Mkutano wa wanahisa wa NICOL - 26, Januari 2013

Mkutano wa wanahisa wa NICOL - 26, Januari 2013

Edo

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2008
Posts
727
Reaction score
93
NATIONAL INVESTMENTS COMPANY LTD (NICOL)

THE NICOL SHAREHOLDERS MEETING IS PROPER AND LEGAL.

1. Page 5 of "The Guardian" and page 3 of NIPASHE, both dated 22[SUP]nd[/SUP] January 2013 carry statements allegedly issued by Mr. Mosha, a self styled Chairman of NICOL, that the planned Annual General Meeting of NICOL scheduled for Saturday 26[SUP]th[/SUP] January 2013 was illegal and the shareholders have been urged not to attend this meeting.

The attention of the general public is hereby directed to the fact that Mr.
Mosha ceased to be the Chairman of NICOL since 14[SUP]th[/SUP] April 2012, when the shareholders of NICOL appointed a new Board which now officially recognized; Dr. G. H. Kaunda is the current Chairman of NICOL. It is advised that the concerned should first carry out a check with BRELA to establish the proper officers of the company before declaring the illegality, or otherwise, of the planned meeting.

2. If the planned shareholders' meeting is illegal, the correct and productive step for Mr. Mosha would have been to take up the matter with the appropriate proper authority for a redress of the alleged forgery and other imagined illegalities, instead of complaining to the media, as has been done.
Furthermore, Mr. Mosha is not qualified to, and cannot be the determinant of illegality, or otherwise, of a NICOL meeting merely on the basis of there being an appeal in the Court of Appeal. There is not restraining order against the Orders issued by Hon. Lady Justice Bukuku. After all, the existence of an appeal in the Court of Appeal cannot be a barrier in the execution of existing valid Orders of the Court.

3. The 26[SUP]th[/SUP] January 2013 meeting is LEGAL being convened in accordance with the earlier decision made by the shareholders in their extraordinary meeting held on 14[SUP]th[/SUP] April 2012. The planned meeting therefore is very much in accordance with the relevant laws and NICOL shareholders' express wishes.
THE SHAREHOLDERS ARE URGED TO ATTEND THIS MEETING.

4. Where does Mr. Mosha get the temerity to assure the stakeholders with such a certainty that "they should not worry about their shares as from 2005 to 2012 the company shares have increased from 8.6bn/= to 40bn/=" when:
i. The NICOL shares are no longer being traded following its suspension from the Dar es Salaam Stock Exchange since 2011, and that NICOL was under the threat of being delisted were it not for the timely action of some of the shareholders;
ii. The last time Mr. Mosha published Audited Financial Statements was in 2010 for the 2008 Audited Financial Statements. Furthermore, he refused to sign the 2009 Audited Financial Statements; the company had by that time accumulated huge losses totaling T.Shs 9.8bn/=. This being the prevailing situation, what would be the basis Mr Mosha's assurance to the shareholders? After all, "mali bila daftari hupotea bila habari".
iii. In any case, if the position was so rosy, why are the shareholders complaining about not receiving commensurate returns on their investments to date?

The frantic efforts being made by the former Chairman of NICOL to stop the planned shareholders meeting from taking place is an indication of the fact that he does not wish the shareholders to emerge from the dark with respect to NICOL's true financial performance.


NICOL SHAREHOLDERS ARE THEREFORE URGED TO ATTEND THE SATURDAY 26[SUP]TH[/SUP] JANUARY 2013 MEETING SO THAT THEY MAY RECEIVE AN AUTHENTIC AND FACTUAL UPDATE ON THE NICOL'S OVER ALL PERFORMANCE AND PARTICIPATE IN DETERMINING THE WAY FORWARD FOR NICOL.
INTERIM MANAGER – NICOL 22[SUP]ND[/SUP] January 2013
 
Katika mkutano ambao si halali kwa mujibu wa Felix Mosha jana alivyotangazia umma, leo mkutano wa wanahisa umefanyika akiwemo mzee Bomani na Mengi na kuamua kumtimua uongozi Mzee Mosha aliyekaa katika uwenyekiti kwa miaka 10 huku aking'ang'ania kuendelea uongozi NICOL bila ya tija. Mzee Idd Simba sijui yupo ktk kundi gani.

Ikumbukwe kuwa hawa wazee walikua pamoja katika kuchangisha pesa za NICOL.

Source: ITV
 
Hapo kuna tatizo. Inakuwaje mzee Felix Mosha aogope kikao cha wanahisa na kukibatilisha?
 
Hawa jamaa wanajuana, walifanya uwekezaji kwenye viwanda vinavyotia shaka ( Kiwanda cha Madawa na Kiwanda cha Minofu ya Samaki) na baada ya kukamilisha hilo aliyekuwa mwenyekiti wa bodi ya uwekezaji -Mengi alijiondoa kwenye bodi..
Wanatumia umaarufu wao kuwadhulumu wawekezaji wadogo maskini.. Serikali kupitia Mamlaka ya Soko la Mitaji na Dhamana (CMSA) iliwahi kuwachachafya NICOL ijapokuwa lengo ilikuwa kuwaonya wawekezaji wa NICOL kijanja juu ya hii kampuni...
 
