wa NIDA abadilishwe ili kuongeza mapato na ufanisi ili ijitegemee na kupeleka mapato serikalini kama TRA

Mkurugenzi wa NIDA abadilishwe ili kuongeza mapato na ufanisi ili ijitegemee na kupeleka mapato serikalini kama TRA

Yaani hakuna taasisi inayochosha kusikia habari zake kama NIDA!
 
Ni wakati sasa mkurugenzi wa NIDA abadilishwe.

Ni wakati wa NIDA ijitegemee yenyewe isipewe fedha na serikali tena

Kama NIDA ingepata kiongozi mbunifu ingeingiza mapato mengi sana kama wafanyavyo TRA.

Serikali yetu ifanye yafuatayo:
Mkurugenzi abadilishwe.

Mkurugenzi mpya imarisha kitengo cha TEHAMA vitambulisho vitolewe ndani ya wiki moja na vilipiwe. Fedha zikusanywe.

Watu wanaotaka kubadilisha taarifa zao za vitambulisho vyao wabadilishe kwa njia ya mtandao na mchakato uchukue siku mbili. Kusanya fedha hizo.

Huduma zote zilipiwe kwani ni watanzania wengi sana wanaohitaji vitambulisho.

Kama kazi ni ngumu NIDA iwe chini ya ofisi za uhamiaji wanaohusika na kutoa passport za kusafiria.
Sheria ya vitambulisho vya Taifa ifanyiwe marekebisho ili iwe idara kwenye Taasisi ya Uhamiaji na kutoza pesa kwa aijili ya vitambulisho kuingiza mapato
 
Mtoa mada inawezekana una ajenda binafsi, kwanini umekumbilia abadilishiwe baadala ya kutoa ushauri namna ya kuboresha huduma?. Inawezekana ukawa mmoja ya waliokataliwa kubadilisha taarifa kutoka zile za kweli kwenda za uongo kwa manufaa yako binafsi au mrundi uliekataliwa kupewa kitambulisho cha uraia.
Kila kitu kinaongozwa na Sheria na kanuni. Hivyo usome kwanza Sheria na kanuni ndio uje na hoja sio unakurupuka
Kuna mdau alishawahi kuandika kwenye stories of change juu ya umuhimu wa kitambulisho cha NIDA hapa nchini.

Jinsi alivyojipambanua anafaa kabisa kuwa mkurugenzi NIDA.

Jiulize ni kipi kinazuia vitambulisho vicheleweshe.

Soma hapa: Vitambulisho vya Taifa: Changamoto zinazowakabili wananchi na mwitiko wa Mamlaka (NIDA)

Soma hapa: SoC04 - Suluhisho la changamoto ya upatikanaji wa kitambulisho cha taifa

Soma hapa: Rais Samia, kero ya upatikanaji wa Kitambulisho cha NIDA imenifika shingoni!

Soma hapa: SoC03 - Kitambulisho cha Taifa kiboreshwe ili kuendana na ulimwengu wa kidigitali

Soma hapa: Vitambulisho vya Taifa: Changamoto zinazowakabili wananchi na mwitiko wa Mamlaka (NIDA)

Soma hapa: NHIF: Tutaanza kutambua Wanachama wetu kwa Kitambulisho cha NIDA
 
Back
Top Bottom