Mkutano wa CCM Dodoma ulikuwa na ulazima wakujaza wasanii na waandishi wa habari?

Mkutano wa CCM Dodoma ulikuwa na ulazima wakujaza wasanii na waandishi wa habari?

Resilience

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2023
Posts
1,096
Reaction score
4,948
Waandishi wa habari na wasanii wameondoa kabisa seriousness ya Mkutano mkuu wa CCM Dodoma. Ni vigumu kwa compositions hii watu wakafuatilia mkutano unavyokwenda kwa sababu waandishi wa habari wapo katika comedy style kuliko kuripoti mambo ya msingi

Vyombo vya habari vinaripoti magari ya CCM mengi jambo linalopelekea mwananchi mwenye njaa aone kama viongozi wa CCM wameshiba na hawana shida na kero za wapiga kura.

Vyombo vya habari vinaripoti viongozi wanavyowasili bila kufanya mahojiano ya kina kuhusu nini agenda ya mkutano husika.

Imefika mahali comments zinazotolewa mitandaoni zinakitukanisha chama kuliko kukijenga. Nadhani wakina Makala wanapaswa kuona kama upo umuhimu wa kubeba waandishi wa habari wote na kuwapeleka Dodoma.

Kuona kama kulikuwa na umuhimu wakionyesha msururu wa magari mamia kwa mamia yakielekea Dodoma katika nchi ambayo wanafunzi wanakaa chini na baadhi ya watoto hawana bima ya afya.

Tunapokwenda kwenye uchaguzi lazima tuangalie alama za nyakati. Mitandao imepanuka sana, kurekodi msururur wa magari ya kijani na kusambaza ilipaswa ipigwe marufuku kwa sababu inaleta tafsiri kwamba viongozi waliopo wanakula urefu wa kamba yao.

Tunategemea updates ziendane na yale maamuzi yanafanyika ndani ya mkutano ili wananchi waweze kusikiliza mipango mipya ya chama kwasaa.
 
Back
Top Bottom