Mkutano wa Kitaifa wa Kutafakari Hali ya Kisiasa Nchini Siku ya Pili, Septemba 8, 2026

Mkutano wa Kitaifa wa Kutafakari Hali ya Kisiasa Nchini Siku ya Pili, Septemba 8, 2026

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876

Kituo cha Demokrasia Tanzania chenye wanachama wanaojumuisha CCM, CHAUMA, ACT Wazalendo, Chama cha Wanannchi CUF pamoja na NCCR Mageuzi leo wanakutana kuzungumza kuhusu hali ya demokrasia Tanzania, na matukio ya wakati wa uchaguzi na baada ya Uchaguzi Oktoba 29, 2025.

Othman Masoud Othman (Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa ACT Wazalendo) ametoa mwelekeo wa kina kuhusu kutatua mkwamo wa kisiasa Zanzibar. Hotuba yake imeangazia changamoto za kimfumo kwenye chaguzi zilizopita, ajenda ya mambo saba ya maridhiano, na sababu za msingi za chama chake kuingia kwenye Serikali ya Umoja wa Kitaifa (GNU).

Amebainisha kuwa makubaliano mengi ya awali ya kusafisha mfumo wa uchaguzi yalipuuzwa:
  • Kura ya Mapema: Licha ya makubaliano ya kuifuta, mfumo huu ulitumika. Badala ya wapiga kura takriban 2,000 waliotarajiwa kisheria, karibu watu 52,000 walipiga kura siku ya kwanza, na wengi wao walijirudia siku zilizofuata.
  • Kunyimwa Vitambulisho (ZAN ID): Makubaliano ya kuwapatia vitambulisho wananchi zaidi ya 21,000 waliokuwa na sifa hayakutekelezwa.
"Daftari la wapiga kura limeendelea kuwa na changamoto, likiwa na majina ya watu waliofariki na wasio na sifa... misingi ya uchaguzi huru ilipuuzwa."

Ili kujenga suluhu ya kudumu ya kisheria badala ya makubaliano ya maneno matupu, pande zote zimekubaliana mambo yafuatayo:

  • Kurejesha Imani: Kugeuza ahadi za kisiasa kuwa utekelezaji halisi wa kiserikali.
  • Tume Huru ya Uchunguzi: Kuunda jopo la wataalamu huru kuchunguza changamoto za uchaguzi wa 2025 na chaguzi zilizotangulia.
  • Mageuzi ya Tume ya Uchaguzi: Kufanya maboresho makubwa kwenye sekretarieti na utendaji wa Tume.
  • Kupunguza Mamlaka ya Rais: Kurekebisha Katiba ili kupunguza nguvu zilizopitiliza za Rais kwenye teuzi ("Imperial Presidency"), na kujenga mfumo bora wa uwajibikaji.
  • Mageuzi ya Serikali za Mitaa: Kupitia upya mfumo wa Masheha na kusafisha daftari la wapiga kura.
  • Tume ya Taifa ya Maridhiano: Kuanzisha chombo cha kudumu cha kutatua migogoro kabla haijaleta madhara.
  • Kamati ya Mashauriano: Kuunda chombo maalum cha kutatua changamoto za kiutawala wakati wa uchaguzi.

    Aidha ameongeza kuwa "Zaidi ya 95% ya uchumi wa Zanzibar unategemea sekta ya huduma na utalii, ambayo inahitaji amani ya kweli. Ili Zanzibar ijiendeshe vizuri, inahitaji kukusanya kati ya Dola Bilioni 3 hadi 4 kwa mwaka. Kwa sasa, inakusanya chini ya Dola Bilioni 1.3. Pato hili haliwezi kukua bila utulivu thabiti wa kisiasa.
 
Ukija uchaguzi wanawabana mbavu kisha wanawaita mezani mnapewa cheo mnatulia CCM hawajawahi kuwa na nia njema hata kidogo.
 
Mzee kahudhuria? Au bado afya haijakaa sawa?
 
Back
Top Bottom