Mkusanya Mapato afungwa miaka miwili Jela licha ya kurejesha Tsh. Milioni 10.6 alizoficha

Mkusanya Mapato afungwa miaka miwili Jela licha ya kurejesha Tsh. Milioni 10.6 alizoficha

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Ni Sylivester Vananth, aliyekuwa Mkusanya Mapato ya Halmashauri ya Ngara, Kagera aliyepewa hukumu hiyo na Mahakama baada ya kukutwa na hatia katika Kesi ya Uhujumu Uchumi na Ubadhirifu.

Mshtakiwa alikiri Kosa na kuomba huruma ya Mahakama kwenye upande wa adhabu kwa kuwa ameshalipa Tsh. 10,666,600 alizokusanya kinyume cha Sheria pamoja na kueleza kuwa yeye ni Mgonjwa.

Mbele ya Waendesha Mashtaka wa Serikali kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na baada ya kuona uthibitisha wa malipo ya Fedha, Mahakama ilimpa adhabu ya kutumikia kifungo hicho.
 
Mahakamani hautakiwi kukubali kosa. Unatakiwa uendelee kukataa ili wapambane kupata ushahidi.

Sidhani hao watuhumiwa wa makosa ya uhujumu uchumi waliokuwa wanajadiliana na DPP walikuwa wanakubali makosa yao mahakamani.

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom