Mkuu Mzizi mkavu,dawa ya mwarobaini ninywe kiasi gani

Mkuu Mzizi mkavu,dawa ya mwarobaini ninywe kiasi gani

Marire

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2012
Posts
12,333
Reaction score
5,292
husika na mada hapo juu dawa za dukani hazinitibu tena sasa hivi nimebandika mwarobaini ila sijui ninywe kiasi gani niweze kupona malaria,msaada wenu pls
 
Bibie.@Marire tumia njia hii hapa chukuwa Mwarubaini kipimo cha mkono wako gao moja tianbdani ya sufuria tia maji glasi 2 chemsha kwa daikika 10 opowa chuja kisha unakunywa Glasi 1 ya Maji ya Mwarubaini Asubuhi kabla ya kunywa kitu na usiku fanya hivyo kwa muda wa siku 7 kisha nenda kapime hiyo Malaria yako utakuta imekwisha ondoka mwilini mwako. La kama bado itakuwepo njoo tena hapa nitakupa dawa ya kuondosha kabisa hiyo Malaria sugu yako tumia uje unipe feedback.
 
Mwarubaini Mmea Mjarabu Kutibu Maradhi Mbalimbali

MWARUBAINI.jpg
Benefits-of-Neem.jpg



KATIKA karne hii ya sayansi na teknolojia, Mwenyezi Mungu amewajaalia baadhi ya wanadamu (Madaktari) kuwapa taaluma (elimu) ya kufahamu maradhi yanayosumbuwa wanaadamu wenzao kwa kutumia vifaa mbalimbali ikiwemo vya kisasa na dawa katika kuwatibu.
Hata hivyo uwezo wa aina hii ulikuwepo hata kabla ya kuja sayansi na teknolojia ambapo binadamu wa awali alitumia tiba za asili kwa kujitibu na maradhi ya aina mbalimbali.

Hivi sasa toka kuwepo sayansi na teknolojia, asilimia kubwa ya watu wanadharau kutumia dawa za asili na badala yake wameelemea sana katika matibabu ya dawa za kemikali.


Kwa mtazamo, takribani miti yote iliyopo duniani ni dawa hivyo ni vizuri kwa jamii kuelimishwa ili kuweza kujuwa ni jinsi gani wataweza kuitumia miti hiyo kwa kuitibu miili yao.

Kutokana na hali hiyo na matibabu hayo, inaonekana wazi kuwa mti wa Muarubaini ama wengine huita Mtunda, ni mjarabu kwakutibu maradhi mbalimbali na hivyo upo umuhimu wa kila mtu kuupanda katika makaazi yake na pia kwa kupitia Wizara ya kilimo kutenga eneo maalum kwa ajili ya kupanda miti ya aina hii.
Mti wa Mwarubaini ambao kwa kiingereza unajulikana kama (Neem) ulianza kugunduliwa kama tiba ya maradhi zaidi ya miaka 4.000 iliyopita.

Mti huu hutibu maradhi ya aina mbalimbali kwa kuanzia mizizi, magome, mbegu na majani yake.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa baraza la tiba asilia Zanzibar Mayasa Salum Ali, alisema mti wa Mwarubaini unapatikana au unaota zaidi katika nchi za joto kote Ulimwenguni.

Mwenyekiti huyo ambae pia ni mtaalam wa fani hiyo alisema kwa upande wa watu wa India, kwao mti huu unasifa sana katika matibabu yao na unajulikana kama duka la dawa la kijiji.
Aidha alifahamisha kuwa wanauthamini kama dawa kutokana na matibabu yake kwani unatibu maradhi ya aina mbalimbali ambayo humuandama mwanadamu na hata wanyama na mimea ya shambani.

Hata hivyo kwa upande wa wataalamu wa India kutokana na umuhimu wa dawa hizi za asili, wamefakiwa kutengeneza bidhaa mbalimbali kupitia mti huu ili kurahisisha matumizi ya watu kwa kupitia tiba ya mwarubaini.

Bidhaa hizo ni pamoja na dawa za kumeza, dawa za mswaki, sabuni, vipodozi vya aina mbalimbali kama vile krimu, mafuta ya kujipaka lotion majani ya chai na vitu vingine vingi.
China nayo haipo nyuma katika kutumia dawa za mti huu kwani nao wameweza kutengeneza bidhaa za aina mbalimbali ili kurahisisha matumizi.

