Mkurugenzi wa zamani wa NIDA, Dickson Maimu akutwa na kesi ya kujibu

Mkurugenzi wa zamani wa NIDA, Dickson Maimu akutwa na kesi ya kujibu

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
1628677691688.jpeg

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemkutana kesi ya kujibu aliyekuwa mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), Dickson Maimu na wenzake wanne na hivyo wanatakiwa kuanza kujitetea.

Maimu na wenzake wanne wanakabiliwa na mashtaka 55 yakiwemo ya kutakatisha fedha na kuisababishia Serikali hasara ya Sh1.175 bilioni.
===
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imewakuta na kesi ya kujibu, aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dickson Maimu na wenzake wanne na wataanza kujitetea, Agosti 25 na 26, mwaka huu.

Uamuzi huo umetolewa leo, Agosti 11, 2021 na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Rashid Chaungu wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili uamuzi kama washtakiwa wana kesi ya kujibu au laa.

Maimu na wenzake, wanakabiliwa na mashtaka 55 yakiwemo ya kutakatisha fedha na kuisababishia Serikali hasara ya Sh 1.175 bilioni.

"Nimepitia mashtaka yote na vielelezo vyote, nimeridhika kuwa washtakiwa wote wana kesi ya kujibu, hivyo wanatakiwa kujitetea" Anasema Hakimu Chaungu.

Hata hivyo, washtakiwa wamedai kuwa watajitetea kwa kiapo na watakuwa na mashahidi na vielelezo.

Hakimu Chaungu baada ya kueelza hayo, ameahirisha kesi hiyo hadi Agosti 25 na 26, 2021 ambapo washtakiwa wataanza kujitetea.

Awali, wakili wa Serikali Mwandamizi, Ladslaus Komanya, alieleza mahakama hiyo kuwa kesi hiyo imeitwa kwa ajili ya mahakama kutoa uamuzi na wao wako tayari kusikiliza.

Itakumbukwa kuwa Agosti 4, 2021 upande wa mashtaka uliieleza mahakama hiyo kuwa wamefunga ushahidi wa mashahidi 26 na vielelezo 45, vilivyotolewa na mashahidi hao.

Mbali na Maimu, washtakiwa wengine ni Ofisa Usafirishaji wa NIDA, George Ntalima; Meneja Biashara wa NIDA, Avelin Momburi; Xavery Silverius maarufu kama Silverius Kayombo na Mkurugenzi wa Sheria NIDA, Sabina Raymond.

Washtakiwa Maimu, Ntalima na Kayombo wamerudishwa rumande huku mshitakiwa Momburi na Sabina wako nje kwa dhamana.

Mwananchi
 
Kesi za kionevu kabisa
Kwa kweli Babati umezidi. Naungana na wote waliokuponda humu. Umezidi kujifanya unajua kila kitu na ushabiki kama wa zezeta. Majina uliyopewa na USSR, akilinene na wengineo unazistahili. Badilika.
 
Huyu mchizi alikua anavaaga bonge la cheni

Hivi Bilioni 1 ni hela ya kujidhalilisha namna hii aisee?

Hivi kwanini mtu unafanya kazi serikalini aisee?

Kwanini usifanye biashara tu kuepuka ungese wote huu?
Kupitia situation kama hizo sio kwa wafanyao kazi serikalini tu....Hata wa sekta binafsi na businessmen wengi wamepitia hali hiyo...Tuna akina manji,rugemalila,seth,nk nk nk….wasiopitia hali hizo muimu ni kushukuru mungu na Maisha kuna ambao watafanikiwa na wengine hawatafanikiwa….ndio maisha
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemkutana kesi ya kujibu aliyekuwa mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), Dickson Maimu na wenzake wanne na hivyo wanatakiwa kuanza kujitetea.

Maimu na wenzake wanne wanakabiliwa na mashtaka 55 yakiwemo ya kutakatisha fedha na kuisababishia Serikali hasara ya Sh1.175 bilioni.

Mwananchi
Sheria huwa inanishangaza sana,
Yaani kipindi chote hicho,mtu yupo ndani,kumbe inatafutwa kama ana kesi ya kujibu au la!
Sasa kwanini hizo taratibu za kutafuta hatia zisifsnywe nikiwa nje?
Mtu kakaa ndani miaka,sasa hv unamuambia anza kujitetea,
Angekuwa hana hatia,huo muda uliopotea,angelipwa?
 
Kupitia situation kama hizo sio kwa wafanyao kazi serikalini tu....Hata wa sekta binafsi na businessmen wengi wamepitia hali hiyo...Tuna akina manji,rugemalila,seth,nk nk nk….wasiopitia hali hizo muimu ni kushukuru mungu na Maisha kuna ambao watafanikiwa na wengine hawatafanikiwa….ndio maisha
X kweli
 
wasisahau kuwashtaki kwa kutakatisha picha yangu ya kwenye kitambulisho kiasi kwamba ukiiangalia picha liliyoko kwenye kitambulisho changu na ukiniiangalia mimi utafikiri ni mimi wa miaka 95 ijayo mpaka nikijiangalia nabaki nalia tu mwenyewe...
 
Back
Top Bottom