Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, William Shellukindo alisema asingependa kuona malumbano yanayoendelea baina ya wabunge hao yanaihusisha kamati ya Bunge ya Nishati na Madini.
"Tukianza kuhoji kwa nini Dk Mwakyembe ana endelea kuwa kwenye kamati yangu, kama Makamu Mwenyekiti wakati ana hisa katika kampuni hiyo, itabidi tupitie kamati zote na kuwaondoa wafanyabiashara wote," alisema Shellukindo na kuongeza:
"Kuna baadhi ya wafanyabiashara wakubwa ambao ni wajumbe katika kamati ya Viwanda na Biashara, lakini sisi hatuwasemi hata kidogo" aliongeza Shullukindo.
Aliwataja baadhi ya wafanyabiashara hao kuwa ni pamoja na Joseph Mungai, Nazir Karamagi, Rostam Azizi na Basil Mramba.
"Kama wataamua kuwa Mwakyembe atoke katika kamati hiyo, basi wengine pia waondoke kwa sababu huwa wanashiriki kutoa maamuzi mazito, yanayohusu wafanyabiashara wakati na wao ni wafanyabiashara," alifafanua Shellukindo.
Source: Mwananchi.