Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Mkutano wa kampeni za mgombea urais wa Zanzibar, kwa tiketi ya chama cha ACT-Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad jimbo la Mpendaye.
Leo tarehe 08/10/2020, Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya chama cha ACT Wazalendo Maalim Seif Sharif Hamad amefanya mkutano wa hadhara kwa kuwakutanisha Wananchi wa jimbo la Mpendaye, Mkutano uliofanyika katika kiwanja cha Binti Amrani Mkoa wa Mjini Magharib Unguja.
Maalim Seif ameanza kwa kusema Elimu ya Zanzibar ilikuwa ya kiwango kikubwa sana miaka ya nyuma lakini chini ya Serikali ya CCM elimu imeshuka sana na hii inatokana na sera mbovu za Elimu ambazo Chama cha CCM inaziendesha.
Maalim Seif pia amesema Idadi kubwa ya wanafunzi darasani ni chanzo kikubwa cha kupelekea wanafunzi kutokumuelewa Mwalimu darasani na kupelekea wanafunzi kufeli.
Kuhusu ubora wa Waalimu, Maalim Seif amesema wapo Waalimu wengi ambao wamesoma na wana weledi, lakini hawapewi ajira na badala yake ajiza za ualimu zinatolewa kwa kujuana au itikadi ya chama, jambo ambalo linachangia kuporomoka kwa Elimu Zanzibar kwani wanaoajiriwa ni Waalimu ambao hawana weledi katika taaluma hio.
Maalim Seif amesema tatizo jengine linaloikabili sekta ya elimu ni Kudharauliwa kwa waalimu, Maalim Seif ameeleza kwamba Waalimu wanatumika kisiasa, kwani hulazimishwa kuhudhuria mikutano ya chama cha CCM na zaidi maslahi yao kimshahara yapo chini.
Baada ya kero hizo alizoziainisha Maalim Seif ameeleza pia namna atakavozitataua pindi tu atakapokuwa Rais wa visiwa vya Zanzibar.
Kuhusu Mikopo kwa wanafunzi, Maalim amesema;
‘’Katika Serikali yetu Wanafunzi wa Kizanzibari watasoma bure kuanzia elimu ya msingi mpaka chuo kikuu, na zaidi tutafuta madeni yote ambayo wanafunzi wa elimu ya juu wanadaiwa kama mikopo’’.
Alipozungumzia suala la wingi wa wanafunzi katika vyumba vya madarasa Maalim Seif alisema;
“Chini ya Serikali yetu nitahakisha suala la kuongeza Majengo ya kusomea kuanzia shule za msingi yanapewa kipaombele ili wanafunzi wasizidi 35 kwa kila darasa tutatofautisha na ile ya sasa chini ya CCM ambapo darasa moja kuna zaidi ya wanafunzi 100, nitafanya hivi ili Mwalimu awe na uwezo wa kuwadhibiti sambamba na Wanafunzi kumuelewa vyema Mwalimu’’.
Maalim Seif amesema vikalio vya Wanafunzi (madawati) kwa mashule mengi Zanzibar hasa shule za msingi vimekuwa changamoto sana, ila chini ya utawala wake atahakikisha suala hili linapatiwa ufumbuzi kwa haraka ili kila mwanafunzi ajifunze akiwa katika mazingira mazuri.
Maalim amesisitiza kwamba katika kulipa nguvu suala la ufaulu wa Wanafunzi atahakikisha vile vyote vinavohitajika kupatiwa mwanafunzi katika kujifunza kwake kama vile Madaftari, Kalamu, Vitabu na Computer vitapatikana bure mashuleleni, na zaidi atahakikisha vifaa vya masomo ya Sayansi kama vifaa vya maabara vinapatikana ili kuleta hamasa zaid katika masomo ya Sayansi.
Akizungumzia juu ya maslahi ya Waalimu, Maalim Seif amesema atahakikisha heshima na hadhi ya Mwalimu katika nchi ya Zanzibar inarejea na kuheshimika zaidi, kwanza atahakikisha mishahara yao inakuwa toshelezi lakini pia Mwalimu hatolazimishwa kuhudhuria shughuli za kisiasa bali atafanya kwa matakwa yake mwenyewe kwani atakuwa ni mtu huru.
Maalim Seif amesema atarudisha pia vyuo vya Uwalimu vyenye hadhi Zanzibar ili tuweze kupata Waalimu wenye ubora na weledi.
Akimalizia hutuba yake Maalim Seif amesema waalimu wa masomo ya dini wametelekezwa mno, Maalim amesema Waalimu hawa kwakiasi kikubwa wao ndio wanao wafundisha watoto na jamii kwa ujumla kuishi katika maadili mema, Akielezea kuhusu hilo Maalim Seif amesema na waalimu wote wa elimu ya Dini wataingia katika malipo ya serikali na kila mwisho wa mwezi nawao watapokea mishahara kama wafanyakazi wengine wa Serikali.
Kesho tarehe 09/10/2020, itakuwa ni zamu ya jimbo la Paje na Makunduchi na Mkutano utafanyika katika uwanja wa Skuli ya Paje kuanzia saa 8:00 Mchana mpaka saa 11 jioni.
Abeid Khamis Bakar
/Afisa Habari na Uenezi
ACT Wazalendo Zanzibar.