Phillemon Mikael
Platinum Member
- Nov 5, 2006
- 10,557
- 8,673
...wakati mkutano mkuu wa ccm unaanza leo kauli mbiu ya MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA YANAWEZEKANA imebadilishwa na sasa mabango yanasomeka MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA YATAKUJA KWA KUJITUMA NA KUFANYA KAZI!! ..yetu macho......"
Hivi kweli Watanzania hawajitumi jamani? Ni wangapi ambao kile kukicha wanahangaika kufanya kweli katika shughuli zao, vibustani, vioski, hadi wanawatuma watoto kwenda kuuza mchicha.. wanaposema kujituma wanataka wajitume kufanya nini?
Watanzania naomba tuwaombee viongozi wetu kwenye Mkutano Mkuu wa CCM. Taifa kwa mwaka huu limekuwa likipatwa na majonzi mengi, na tumwombe Mungu atuepushe na machozi, na wale watakaoangushwa wasiumie mioyo na kudhurika afya. Tumwombe Mungu watakaoshindwa wakubali kushindwa kwa mioyo ya ucheshi! Wingu la huzuni na litanduke toka Anga la Dodoma!