Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Bw. Masanja Kadogosa amesema serikali ipo katika hatua muhimu za kuanza ujenzi wa reli ya kisasa ya treni za mwendokasi (SGR) katika mikoa ya kusini.
Akizungumza wakati wa kikao kazi cha Menejimenti ya TRC na waandishi wa habari mkoani Morogoro, Bw. Kadogosa amesema tayari taasisi za kifedha zimeonesha nia ya kutoa kiasi cha Dola za Marekani bilioni 2.4 (zaidi ya Shilingi Trilioni 6.4) kufanikisha ujenzi huo.
"Kuna uwezekano tukaanza ujenzi wa reli ya kusini, tumedhamiria kuanza ujenzi huu na mpango mwingine ni ule unaohusisha ujenzi wa reli ya kilometa 1,053 kutoka Tanga hadi Musoma kupitia Arusha"
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Aidha, Bw. Kadogosa amesema maeneo hayo pia yanafursa hasa usafirishaji wa mizigo kutokana na shughuli za kiuchumi zikiwemo uchimbaji wa madini.
Chanzo: ITV Digital