Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Baadhi ya Wadau wengine wanaotarajiwa kushiriki ni Viongozi wa Dini, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Msemaji wa Serikali, Gerson Msigwa, Mkuu wa Mkoa wa Dar – Albert Chalamila.
Wengine ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Palamagamba John Aidan Kabudi, Egbert Mkoko (SJMC), Mhandishi Andrew Kisaka (TCRA), Kenneth Simbaya (UTPC), CCP David Misime (Msemaji wa Jeshi la Polisi), Wakili Patrick Kipangula (DG JAB), Humphrey Mtui (PDPC) na Waandishi wa Habari.
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Wakili Albert Msando:
Akizungumza kwa niamba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar, Albert Chalamila, Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Wakili Albert Msando amesema:
“Serikali ngazi ya Mkoa na Wilaya tutaendelea kutoa Ushirikiano kwenye Sekta ya Habari kuhakikisha majukumu yao yanafanyika bila mkwamo, wapate taarifa sahihi kwa kuwa tunatambua Taarifa Sahihi ndizo ambazo Wananchi wanastahili kupata.”
Msemaji wa Serikali, Gerson Msigwa:
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa anasema sasa Waandishi wa Habari wanafanya kazi Kidigitali chini ya Bodi ya Ithibati ambayo imekuwa ikisimamia zoezi la kujisajili kupitia Mfumo wa bodi hiyo.
Waziri Prof. Kabudi: Vyombo vya Habari vimewekewa mazingira ya kufanya kazi kwa uhuru
Wakati akimkaribisha Mgeni rasmi, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Palamagamba John Aidan Kabudi ametoa hotuba kwa kueleza”
Amesema “Takribani Miaka minne ya Uongozi wa Rais Samia Suluhu, Vyombo vya Habari vimeshamiri na kuwekewa mazingira mazuri ya kufanya kazi zao kwa uhuru na kwa kuangalia mustakabari wa Nchi yetu.”
Mhadhiri wa Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano kwa Umma (SJMC), Abdallah katunzi akitoa wasilisho kuhusu matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii na teknolojia ya akili Unde (AI) kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025. Wasilisho hilo amelitoa leo Julai 9, 2025 katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. wakati wa Mkutano wa Wadau wa Kujadili Mchango wa Sekta ya Habari katika Kufanikisha Uchaguzi Mkuu 2025.
Prof. Kabudi: Bodi imesajili waandishi wa Habari 2,900
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Palamagamba John Aidan Kabudi amesema mpaka sasa Bodi ya Ithibati imefanikiwa kusajili Waandishi wa Habari 2,900 katika Mfumo wa Kidigitali wa TAI -Habari ambao unachakata taarifa na kumpatia Mwanahabari.
Ikumbukwe, Julai 4, 2025, Bodi hiyo iliagiza kuwa Waandishi wote wanaoendelea kufanya kazi kwenye Vyombo vya Habari vya uchapisho na kielektroniki bila kusajiliwa na Bodi hiyo wanatakiwa kuacha mara moja shughuli zao hadi pale watakapokamilisha usajili kupitia mfumo wa TAI HABARI.
Ilieleza kuwa kufanyakazi bila kujisajili ni kuvunja Kifungu cha 19 cha Sheria ya Huduma za Habari, kinachokataza mtu yeyote kufanya kazi za kihabari bila kibali rasmi.
Meneja wa Huduma za Utangazaji kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mhandisi Andrew Kisaka akifanya wasilisho kuhusu kuripoti migogoro na maafa kipindi cha uchaguzi. Ametoa wasilisho hilo wakati wa Mkutano wa Wadau wa Kujadili Mchango wa Sekta ya Habari katika Kufanikisha Uchaguzi Mkuu 2025, ambao umefanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, leo Julai 9, 2025.
Msemaji wa Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) David Misime akitoa wasilisho kwa wadau wa Sekta ya Habari kuhusu wajibu wa Waandishi wa Habari na Jeshi la Polisi katika kulinda usalama wakati wa uchaguzi. Ametoa wasilisho hilo wakati wa Mkutano wa Wadau hao Kujadili Mchango wa Sekta ya Habari katika Kufanikisha Uchaguzi Mkuu 2025 ambao umefanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam leo Julai 9, 2025.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko
Kutofautiana kimaoni sio uhalifu, Mtu kuiwaza kinyume na wewe sio dhambi, dhambi ni vile kuamini kile unachoamini wewe ndio sahihi na kwamba kila mtu anatakiwa kuamini kama unavyoamini wewe.
Takwimu za Vyombo vya Habari Tanzania
Magazeti 375
Vituo vya Redio 247
Vyombo vya Habari Mtandaoni 355
Blogs 72
Vituo vya Runinga (TV 68)
Chanzo: Wizara ya Habari
Biteko: Kila Mtu apate haki ya kusikilizwa hata kama jambo hulipendi, tuvumiliane
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko ametoa wito wa Wadau wa Sekta ya Habari na wengine kuwa kuelekea wakati wa Uchaguzi Mkuu kuwe na kuvumiliana na kukubali kuwapa nafasi Watu kutoa mawazo yao.
Amesema hayo wakati wa Mkutano wa Wadau kujadili mchango wa Sekta ya Habari katika kufanikisha Uchaguzi Mkuu wa 2025, ambapo pia amepata nafasi ya kuzindua Mfumo wa Vitambulisho kwa Waanahabari katika mfumo wa Kitigitali kupitia TAI-Habari, leo Julai 9, 2025.