Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MBUNGE JULIANA SHONZA AFYA MKUTANO WA HADHARA KATA YA IFWEKENYA WILAYA YA SONGWE KUELEZEA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Songwe, Mhe. Juliana Daniel Shonza ameendelea na ziara katika Kata mbalimbali za Mkoa wa Songwe huku alitembelea Wajasiriamali wa vikundi mbalimbali alivyovianzisha na kuvipa mitaji ya Shilingi 300,000 kila kikundi
Mhe. Juliana Daniel Shonza amefanya mikutano ya hadhara Kata kwa Kata na kuelezea utekelezaji wa Ilani ya CCM 2020-2025 na utendaji wa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan
Mhe. Shonza amesema kuwa katika mwaka huu wa fedha 2023-2024 Serikali imepanga bajeti ya ujenzi wa barabara ya Mbarizi hadi Mkwajukuni yenye Kilomita 86 ambayo itafungua kazi mbalimbali za kiuchumi kama usafirishaji kwa wananchi wa maeneo hayo
Vikundi vya wanawake wajasiriamali katika Kata ya Ifwekenya vinajishughulisha na Ufugaji wa Kuku, Biashara za Vitenge & Kilimo cha Ufuta na Karanga ambavyo vimewezeshwa na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Songwe, Mhe. Juliana Shonza
Aidha, Wanawake wajasiriamali wamempa zawadi ya Kuku, Vitenge, Mafuta, Ufuta na Karanga na wamempongeza sana Mhe. Juliana Shonza kwa kazi nzuri anayoifanya ya kuwapa semina ya ujasiriamali na kuwapa mitaji ambavyo vinawasaidia kuendesha shughuli za uzalishaji ndani ya Mkoa wa Songwe.
Wakizungumza katika Mkutano wa hadhara, viongozi mbalimbali wa Kata na wananchi wamemshukuru Mbunge Juliana Shonza kwa kufanya mkutano na kuwaeleza mazuri ya Serikali kwani na wao pia wamepata nafasi ya kuzungumzia changamoto zao mbele ya Mbunge ambaye naye amekiri kuzipokea na kuzifanyia kazi.