Mkutano wa waandishi: Lipumba, Shelukindo, TANESCO na PPRA

vita dhidi ya ufisadi karibu inaishia tena kwa kushindwa vibaya. Kinachoendelea sasa ni vita ya Rostam v's Mwakyembe, Zitto v's Mwakyembe, Rostam v's Sitta, Zitto v's Chadema national leaders, CCM (mafisadi) v's CCM (maadili), Lipumba + Zitto v's Upinzani, Rostam + Manji + CCM (mafisadi) v's Mengi nk.

Kati ya hawa mafahari kuna wenye dola, wenye madaraka kisiasa, wenye mapesa, wenye vyombo vya habari ... almost all resources. Hivyo Mhe. Rais Kikwete hana pressure tena ya kuwashughulikia mafisadi, anatulia kimyaaa huku Watanzania tukiwa washangiliaji katika kushindwa. LOL!
 
Huyo ni Lipumba amesha mwaga hoja. Bado PPRA na Zitto nao si watazungumza na wahariri leo leo na kumwaga hoja? Hongera Ngeleja na Dr Iddrissa, nchi haipaswi kuwa gizani kwa sababu ya ushabiki wa wakina Mwakyembe.


........ndiyohiyo
 
Ilishasemwa earlier, kama TANESCO or whoever angetaka kununua, they had an option of doing that bila kuihusisha public na Bunge or whatever. The govt has all the powers and Tanesco is its agency (or company).

Hata Ndege ya rais na rada zilinunuliwa katikati ya 'controversies' hata hivyo zikaendelea. Lakini hatimaye ilikuwa wazi ni kwa nini kulikuwa na controversies. All deals were rotten. Hata hivyo ziliendelea, ingawa tunajua kilichotokea na hata wakati ule tulijua!! Hata hili pamoja na hizi zig-zag mara yes, mara no, tunajua msimamo wa walioshika mpini ni nini. Hawaitaji kuungwa mkono, wala nini. Wanahitaji kumaliza mkataba huu ambao baada ya miaka mitatu tutajua kuwa ilikuwa rotten deal. Halafu tutaanza kutafuta kisingizio hiki na kile.

Wanasiasa? Wako katika mchezo wao as usual. Wapo watakaoanguka kwa hili na wapo watakao inuka kidedea. Hata hivyo ukweli mmoja unabaki. THIS COUNTRY IS STILL STINKING WITH CORRUPTION, GRAND CORRUPTION, NOT PETTY ONES.
 


Lipumba tena? Mungu wangu , hivi hawa wapinzani wamelogwa? Hivi huo ndio msimamo wake binafsi au wa chama?

Kwa mtindo huu bora hata ROSTAM+CCM kuliko upuuzi wa hawa upinzani. Mbona ameamua kukimaliza chama chake tena? Asijeakawa amenaswa na harufu ya UDINI huyu, wenyewe wanasema " UDUGU WA KIISILAMU".

Samahani kama nimetoka kwenye mada lakini nimeboreka vya kutosha? Lipumba anatetea DOWANS? au sijauelewa?
 
Kwani hiyo kesho bado tu,mbona siambiwi kilichojiri huko?
 
Asijeakawa amenaswa na harufu ya UDINI huyu, wenyewe wanasema " UDUGU WA KIISILAMU".

Wewe KGM ni ama KAFIRI au FAKIRI wa kufikiri. Acha upumbavu wako! Huna cha kusema mpaka uutaje uislam. Uliutaja kule kwenye mada yako ya Kigoma naona umeiona ndio agenda. Kwani lazima kila topic uchangie hata kama huna points. Acha ulimbukeni!

NN.
 
Wakati wakijitetea, Rostam na Lowassa, walijua kuhusu kampuni ya Mwakyembe kwa kuwa na wao walianzisha ya kwao kushindana nayo kule Singida, lakini hawakusema. Sababu ya kuwafanya wasiseme wakati ule pale bungeni ni kwa kuwa walijua na wao wana interest na kwamba haikuwa na madhara yoyote. Walikubali yaishe, Lowassa akaachia ngazi. Sasa wameamua 'kumwaga mboga' baada ya kuona mpango wao umekwama, mpango ambao walikuwa nao muda mrefu wa kwamba baada ya mkataba Tanesco wauziwe mitambo.

Kwa kweli Vodacom connection bado inafanya kazi na tutaona, Makamu Mwenyekiti wa CCM (alikuwa Vodacom), Dk. Rashid (alikuwa Vodacom), Ngeleja (alikuwa Vodacom), Lowassa (Dealer mkubwa, Alphatel), Peter Noni (Vodacom/EPA), Rostam (Vodacom/Kagoda?/Dowans) sasa tunategemea nini? Watanzania WATALIA SANA.

Hebu angalieni, PPRA walikwisha kuona hata kabla kwamba jamaa wana mpango wa kununua Dowans. Na jambo la kusikitisha, hebu jiulizeni, ni kwanini Serikali ikasitisha mkataba na Dowans muda mfupi kabla ya mkataba kwisha? kama kweli waliipenda mitambo ya Dowans, kwanini wasisubiri miezi iliyobakia waepuke kudaiwa fidia? Ama fidia ni sehemu ya kifuta jasho cha wazee? Jamani huu ni usanii toka mwanzo hadi mwisho na tutaona mengi na wengi wataingia humo. TUTAKE TUSITAKE

Source: ThisDay
 
Mwenyezi Mungu, mwingi wa Rehema na atende muujiza ili wote wasiolitakia taifa letu mema waumbuke vibaya na wafe vifo vya ajabu.

