Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,267
Katika kuhakikisha wanafikia malengo yao, Klabu ya Simba SC imewataka wanachama wake kujitokeza kwa wingi katika mkutano mkuu wa mwaka utakaofanyika leo kuanzia saa 4:00 asubuhi kwenye Ukumbi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mwalimu Nyerere.
Kaimu Makamu wa Rais wa Simba, Idd Kajuna, awali aliwahakikishia mwandishi wetu kuwepo kwa mkutano huo ambao licha ya malengo yake kuweka wazi, ni unaelezwa ni kwenda kupitisha uamuzi wa kumuuzia hisa mfadhili wa klabu hiyo Mohammed Dewji 'MO' awe mmiliki rasmi wa Simba.
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara alinukuliwa jijini Dar es salaam jana akisema mkutano wa Jumapili (leo) upo pale pale kufuatia mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es salaam kutupilia mbali ombi la mmoja wa wadhamini wa klabu hiyo, Hamisi Kilomoni kuzuia usifanyike.
"Tunawaomba wanachama kuhudhuria kwa wingi mkutano huo muhimu mahitaji yote yatapatika ikiwemo chakula na vinywaji".
"Uamuzi wa Mahakama ni ushindi mkubwa siyo tu kwa klabu, bali kwa mustakabali mzima wa maendeleo ya mchezo wa soka nchini", alisema Manara
MO anataka kuuziwa asilimia 51 ya hisa za klabu kwa Shs bilioni 20 na baada ya hapo atatumia bajeti ya Shs bilioni 5.5 kwa msimu kwa ajili ya Simba SC, ili kuifanya klabu hiyo kuwa ya kisasa ikiwemo kuujenga Uwanja wa Bunju.
Updates
=>Mkutano mkuu wa Wanachama wa klabu ya Simba unaendelea hivi sasa katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere International Conference Center
=>Mkutano mkuu umeridhia kumsimamisha uanachama wa Mzee Hamisi Kilomoni na kumuondoa kwenye baraza la wadhamini wa klabu ya Simba kwa kupeleka kesi katika mahakama.
=>Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Adam Mgoyi amechukua nafasi ya Hamis Kilomoni ambaye mkutano mkuu umeridhia aondolewe nafasi yake ya udhamini.
=>Prof Juma Kapuya amepitishwa kwa sauti moja na mkutano mkuu wa wanachama kuwa Mdhamini wa klabu ya Simba na kuchukua nafasi ya Marehemu Ally Klaiyst Sykes
=>Mkutano mkuu umeridhia kuwasamehe wanachama 71 kwa sharti la kufuta kesi waliyokuwa wamefungua mahakamani