Mkurugenzi wa TPA aliyesimamishwa kazi, Kakoko ashikiliwa kwa mahojiano na TAKUKURU


Hawa ni wa kufungwa tu ,hauwezi kucheka na majizi.
 
Huyo jamaa inaonekana alikuwa mpigaji, kajificha kwenye kichaka cha kuaminiwa na Magufuli. TAKUKURU endeleni kuusaka uhalifu wote na mtandao huo uliokuwa TPA.
Ilikuwa hvy mkuu huy bwana alikuwa anachenga anawauzia masara wachin koo hayati mh alikuwa akifika inaonekana yeye yuko sahihi kutimuliwa kunamkosa sasa mwisho wake umewadia maana kasabisha wengi sana kuondoka
 
... bora wapotezee tu maana Jua laweza kugeuza direction; likaanzia West to East! Miradi ile itakuwa na madudu ya hatari!
Umeona eee! Bunge halijawahi kupitisha bajeti yake. Inaonekana huyu Kakoko alikuwa mshirika wa mwendazake
 
Gazeti la the Citizen online limeandika kwamba Kakoko alikamatiwa Morogoro akiwa njiani kukimbia nchi.
 
Sisi wananchi tunataka hapo TPA Kusafishwe, watendaji wote hapo wananuka, hakuna aliye msafi, Takukuru jiongezeni, mhe Rais amewapa tu clue sasa kazi kwenu, hapo Bandari ni ufisiadi tu, wazee kwa vijana wanapiga dili tu.
 
Umeona eee! Bunge halijawahi kupitisha bajeti yake. Inaonekana huyu Kakoko alikuwa mshirika wa mwendazake
... fikiria mtu akihemuka anagawa fedha mabarabarani hadi unajiuliza ni mshahara wake au zinatoka fungu gani hizi? Hakuna kanuni yoyote ya fedha inayoruhusu kitu kama hicho!
 
Bodi ya TPA Pia itakuwa imechangia ubadhirifu huu, ilikuwa wapi?
ni vyema pia wajumbe wa Bodi ya TPA wakachunguzwe kwa undani maana kuna kila dalili......uchunguzi ufanyike kwa wote.
na hatua kali zichukuliwe dhidi yao maaana hao ndio wachawi wa maendeleo ya nchi yetu.
tusioneane haya wala hakuna kuangaliana sura.
 
Kakoko analaumiwa sana Kwa kudharau kila mtu, kutukana wafanyakazi na kuwatishia, style yake ilikua ni copy and paste na watu wengi katika mawizara na idara mbali mbali za Serikali.

Kakoko unalaumiwa pia kujifanya Mungu mtu kwenye kazi za umma umenyanyasa sana watumishi wenzio lakini ukasahau ya Dunia hii ni mengi.

mko wengi na wote kwa nyakati tofauti Mungu atawalipa hapa hapa Duniani.
Mmeumiza watu sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…