incognitoTz
Senior Member
- Apr 19, 2019
- 133
- 172
Februari 28, 2025, Donald Trump kupitia mtandao wa X, alimkashifu Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky kwa kutoheshimu nchi ya Marekani wakati wa mkutano wake na raisi huyo katika ikulu ya Marekani. Trump alimkosoa Zelensky juu ya kutoheshimu nchi hiyo kwa kuidharau ndani ya ofisi ya "oval" na kuongezea kuwa - "Anaweza kurudi kama atakuwa yuko tayari kwa Amani" -
Ukosaoaji huu umemuweka Zelensky aonekane kama mtu asiye na msimamo katika kutatua mgogoro kwa njia ya mazungumzo ya amani kati ya Urusi na Ukraine, jambo linalokinzana na msukumo wa Trump wa kutafuta muarobaini wa mgogoro huo kwa njia ya haraka.
Licha ya rais wa Ukraine kuonekana mtu mwenye kupenda kujibizana, kwenye hili ameonesha kukwepa mitego ya Trump inayolenga kumfarakanisha na watu wa Marekani.
Dakika thelathini tu baada ya kuondoka katika Ikulu ya Marekani alichapisha kwenye mtandao wa X, akiishukuru Marekani na kusisitiza "amani ya haki na ya kudumu" bila ya kujibu shutuma za Trump. Hii inaakisi mtazamo na nia yake ya tangu awali ya kutovunja mahusiano na nchi hiyo: Ukizingatia alipokaa kimya kipindi Trump alipomwita "dikteta" mnamo Februari, Zelensky aliikwepa hoja hiyo kwa kuto kumjibu Trump, huku akihamisha shutuma kwenye upotoshaji wa nchi ya Urusi.
Kujishikiria kwa Zelensky hakutokani na busara tu bali uhitaji wa kuihusisha marekani katika kuumaliza mgogoro wake na nchi ya Urusi.
Wakati mazungumzo ya amani yakiwa yanaendelea ni vyema kwa Ukraine kutopoteza kuungwa mkono na Wamarekani, ili kufanikisha hilo, rais Zelensky atapaswa kutanguliza diplomasia huku akipigania maslahi ya Ukraine kwenye mchakato huu wa makubaliano.