Kwa upande wa Zanzibar, sehemu ndogo sana ambayo inatumia mti huu kama ni dawa ya malaria na sehemu hiyo ni kwa wale watu wazima wanaoishi vijijini. Wao kidogo wanatumia mti huu kama ni dawa ya kutibu malaria sugu huku ikiwa mti wa Mwarubaini unatibu maradhi ya aina mbalimbali.

Watu wengi husikia wakisema kuwa Mwarubaini ni dawa ambayo inatibu maradhi arobaini (40) kumbe sivyo ilivyo kwani mti huu unatibu zaidi ya maradhi arubaini lakini tu jamii haijui na haina utaalam wa kufahamu kwa maradhi mengi yanayotibiwa kwa kutumia mti huo.

Hivyo upo umuhimu kwa upande wa wataalamu wa tiba asilia kutoa elimu hiyo kwa jamii ili kuweza kujuwa kutumia mti huo ili kuweza kuondokana na maradhi ya aina mbalimbali.

Kutokana na ufahamu huo mdogo kwa Wazanzibari katika tiba zinazopatikana kutokana na Mwarubaini, wengi wanapoumwa na maradhi ya aina mbalimbali na hata malaria hukimbilia hospitali kupata dawa za vidonge au sindano vitu ambavyo hutokana na mchanganyiko wa kemikali mbalimbali ambazo zinauwezo wa kusababisha madhara makubwa kwa mwili wa mwanadamu.

Miongoni mwa dawa ambazo zina madhara yanayoweza kumpata mwanadamu ambayo husababisha na vidonge au sindano hizo ni pamoja na Fansida au Chloroquine ambapo utafiti unaonesha kuwa baadhi ya wagonjwa waliotumia dawa hizo wameathirika aidha kwa kuwashwa na mwili na wengine wameathirika na macho kwa kutumia Fansida.
Ili kuondokana na athari kama hizo, Mwenyekiti huyo amewashauri Wazanzibari na Watanzania kwa ujumla kutumia dawa za asili ili kuondokana na matatizo kama hayo.

Hata hivyo Mwenyekiti huyo alifahamisha kuwa katika baadhi ya maradhi badala ya kutumia pesa nyingi kwa kununua dawa za kemikali ambazo bei zake zinapanda siku hadi siku ukilinganisha na dawa za asili ambazo bei zake ni nafuu.
Hata hivyo aliwashauri wagonjwa kufuata ushauri wa kitaalamu kabla ya kutumia dawa hizo ili kuzidi kuboresha afya na kujiepusha na matatizo yasiyo ya lazima.

Majani ya mti wa Mwarubaini yanatumika kwa kutibu maradhi mbalimbali kama vile homa za watoto, suruwa na kwa upande wa watu wazima hutibu malaria, muwasho, maradhi ya moyo, Ukimwi, mkanda wa jeshi na maradhi ya buba.
Mengne ni maradhi ya ganzi ya mwili, kisukari na mtu ambae anaupungufu wa kinga mwilini, mapele sugu yalioshindikana kutibika hospitali na maradhi mengine.

Dk. Mayasa pia alifahamisha majani hayo yanauwezo wa kuuwa hata kwa upande wa wadudu wa shambani ambao wanakula mazao.

Mbegu za Mwarubaini zinatengenezwa mafuta ambayo mafuta hayo yanajulikana kwa jina la (Neem oil) ambayo yanauwezo wa kutibu maradhi ya aina mbalimbali kama vile kuondoa chunusi, mapele, fangasi na mabaka mwilini.
Pia mafuta hayo huuwa wadudu mbalimbali ambao wanatambaa na kuruka nyumbani na hata vijidudu (bacteria), sisimizi na wadudu wengine.

Mizizi na magome ya mwarubaini huuwa wadudu wa aina mbalimbali kama vile funza, maradhi ambayo huwapata wanawake kama vile vikanga na maradhi mengine mengi ambayo ni maradhi sugu na yameshindwa kutibiwa basi Mwarubaini huyatibu.

Kwani hata wanyama tunaofuga nyumbani mfano ngombe na wengine ambao hugandwa na kupe na wadudu wengine, mnyama huyo ukimkogeshea maji hayo uliosaga magome ya mti huo huondoa wadudu wote, alifahamisha dk. Mayasa.

