Mkutano Mkuu wa Klabu ya Simba SC, MO kupewa timu leo

Mkutano Mkuu wa Klabu ya Simba SC, MO kupewa timu leo

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Katika kuhakikisha wanafikia malengo yao, Klabu ya Simba SC imewataka wanachama wake kujitokeza kwa wingi katika mkutano mkuu wa mwaka utakaofanyika leo kuanzia saa 4:00 asubuhi kwenye Ukumbi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mwalimu Nyerere.

Kaimu Makamu wa Rais wa Simba, Idd Kajuna, awali aliwahakikishia mwandishi wetu kuwepo kwa mkutano huo ambao licha ya malengo yake kuweka wazi, ni unaelezwa ni kwenda kupitisha uamuzi wa kumuuzia hisa mfadhili wa klabu hiyo Mohammed Dewji 'MO' awe mmiliki rasmi wa Simba.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara alinukuliwa jijini Dar es salaam jana akisema mkutano wa Jumapili (leo) upo pale pale kufuatia mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es salaam kutupilia mbali ombi la mmoja wa wadhamini wa klabu hiyo, Hamisi Kilomoni kuzuia usifanyike.

"Tunawaomba wanachama kuhudhuria kwa wingi mkutano huo muhimu mahitaji yote yatapatika ikiwemo chakula na vinywaji".

"Uamuzi wa Mahakama ni ushindi mkubwa siyo tu kwa klabu, bali kwa mustakabali mzima wa maendeleo ya mchezo wa soka nchini", alisema Manara

MO anataka kuuziwa asilimia 51 ya hisa za klabu kwa Shs bilioni 20 na baada ya hapo atatumia bajeti ya Shs bilioni 5.5 kwa msimu kwa ajili ya Simba SC, ili kuifanya klabu hiyo kuwa ya kisasa ikiwemo kuujenga Uwanja wa Bunju.

Updates

=>Mkutano mkuu wa Wanachama wa klabu ya Simba unaendelea hivi sasa katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere International Conference Center
557a8bc2ec999f71b8ba78a18ad5be04.jpg

=>Mkutano mkuu umeridhia kumsimamisha uanachama wa Mzee Hamisi Kilomoni na kumuondoa kwenye baraza la wadhamini wa klabu ya Simba kwa kupeleka kesi katika mahakama.

=>Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Adam Mgoyi amechukua nafasi ya Hamis Kilomoni ambaye mkutano mkuu umeridhia aondolewe nafasi yake ya udhamini.

=>Prof Juma Kapuya amepitishwa kwa sauti moja na mkutano mkuu wa wanachama kuwa Mdhamini wa klabu ya Simba na kuchukua nafasi ya Marehemu Ally Klaiyst Sykes

=>Mkutano mkuu umeridhia kuwasamehe wanachama 71 kwa sharti la kufuta kesi waliyokuwa wamefungua mahakamani
 
Sijawahi kumwona mhindi akiendesha biashara yake Kwa hasara..... Simba ndo baibai... Nilikuwa nashangaa sana huu usajili hela inatoka wp? Ndo basi tena....Wanachama hamna sauti tena ndani ya club

Sent using Jamii Forums mobile app
Hata wewe huwezi kuanzisha biashara kwa lengo la kupata hasara

Na si kweli kuwa Simba baibai, mbona mambo yote yako wazi juu ya hili?
 
Nimekua mshabiki wa simba kwa miaka mingi lakini kuanzia sasa..sitakaa niishabikie tena..pumbavu sana hawa viongozi wa hii club....imejaa ujinga na ubabaishaji..kila siku mambo mapya ya kipuuzi yanaibuka..no focus at all nonsense.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naona Mo atanifanya angalau niwe nafuatilia soka la bongo maana ubabaishaji siasa ujinga vilikua vinaua soka letu afadhali uku tuendako tutapata timu nzuri ya taifa

Sent using Jamii Forums mobile app

MO ni mfanyabiashara, anaweza kutufanyia kama alivyoifanya African Lyon vile vile! ingependeza kama mchakato ungekuwa wazi tukapata several bidders tuka chagua the best evaluated bidder, labda tungepata matumaini,
 
Nimekua mshabiki wa simba kwa miaka mingi lakini kuanzia sasa..sitakaa niishabikie tena..pumbavu sana hawa viongozi wa hii club....imejaa ujinga na ubabaishaji..kila siku mambo mapya ya kipuuzi yanaibuka..no focus at all nonsense.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa si bora iuzwe iwe kama azam kuliko ilivyo sasa na wapiga dili miaka hamsini hata uwanja hakuna?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sijawahi kumwona mhindi akiendesha biashara yake Kwa hasara..... Simba ndo baibai... Nilikuwa nashangaa sana huu usajili hela inatoka wp? Ndo basi tena....Wanachama hamna sauti tena ndani ya club

Sent using Jamii Forums mobile app

Klabu kubwa zote zenye mafanikio tunazozipenda mimi na wewe duniani haziitambui sauti ya mwanachama Bi. Hindu.
 
Sijawahi kumwona mhindi akiendesha biashara yake Kwa hasara..... Simba ndo baibai... Nilikuwa nashangaa sana huu usajili hela inatoka wp? Ndo basi tena....Wanachama hamna sauti tena ndani ya club

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwani Manji alikuwa mzungu? Hao unao wasema walikuwa wapigaji na ndio maana wanajiita tu wadhamini wa club wanakimbilia kuzuia mkutano Kwa sababu ulaji wao utakoma timu ina resources kibao alafu inakuwa maskin hii yote ni kwa sababu ya viongozi njaa tuliokuwa nao big up Mo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
MO ni mfanyabiashara, anaweza kutufanyia kama alivyoifanya African Lyon vile vile! ingependeza kama mchakato ungekuwa wazi tukapata several bidders tuka chagua the best evaluated bidder, labda tungepata matumaini,
Aisee asidanganye mtu kuwa mfanyabiashara sio tatizo Wamiliki wa vilabu vyikubwa Duniani wote ni Wafanya biashara tena wakubwa sikatai MO kaona kuna tija katika hilo kwani kupitia ilo atatangaza vzr biashara yake, alafu ikumbukwe mwaka 2003 simba inaingia hatua ya makundi MO ndiye alisimamia show zote ikiwa ni pamoja na kuipeleka timu Oman kufuliwa na Talib Hilali tukafanikiwa kuwa galagaza Zamaleki ya Misri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sijawahi kumwona mhindi akiendesha biashara yake Kwa hasara..... Simba ndo baibai... Nilikuwa nashangaa sana huu usajili hela inatoka wp? Ndo basi tena....Wanachama hamna sauti tena ndani ya club

Sent using Jamii Forums mobile app
Refer moses katumbi na Tp mazembe,Abrahamovic na Chelsea,Mimi naona sawa,hata kama hawatakua na sauti kumbuka tangu club ianzishwe,ilikuwa mikononi mwao kipindi chote hiko na hakuna cha maana walichokifanya,wampe Mo dewji naye aonyeshe uwezo wake.
 
Back
Top Bottom