mkuu wa it baraza la mitihani asimamishwa kazi.

mlishajiuliza kwanini somo la dini a level si islamic wala divinity watu wanafeli na kitu chengine kwanni watu wengi wanafeli sana alevel tusiwe upande mmoja tu fikiri njema..
 
Bado ninafikiria kuhusu hili la vijana wa Kiislamu kuathirika kisaikolojia! sasa hivi inafikia wakati kijana wa Kiislamu anakwenda Shule au anaingia katika mtihani akijua wazi kuwa nitafelishwa tu!
Sijui serkali itawafidia vipi?!Ni wakati kwa serikali sasa kufanya zaidi kuwarudishia Waislamu wanafunzi na wazazi imani...elimu ni haki yao kama wananchi si msaada na ni wajibu wa Serikali kuhakikisha kuwa raia wake wanapata elimu.
Ni hayo tu!
 
Jamii forums bana mtu anatoa mada ya msingi,angalia pumba zitakazochangiwa teh teh teh!
 
Ni kweli na binafsi naamini kuna hujuma katika wanafunzi wa kiislamu.
Matokeo ya Mtihani wa Islamic Studies baada ya marekebisho yalichapishwa jana na Waziri Dr. Shukuru Kawambwa katika magazeti (mimi niliyaona katika gazeti MWANANCHI). Nimeshangaa baada ya kuona marekebisho ambayo tangazo linasema yamekwishaafikiwa na wakuu wa shule zinazofundisha somo hilo. Asilimia kama 60-70 ni F. Niliona A kama mbili hivi, B na C nazo chache mno. D ni nyingi za kutosha. Sasa najiuliza kabla ya marekebisho matokeo yalikuwaje. Nilitegemea baada ya marekebisho kuwe na msururu wa A na B. Hivi hilo somo ni gumu kiasi hicho au watahiniwa nao ni wagumu. Hata hivyo naungana na walalamikaji dhini ya NECTA. Swala la mtandao unaokokotoa mitihani haufai kuachiwa mtu mmoja peke yake. Unapaswa kukaguliwa kila msimu wa mitihani na watu wengine kuhakikisha kuwa utatoa matokeo sahihi na ya haki. Kwa hilo Dr. Ndalichako anastahili kuwajibika hata kama tatizo hakusababisha yeye binafsi. Halafu najiuliza, hivi mifumo ya komputa ya Tanzania ni tofauti na mingine? Maana hata ile ya Tume ya Uchaguzi nayo mpaka leo haijatoa matokeo sahihi ya uchaguzi wa 2010.
 
nyie wazir wa mambo ya ndani kwa kuwanyima wale masalia viza !

Mkuu Ally Kombo, Asalaam aleykum, kumbe siku hizi viza ya kusafiria ughaibuni inatolewa na waziri wa mambo ya ndani?!, o.k, nijiandaa kwenda hija ijayo, nitawahi kwa Dr nchimbi mapema.
 

Kuropoka ruksa mdomo ni wako
 
mlishajiuliza kwanini somo la dini a level si islamic wala divinity watu wanafeli na kitu chengine kwanni watu wengi wanafeli sana alevel tusiwe upande mmoja tu fikiri njema..
Mimi kichwa kinazunguka nashindwa kupata jibu na mantiki. Hivi mtihani wa Islamic Studies unasahihishwa na watu wasio na elimu/ujuzi wa somo hilo, hasa nikiwa na maana ya Wakristo? Kama ni hivyo hata mimi nitabeba bango kuipinga NECTA. Kwa nini wasimuombe Shehe Mkuu Bin Simba ateue mashehe wakasahihishe mitihani yao ili wasionewe?
 
Kama hazimo, hazimo tu, hata ukijiita John.
 
Alieanzisha Algebra ni nani? katoliki au?
Zaidi Mwislamu. Neno "algebra" ni Kiarabu, wazungu waliijifunza kutoka Waislamu.

(labda ufarijiwe: Waislamu walikopa kutoka Wahindi. Kwa hiyo tusema: mwanzilishaji alikuwa kitu kama Mhindu. Nadhani walitangulia katika maendeleo ya hisabati kwa sababu ya idadi kubwa ya mingu yao - nasikia ni milioni 300 hivi.
Wala "utatu" wala "tawhid" ni hamasisho kubwa kuendelea mbali na namba...)
 


Rufaa ni haki ya Mtahiniwa. kama waalimu wakiislamu walilalamikia matokeoa ni sawa na watahiniwa kulalamikia matokeo. na katika hilo kufanya uchunguzi na kuona dosari na hatimaye kutendea haki watahiniwa si kosa. Mfumo wa kompyuta ni mfumo tu waweza kukosea kama inavyotokea kwa M-Pesa au Benki zetu TZ na Duniani. Hapo si hujuma!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…