Mtaalamu huyo alifahamisha kuwa dawa za mti huo hazina madhara kama zilivyo dawa nyengine za kemikali lakini kwa ushauri unatakiwa kumuona daktari mwanzo alio karibu nawe kabla ya kuanza kutumia.
Alifahamisha kuwa dawa za kemikali zinatibu haraka kuliko dawa za asili lakini dawa za asili ni bora zaidi kuliko dawa za kemikali kwani zinatibu kidogo kidogo na zikitibu zimetibu na hazina maradhi yanayosababishwa na dawa hizo.
 
jana usiku nimekunywa glass moja na sasa hivi nimesha kunywa moja,nilivyokuwa nanijisikia jana leo nina afadhali sana,ngoja niedelee na dozi nitaleta majibu next week
 
Tatizo la kutibu malaria ni kuwa vijidudu vinakuwa attached kati ya chembe nyekundu za damu. Katika kutibu dawa inachangia kuharibu chembe hizo. Kunywa mwarobaini bila dozi kamili ni hatari sana inaweza kuleta upungufu wa damu.

Natamani tungeestablish dosage. Kg ngapi za mwarobaini, maji kiasi gani na yawe reduced kwa kiasi gani.
 
Tatizo la kutibu malaria ni kuwa vijidudu vinakuwa attached kati ya chembe nyekundu za damu. Katika kutibu dawa inachangia kuharibu chembe hizo. Kunywa mwarobaini bila dozi kamili ni hatari sana inaweza kuleta upungufu wa damu.

Natamani tungeestablish dosage. Kg ngapi za mwarobaini, maji kiasi gani na yawe reduced kwa kiasi gani.
Mkuu King'asti Kwani yeye Mkuu.@Marire atakunywa Tani nzima ya Muarubaini? nimesha muambia achukuwe majani kiasi cha kuweza kuchemsha Glasi 2 achemshe kwa dakika 10 anywe kabla ya kula kitu asubuhi na usiku kwa muda wa siku 7 kisha aende kupima Malaria bibie King'asti upo pamoja na mimi?
 
Last edited by a moderator:
jana usiku nimekunywa glass moja na sasa hivi nimesha kunywa moja,nilivyokuwa nanijisikia jana leo nina afadhali sana,ngoja niedelee na dozi nitaleta majibu next week
endelea mkuu..yaonekana itakusaidia...usikate tamaa....
 
mzizi mkavu toka jumamosi nimetumia hiyo dawa ila naona kama imetuluza malaria tu kupona naona bado.toa muongozo nifanyeje??
 
Mkuu King'asti Kwani yeye Mkuu.@Marire atakunywa Tani nzima ya Muarubaini? nimesha muambia achukuwe majani kiasi cha kuweza kuchemsha Glasi moja anywe kabla ya kula kitu asubuhi na usiku kwa muda wa siku 7 kisha aende kupima Malaria bibie King'asti upo pamoja na mimi?
Sasa Mkuu MziziMkavu hiyo glasi moja ya moja inapaswa kuchemshwa na majani kiasi gani?

Kwasababu ukisema tu glasi moja yupo atakayechemsha majani mengi na mwingine atachemsha kidogo.

Ni vizuri ukatuambia glasi moja ya maji yanahitaji majani kiasi gani.

Pia magome na matunda yake yanatumikaje yaani kwa dozi?

Shukran sana.
 
Sasa Mkuu MziziMkavu hiyo glasi moja ya moja inapaswa kuchemshwa na majani kiasi gani?

Kwasababu ukisema tu glasi moja yupo atakayechemsha majani mengi na mwingine atachemsha kidogo.

Ni vizuri ukatuambia glasi moja ya maji yanahitaji majani kiasi gani.

Pia magome na matunda yake yanatumikaje yaani kwa dozi?

Shukran sana.
Majani kipimo cha kiganja cha mkono wako majani ya mwarubaini yanatosha.Tia ndani ya chombo chenye maji glasi 2 chemsha hayo majani ya Mwarubaini kwa dakika 10 kisha chuja unywe fanya hivyo ukiweza japo mara 2 au mara 3 kwa siku tumia siku 7 au inategemea maradhi yako kama ni makubwa tumia siku 14 au siku 21 utapona. kila unapo taka kutumia dawa chukuwa dawa mpya uchemshe.
 
Majani kipimo cha kiganja cha mkono wako majani ya mwarubaini yanatosha.Tia ndani ya chombo chenye maji glasi 2 chemsha hayo majani ya Mwarubaini kwa dakika 10 kisha chuja unywe fanya hivyo ukiweza japo mara 2 au mara 3 kwa siku tumia siku 7 au inategemea maradhi yako kama ni makubwa tumia siku 14 au siku 21 utapona. kila unapo taka kutumia dawa chukuwa dawa mpya uchemshe.
Shukran sana
 
Back
Top Bottom