Mkutano wa G20 ni Tanzania pekee imepeleka wajumbe wengi sana, watu 100+kuliko hata wajumbe wa Brazili mwenyeji

KIONGOZI MAKINI NA MTAFUTA FULSA MWENYE AKILI NYINGI NI MAMA SSH AMEBEBA UJUMBE MKUBWA ILI KWENDA KUPAMBANIA FULSA ZILIZOPO KULE YAANI KAKABA KILA ANGLE HYO NDIYO MAONO YA MAMA YETU MPENDWA SSH SUBIRINI MATOKEO CHANYA YA ZIARA HIYO YENYE UJUMBE MZITO MUONE TAIFA LINAVYOFAIDIKA PAMOJA NA WEWE UNAYESHANGAA KWENDA NA WATU WENGI
 
MAMA ANACHUNGULIA FULSA ZA KUWALETEA WATANZANIA UKIWEMO WEWE MSHANA JR ACHENI UTOTO MAMA ANAUPIGA MWINGI
 
Anaupiga mwingi
 
Fursa hasotafutwi kwa kubeba rundo la watu, yeye ndio pekee anajua furusa?
 
Si mnamsifia kufungua nchi mwacheni afungue nchi.
 
We hauna akili,sasa mbona tofauti ni ndogo sana,maana kuna mwingine hapo ana wajumbe 90,mwingine 70,

Acheni chuki zenu,Samia akimaliza awamu yake 2035,atakuja mnaempenda ambae ni Rais Mwinyi wa Znz au Kassim Majaliwa,

Yaani mnalaumu kila kitu aisee,nikweli serikali ina mambo mengi ya ovyo,lakini sasa lawama tumezidisha
 
Watakosa viti vya kukalia, labda baadhi ni wasindikizaji mkutano hauwahusu wako wanapiga misele tuu😂
 
Nchi ya hovyo hii🤣

Kamata mjumbe mmoja umuulize maswali mawili matatu akudadavulie alichoambulia huko, anaweza asiwe na jibu lililonyooka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…