Mkuu wa chuo cha SAUT Mwanza ajiuzulu

Status
Not open for further replies.

shigegele

JF-Expert Member
Joined
Mar 13, 2014
Posts
211
Reaction score
25
katika hali ya kushangaza mkuu wa chuo cha saut mwanza ameachia cheo hicho baada ya kuona wanafunzi nane wamefukuzwa chuo bila utaratibu wowote,sababu nyingine ni kuwatoza wanafunzi penalty ya laki moja wachelewapo kulipa ada ameuliza hyo penalty inaenda wap na kwanini wanafunzi wapigwe penalty,source mimi mwenyewe lecturer naitwa slaa


 
Chadema lazima warudie asili yao kuwa chama cha kuweka na kukopa cha jamii yamkule kwao.
 
Ila hili swala la penalty, si la kiungwana, huwezi mpiga mtu penalty, ya kiasi kikubwa hicho ukizingatia chuo kipo chini ya dini, na ada yake kubwa, na kwa upande wa pili, asilimia kubwa ya wanafunzi hawana government sponsorship.
 
Kwenye Suala la Penalt hiyo ya Laki moja ni kukosa utu, yaani ni adhabu kwa Maskini walioshindwa kulipa ada kwa wakati. Mtu kashindwa kulipa Principal on Time una Top up na Penalt!
 
Ni mtindo wa taasis binafsi huo ovyo sana.mf mtoto akichelewa shule siku moja anatimliwa shule.na baadhi ya sekondari binafsi wanataka watoto waliofaulu sana std 7 au form 2 ubaguzi mtupu.eti zajiita saint
 
Mi nilikua nashangaa sana hii kitu Chuo kinasema kinasaidia wanyonge alafu kinaweka penalty ya laki 1.watu wameteseka sana na hii kitu hongera mkuu Wa Chuo kwa uamuzi uliochukua.
Asante mkuu kwa taarifa
 

Acha kudanganya bwana,mtoa mada.. nani kakudanganya kama mkuu wa chuo cha SAUT amejiuzuru kwa sababu za kijinga kama hizo. Kwa akili zako zilivvyo fupi,wewe ungeweza kuwatetea watu waliokamatwa wanaibia mitihani na wamekiri au unaweza kuwatetea watu wanaopewa ada na kwenda kufanyia biashara halafu hawalipi kwa wakati huku miradi ya chuo kama ukumbi na bweni la wasichana imesimama. Think twice bwana,yule ni dokta na padri pia. Sasa nakufahamisha usioyajua. Makamu mkuu wa chuo kabla hajateuliwa alikuwa Principal wa Bukoba,na Maprincipal wote wa vyuo vya SAUT ni members waalikwa wa BOARD OF TRUSTEE na UNIVERSITY SENATE ambayo ndo hupendekeza hiyo PENALTY na BOARD OF TRUSTEE ambayo ndo chombo cha mwisho cha maamuzi ndo walioamua hao 8 wafukuzwe chuo akiwemo VC wenyewe ambaye pia ni mwenyekiti wa Discipline commette. Sasa atapingaje kitu mbacho alishiriki kukiamua. Uwe unauliza kabla ya kuleta mada, fualitia mchakato uliofanyika kumpata VC na watu walipendekezwa halafu wakakatiliwa akapita yeye,hao ndio sababu ya yeye kujiuzuru sasabu wapo nae mpaka sasa na hawampi ushirikiano wa kutosha..kama upo SAUT unaweza kuwa shuhuda wa kutosha khsu kusimama kwa mambo mengi hasa majengo na kuongezeka kwa madeni ya chuo..na alishajiuzuru toka January ila alikuwa anasubiri idhini ya tume ya maaskofu 4 iliyoundwa kufanya uchunguzi wa sbb alizotoa..
 
Hakuna cha source lecture wala nn hapa,watu ambao huwa anawaambia ukweli ni mapadri wenzake tena sio mapadri wakufunzi,wale wa kawaida tu wanafunzi..malecture watoe wapi hizo taarifa,hawana huo muda ndo mana wanaongea juu juu tu
 

Yan mapadre wanaoishi kwa sadaka za waumini wa kipato cha chini, ndo hao hao wanakubaliana kupitisha sheria kandamizi kwa mtoto wa kimaskini kupata Hak ya kimsingi, Elimu. Waafrika tunakwamishana wenyewe kusukuma gurudum la maendeleo.
 
Excellent!


 

Mtoa mada ni MUONGO MKUBWA, SAUT hakuna lecturer anayeitwa SLAA, ametumia jina la watu vibaya. Tujihadhari na taarifa hizi kwani ni za uongo
 

unafundisha kozi gani hapo mkuu?
 
Mleta mada hii nashindwa kuwa na imani naye. Kama bado ni mfanyakazi pale halafu unaleta mada kama hii na unaweka jina.... sasa wewe utaponea wapi??
 

mkuu hapo umeongea nimekuelewa, mleta mada amejaza propaganda nyingi
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…