Elections 2010 Mkutano wa lala salama wa CHADEMA uko Igunga wafunika

Ni kweli CCM wanaweza kuwa wanaiba kura lakini pia nafikiri mashabiki wetu ni watu waliokata tamaa, vijana wa vijiweni ambao wengi wao hawajajiandiksha.

Ukitaka ujue vijana walivoamka angalia Mbeya ilikuaje, Vijana hao hao ndo waliomfikisha Sugu Mjengoni uje hapa Ubungo kwa Mnyika, kwa Mdee ndo vile vile, Arusha ndo kabisa, Takwim unazoleta hapa ni za 2005 na sio karne ya sasa ambayo vijana wanahitaji mabadiriko
 
Ushindi ni wachadema mapema, View attachment 38170
picha hii ya leo

watu weweeeee!!!!! hii inatia moyo kwa kweli, na wakichakachua watu watajua na wachakachuaji watajipalia makaa zaidi kwa 2015, ushindi au la, mesage sent..imewafikia walengwa.

kwa wenye magamba, kujivua magamba hakutoshi, tunahitaji full blood and brain transplant kwa sababu ufisadi wenu uko damuni na ubongoni.
 
Nimeangalia ITV taarifa ya hbr usiku huu mkutano wa CDM funika bovu ulkifuatiwa na wa CCM wa mwisho ni CUF......Nasubiri kifo cha CCM leo 2 oct, 2011.
 
Mabadiliko ni Muhimu na yakitaka kutokea huwezi kuzuia kwa njia yeyote. Ccm kubalini the Game is oveq
 
KAFU NGANGANGARI MUHONA AJIZIKA MWENYEWE RASMI KI-SIASA DAKIKA ZA MAJERUHI IGUNGA

Ndugu Mwita Maranya na Ephata Nanyaro,

hebu pekueni huyu kijana hapo chini mwenye T-sheti nyekundo ambaye yuko karibu na hao maafisa polisi ili mkaangalie kama kweli huo mfuko wa nyuma uliotuna sana kama si shahada za kupiga kura.

Pengine ndicho kilicholeta ngumi mambo kuparaganyika mara baada ya wapiga kura wa Igunga kulamba hela zake Mahona na kadi vile vile wakatolea nje.

Ni kweli kabisa ukimuangalia sana usoni huyu Mahona, utaona kama vipi wananchi walimwambia kwamba 'KULA NI KWA KAFU NA MAGAMBA ILA KURA KESHO NI KWA MAGWANDA' tu - kama unakataa kwa nini mgombea mzima alipuke na hasira mpaka kuharibu harusi yake mwenyewe???

Hebu muone alivyojinunisha mpaka akabadilika mweusi wa GIZA GIZA vile wakati anajua hata ngumi hawezi kurusha marambili hewani kabla hajapoozwa kama maji ya mtungi ...

Huu ni ushindani wa kidemokrasia na wala si kwa ajili ya masumbwi, kubaka wala kuchoma nyumba za watu Igunga.

Pisha huko bwana harusi wa kweli Ndugu Kashindye akachukue nafasi yake stahiki kiulaiiiiini vile.
 
Chadema kiboko kumbe imewalambisha CCM mawakala feki magalasa kwa uroho wao wakawahonga sijui wamekula ngapi ngapi dah ndio maana January alikuwa anasisitiza mawakala hawawezi kubadilishwa na lazima watoke Igunga poleni sana watani.
 
duh nilicheka sana usiku namna habari ya mkutano wao ilivyo chakachuliwa.. Yaani ilituliwa kwenye tukio bwaa! Inaonekana ilimaliziwa kuchakachuliwa ghafla muda ule na TBC, make hakukuwa na picha iliyoonesha umati live toka jukwaani na nina wasiwasi zile picha zilichanganywa na viporo vya picha za mikutano yao ya awali!

Hongera CDM, KWANI MMEWALAZA MAGAMBA CHALI WANAHAHA NA MSTAAFU WAO MKAPA! Maji yamewafika shingoni! Wakilichukua hili lazima na Niliyehuku Bukoba ntaandamana... Mwisho wenu umefika MAGAMBA
 
QUOTE=kuberwa;2576260]duh nilicheka sana usiku namna habari ya mkutano wao ilivyo chakachuliwa.. Yaani ilituliwa kwenye tukio bwaa! Inaonekana ilimaliziwa kuchakachuliwa ghafla muda ule na TBC, make hakukuwa na picha iliyoonesha umati live toka jukwaani na nina wasiwasi zile picha zilichanganywa na viporo vya picha za mikutano yao ya awali! Hongera CDM, KWANI MMEWALAZA MAGAMBA CHALI WANAHAHA NA MSTAAFU WAO MKAPA! Maji yamewafika shingoni! Wakilichukua hili lazima na Niliyehuku Bukoba ntaandamana... Mwisho wenu umefika MAGAMBA[/QUOTE]

picha ya wahudhuriaji wa ccm iliyoonyeshwa TBC kwenye taarifa ya habari haikiwa ya leo, yani aibu kubwa mkutano ulikuwa hauna watu, mzee Mkapa amejitia aibu tu!
 
Nimeanza kupata mashaka kesho CCM watachakachua kura, maana kama hata moderator anachakachua thread zetu hapa jamvini ni hatari. Yani mie nimeanzisha thread inayoendana na hii heading yeye kachakachua kaweka habari nyingine ambayo hata haiendani, sijui tumueleweje!
 
saa moja imeshatimu, Makamanda wetu mliopo Igunga mambo yanaendeleaje?
 
eeee Mungu unawasikia wanaoniotea mabaya, naomba uwe kwangu ngao na kigao ili wafedheheke wote wanaoiotea mabaya CDM,
NI WAKATI ULIOUPANGA WEWE KWA MABADILIKO YA TAIFA LETU NAOMBA UTUSAIDIE ILI JINA LAKO LITUKUZWE CDM ITAKAPOSHINDA NGUVU ZOTE ZA MAFISADI NA HILA ZA CCM. Hakika tutakutolea dhabihu za kushukuru kwa matendo yako makuu.
Tunafahamu kuwa tunashinda na zaidi ya kushinda katika wewe uliyetupenda.
 
Amen!!!!!!!!!!!!!!

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…