Amen
 

Hiyo ndiyo tabeyi (sp) hiyo. Inaliua kabisa taifa hili
 
hIVI KUNA MIKATABA INASAINIWA .........YA MIAKA 20????????????????????? MY GOD - YAANI WANAWASAINIA HATA VIZAZI VIJAVYO???? ITS VERY UNFAIR - WABADILI SHERIA MIKATABA ISIZIDI 5 YEARS - OTHERWISE KIZAZI KIJACHO KITAPATA SHIDA SANA KWA AJILI YA TAMAA YA WATU WACHACHE - GOD SAVE OUR NATION - AMEN
 
Wewe KGM ni ama KAFIRI au FAKIRI wa kufikiri. Acha upumbavu wako! Huna cha kusema mpaka uutaje uislam. Uliutaja kule kwenye mada yako ya Kigoma naona umeiona ndio agenda. Kwani lazima kila topic uchangie hata kama huna points. Acha ulimbukeni!

NN.

Samahani, tena samani kwa utoka nje ya mada,
ila nauliza nini hasa kinamsukuma huyu profesa kufumbia uozo wa richmond na Downs. Mimi kama mpenda mageuzi ananikatisha tamaa.
 
hivi huo mkutano haujaisha? tunaomba update
 
Tumeandika kwa karibu miezi miwili.. Dowans itanunuliwa tu! Ni jukumu letu kuwapinga. Huwezi kununua mali ya mtu aliyekuibia. Kwanini hawataki kuzungumzia Dowans ni nani hasa na waliingiaje nchini. Kama kweli serikali inataka, itaifishe mitamnbo hiyo
 
Tumeandika kwa karibu miezi miwili.. Dowans itanunuliwa tu! Ni jukumu letu kuwapinga. Huwezi kununua mali ya mtu aliyekuibia. Kwanini hawataki kuzungumzia Dowans ni nani hasa na waliingiaje nchini. Kama kweli serikali inataka, itaifishe mitamnbo hiyo

Lakini kwa kweli naona kuna vitu vingi behind the move, ndio maana mpaka nikaingiza na udini ndani, kwa sababu napata matatizo sana katika kufikiri kwangu.

Swala la kutaifishwa halizungumuziki, wanazungumzia kununua tu. How? ununua toka kwa nani?

Hebu angalia issue ya Mwakyembe, hivi kwa nini hatujiulizi nini chanzo cha kamati ya mwakyembe kuundwa. Hivi yasingekuwa madudu hayo waliyoyafanya Richmond, ile kamati ya mwakyembe ingeundwa? Lakini watetezi wa MAFISADI hawakosi jibu, watakwambia Dr ndie aliyechagiza kamati iundwe.

Sasa unapoona mtu kama LIPUMBA,zitto Mr DOWN ambao wapenda mageuzi walikuwa wamewekeza mitaji yao kwao!!!!!!!!!!, wanabwabwaja kama wana homa kali, maswali yanakuwa mengi ndugu zanguni.

Just imagine lipumba anaitisha mkutanao na WAHARIRI kwa sababu tu FISADI la KUPINDUKIA ROSTAMU KAGUSWA, KWA NINI, TENA ANAUNGA MONO UNUNUZI WA HIYO MITAMBO ILIYOKWISHA OZA, KAMA SIYO MAJITAKA NINI?
 
Ajabu na kweli, wataalamu wa Tanesco wamesema wameshasema mitambo isinunuliwe. Na tayari kampuni moja ya hapa bongo iko katika hatua za mwisho za kuinunua. Si ajabu ikawa ni ile ile ambayo tuna mkataba nayo wa kununua umeme. Hii ni HATARI sana, na watatuambia;

"SI MUNAONA, SASA TUNAUZIWA UMEME KUTOKA KATIKA MITAMBO ILE ILE AMBAYO MULIKATAA TUSIINUNUE. TULIWAAMBIA NI MIZURI"
 
Tanzania hakuna UPINZANI wa KWELI.Period!
 
Wakati Chadema haijatoa msimamo kuhusu Dowans, Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba anasema; Kama chama wanaunga msimamo wa Zitto, kwamba mitambo ya Dowans inunuliwe. Wanatoa mifano ya vitu mitumba kama ndege za ATC ni mitumba, mabehewa ya TRC ni mitumba. Wanasema kwamba sababu sheria ni mbovu. Anasema malumbano yanayoendelea hayana tija yanaenda kwa watu binafsi, na kwamba Zitto yuko sahihi kabisa. Zitto hakuwapo.
 

halisi haya ya kutolea mifano ya ATLC na TRC wanataka kuhalalisha uozo tu;

Hakuna cha mitambo mibovu au kuukuu.. kama ni kutaka kunununua kuukuu mbona tunaweza kununua hata nje tena kwa bei ya chini zaidi? Hapa suala ni kutaka Dowans walipwe kwa sababu ya ahadi yao waliyowapa miaka miwili iliyopiota iliyowafanya wakurupuke walete majenereta hayo na kudandia mkataba wa Richmond. That is it!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…