Wakati mkutano ukiendelea, nilipata fursa ndogo ya man to man na Maalim Seif nikamtupia dukuduku langu la moyoni kuhusu uchaguzi mkuu ujao, nilimuuliza nimekwenda Pemba, nimeshuhudia wafuasi wake wakiendelea kususia zoezi zima lauboreshaji wa daftari la kudumu la kupiga kura, maadam yeye na Karume weshamaliza tofauti zao, kwanini mpaka sasa hatatoa tamko rasmi kuwataka wafuasi wake wakajiandikisha?.
Seif akajibu, ni kweli yeye na Karume, wamemaliza kabisa tofauti zao, kinachoendelea sasa, tuvute subra tuone mambo yanivyokwenda, ndipo atawahimiza wafuasi wake wakajiandikishe., hawawezi
Seif amesema, matatizo ya uandikishaji ni moja ya maeneo viiini vya mgogoro, kama walisusia kutokana na matatizo, hawawezi kwenda kujiandikisha ili hali matatizo yangalipo.
Pia alininong'oneza kwa sauti ndogo ' mambo mazuri sana yanakuja, tuvute tuu subra tuone'
Huu ni uthibitisho kuwa mazungumzo ya Seif na Karume, was not only a handshake, but there is a undisclosed substance in it, only time will tell.