Hiyo NICOL Inashangaza ilichukua kiwanda cha dawa kilichokuwa Active , Soon walipokinunua kikafa kifo cha Mende ! Bila shaka Kuna mchezo ulichezwa , Hawa wazee lazima wachunguzwe ( na hasa uchunguzi huru ) , maana hawa ndiyo wachangiaji wakubwa wa MAGAMBA , hawa akina Manumba hawawezi kutupa Majibu sahihi .
 
haya kama ni mabadiliko yenye kuleta tija ntashukuru maana hata mimi ni mhanga sijawahi kuonja hata senti 1,
 
January 27, 201Dar-es-Salaam, Tanzania

Wanahisa wa Kampuni ya Uwekezaji ya Taifa (NICOL) wameunda jopo la wazee sita kwa ajili ya kumshawishi aliyekuwa Mwenyekiti wa kampuni hiyo Felix Mosha kutii uamuzi wa wanahisa hao wa kumuondoa madarakani.

Akitoa mazimio ya Mkutano Mkuu wa kampuni hiyo uliofanyika jana jijini Dar es salaam. Meneja wa Kampuni hiyo Wanoni Wamuza alisema jopo la wazee hao ambao ni waasisi wa NICOL watakuwa na jukumu la kumshawishi Mosha kuachia nafasi hiyo na kuruhusu uongozi mpya kutumia ofisi za kampuni.

Walioteuliwa kufanya kazi hiyo ni Jaji Mark Bomani, Dk. Reginald Mengi, Balozi Paul Rupia, Balozi Anthony Nyaki, Arnold Kileo na mzee Hance Kitine.

Wamuza alisema kazi hiyo itafanyika ndani ya mwezi mmoja na endapo hakutatokea makubaliano kampuni itachukua hatua za kisheria kwa ajili manufaa ya wananchi wanaoimiliki.

Uamuzi wa kumuondoa Mosha madarakani ulifanywa na wanahisa katika mkutano uliofanyika mwaka jana baada ya kutoridhishwa na uendeshaji wa kampuni uliokuwa chini yake na kusababisha hasara ya kiwekezaji inayofikia Shilingi Bilioni 10.

"Wazee na waasisi wetu watakwenda kuongea naye na kumshauri aondoke na kuziacha ofisi wazi ili tuendelee na nia yetu nzuri ya kuendeleza Kampuni kwa ajili ya wanahisa wote," alisema

Awali Katika michango iliyotolewa na mzee Kileo, Jaji Bomani na Dk. Mengi walitaka kuitishwa kwa jopo la watu maalum kwa ajili ya kushauriana na Mosha ili ipatikane suluhu kabla ya kwenda mbali zaidi.

Katika mazimio mengine wanahisa hao waliamua kumpa onyo kali Mosha kwa tabia yake ya kuingilia maamuzi ya wanahisa ambao ndio wamiliki wa kampuni hiyo.

Wamuza alieleza wanahisa pia wameagiza kesi zilizokuwa Mahakamani ambazo hazina tija kwa Kampuni zifutwe.

Aidha taasisi zinazoendelea kushirikiana na mwenyekiti huyo wa zamani zimeomba kusitishwa haraka kwa sababu uongozi huo umeondolewa kwa mujibu wa sheria ya uanzishwaji wa mifuko ya uwezeshaji.

Wakati akifungua mkutano huo Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya NICOL, Dk. Gidion Kaunda alisema uongozi wao mara ulipoingia madarakani umefanya kazi kubwa ya kuweka kampuni katika utaratibu wa kutambulika baada ya Wakala wa Usajili wa Makampuni (Brela) kutokuwa na orodha ya viongozi kwa kipindi kirefu.

Alisema katika kipindi hicho wamefanikiwa kupata barua ya kutambuliwa kwenye taasisi hiyo pamoja na kufuatilia baadhi ya vitabu vya mahesabu ya matumizi.


Source: Home

Hali halisi ilivyokuwa katika mkutano mkuu wa wanahisa- video:

Nicol yakanusha tuhuma dhidi ya Dk. Reginald Mengi



Source: ITV TANZANIA youtube
 
Last edited by a moderator:
Hawa jamaa wanajuana, walifanya uwekezaji kwenye viwanda vinavyotia shaka ( Kiwanda cha Madawa na Kiwanda cha Minofu ya Samaki) na baada ya kukamilisha hilo aliyekuwa mwenyekiti wa bodi ya uwekezaji -Mengi alijiondoa kwenye bodi..
Wanatumia umaarufu wao kuwadhulumu wawekezaji wadogo maskini.. Serikali kupitia Mamlaka ya Soko la Mitaji na Dhamana (CMSA) iliwahi kuwachachafya NICOL ijapokuwa lengo ilikuwa kuwaonya wawekezaji wa NICOL kijanja juu ya hii kampuni...

Nothing could be further than the TRUTH you have expoused above. Walipita nchi nzima wakiwahamasisha watanzania kwa sauti za decibel kubwa kwamba wawekeze kwenye hiyo kampuni, baada ya kukusanya fedha za maskini wakaanza kuwatapeli kwa kununua viwanda na mashirika ambayo walijua fika hata kabla kwamba yamefilisika au yamekufa. Baada ya kuona hayo yametimia basi wakaanza eti "kujitoa" kwenye uongozi. Kwangu mimi dhamira ya dhati ya kujitoa ingeaminika kama ingeambatana na kurudisha hela za wanahisa kitu ambacho hakijafanyika hadi leo. Kuna story imetoka kwenye gazeti last week ya Benki Moja kutaka kunadi nyumba ya mmoja wa viongozi hao hao wa NICOL na imebidi akimbiie Mahakamani kusitisha mpango huo. Hii inaonyesha kuwa NICOL inaongozwa na serial conmen.
 
Back
Top Bottom